Staa wa filamu za Bollywood Sanjay Dutt yupo ndani ya Tanzania kwa sasa

dos.2020

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2009
Posts
11,880
Reaction score
10,372
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na muigizaji mashuhuri wa filamu za Kihindi kutoka nchini India, Sanjay Dutt ambaye ameahidi kushirikiana na Serikali katika kukuza tasnia ya filamu nchini.

Amekutana na msanii huyo leo (Jumatano, Novemba 10, 2021) katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu amesema Serikali itampa ushirikiano wote kuhakikisha msanii huyo anatimiza malengo ya ziara yake nchini.

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwataka wadau wa filamu nchini kutumia ujio wa msanii huyo mkubwa duniani kuimarisha uhusiano pamoja na kujifunza namna bora ya kuboresha kazi zao kupitia yeye na kuweka mipango ya kufanyakazi kwa pamoja.

Pia, Waziri Mkuu amemshukuru msanii huyo ambaye pamoja na mambo mengine ameahidi kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania katika kuendesha mafunzo ya masuala mbalimbali katika tasnia hiyo ikiwemo uandaaji wa filamu kwa kutumia teknolojia ya kisasa hususani kwa vijana.

Naye, Dutt amesema amevutiwa na fursa nyingi zilizoko kwenye sekta ya utalii nchini na kwamba ameahidi kuvitangaza vivutio hivyo na kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa kwenye ramani ya dunia katika masuala ya utalii.

Wakati huo huo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema kupitia ujio wa Dutt, Wizara inategemea kuangalia maeneo ya kimkakati ambayo wanaweza kushirikiana na msanii huyo ikiwemo uandaaji wa filamu, kuongeza wigo wa masoko ya filamu na matumizi ya teknolojia katika kuikuza sekta ya filamu nchini.

Aliongeza kuwa kupitia Chuo cha Sanaa Tanzania (TaSUBa) Dutt ametoa ushauri wa namna bora ya kushirikina ikiwemo kutoa mafunzo kwa wasanii na waandaaji wa filamu “Lengo letu ni kuhakikisha wasanii wetu wanatengeneza filamu ambazo zitakuwa na viwango vya kimataifa na ameahidi kuwaleta wataalamu ili wawasaidie wasanii wetu

255782963_608330700613525_7452765967735870624_n.jpg

254349284_10161404109088082_7888892382562484829_n.jpg
 
Macho yake tu. kwenye movie zake alikuwa bonge la katili ukiingia anga zake..kwenye movie ya Deewar ile scene waliyokuwa wanatoroka jela yeye na wenzie akina Amitabh Batchan kuna mbwa akataka kuwaletea zengwe abweke akamtuliza hapohapo kwa mikono yake
 
Namkubali sana jamaa btw Actors wengi wa kihindi kuanzia wa 20s mpska 80s nawakubali
 
Sanjuu baba!yasemekana sio mtoto wa mzee Sunil Duty mama alichakachua tu mimba ilikua ya mzee Raj Kapoor(Baba yao kina Rish Kapoor)maana mama ake alikua na mahusiano ya wazi na Mzee Raj Kapoor!

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Kipindi nakuwa nimeiba sana hela home niende kwa Mbuluu pale mbauda na machalii zangu kuangalia picha za kihindi za akina Sunjay Dutty, Sunil Shety, Ajay Devgan, San Deol (Kabangi), Akshay Kumar, Mithun Chakarabot, Amrishpur, Amitah Bachan, Karishma Kapoor nawengineo.

Mambo ya utoto.
 
Movie za kihindi siku hizi wanakula denda live nachi zao zina midundo ya pop music
 
Waafrika ni ujinga mtupu diamond akienda india atapifa picha na raisi wao?
Kama raisi wa India akiwa ni shabiki kindaki ndaki wa domo!

Then kuna namna raisi kafanya promo kwenye sector ya utalii,

Inategemeana amkeuja kwa ajili ya swala gani? Kama ni mambo ya Sanaa na raisi ndo mgeni rasmi/mwalikwa lazima wapge picha pamoja..
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na muigizaji mashuhuri wa filamu za Kihindi kutoka nchini India, Sanjay Dutt ambaye ameahidi kushirikiana na Serikali katika kukuza tasnia ya filamu nchini.

Amekutana na msanii huyo leo (Jumatano, Novemba 10, 2021) katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu amesema Serikali itampa ushirikiano wote kuhakikisha msanii huyo anatimiza malengo ya ziara yake nchini.

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwataka wadau wa filamu nchini kutumia ujio wa msanii huyo mkubwa duniani kuimarisha uhusiano pamoja na kujifunza namna bora ya kuboresha kazi zao kupitia yeye na kuweka mipango ya kufanyakazi kwa pamoja.

Pia, Waziri Mkuu amemshukuru msanii huyo ambaye pamoja na mambo mengine ameahidi kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania katika kuendesha mafunzo ya masuala mbalimbali katika tasnia hiyo ikiwemo uandaaji wa filamu kwa kutumia teknolojia ya kisasa hususani kwa vijana.

Naye, Dutt amesema amevutiwa na fursa nyingi zilizoko kwenye sekta ya utalii nchini na kwamba ameahidi kuvitangaza vivutio hivyo na kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa kwenye ramani ya dunia katika masuala ya utalii.

Wakati huo huo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema kupitia ujio wa Dutt, Wizara inategemea kuangalia maeneo ya kimkakati ambayo wanaweza kushirikiana na msanii huyo ikiwemo uandaaji wa filamu, kuongeza wigo wa masoko ya filamu na matumizi ya teknolojia katika kuikuza sekta ya filamu nchini.

Aliongeza kuwa kupitia Chuo cha Sanaa Tanzania (TaSUBa) Dutt ametoa ushauri wa namna bora ya kushirikina ikiwemo kutoa mafunzo kwa wasanii na waandaaji wa filamu “Lengo letu ni kuhakikisha wasanii wetu wanatengeneza filamu ambazo zitakuwa na viwango vya kimataifa na ameahidi kuwaleta wataalamu ili wawasaidie wasanii wetu

View attachment 2004774

View attachment 2004775
Huyu hana lolote kaja kutalii tu na kuondoka

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom