St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

Nakumbuka nilikua dar
asa la 5 mkuu wa shule aliagiza mbolea ya thamadi mimi nikaleta ya pumba kumbe kulikua kunakukaguliwa kila mtu anashika mfuko wake kwa asie na thamad adhabu yake fimbo na kupukuchua mahindi ya shule...mweeee unapukuchua mpaka vidole vinaota sugu[emoji23][emoji23][emoji23] najivunia St. Kayumba Kwa kunifundisha kazi na Utii.
 
kule kwenye shule zetu za kajamba nani kuna ml wa kiingereza alkiwaga akiingia kipindi hicho tupo darasa la nne ..darasa linabadilika linakua kama hospitali ya watoto kwenye chumba cha sindano ..Mama yule alikuwa anafinya hakuna mfano .. yan vilikuwa ni viliona majonzi kwenye kipindi cha english mtu unamlaani baba kwanini alikupeleka shule
Kulikuwa na mwalimu mmoja aitwaye Suzan nahisi alikuwa hana mtoto yule.Kwenye English alikuwa anatukamata kwa Dictation na hapo ndio kipigo kilikuwa kikitembea sasa.
 
Back
Top Bottom