Comrade!ikitokea hatma imekudondokea na hatmae ukawa mkuu wa kiti kikubwa katika nchi hii!Hili nalo lipatie ufumbuzi kama ninavyoandika sasa!
Kumbuka nchi yetu Haina tatizo la ajira Bali sera mbovu za ajira ndio zimetufikisha tulipo,unawezaje kumuajiri mtumishi ajira ya maisha !?wakati Kuna wimbi la vijana wasomi wanahitimu kila mwaka!!?
Inajulikana kabisa mtumishi mwenye miaka zaidi ya 45 performance yake hushuka kutokana na majukumu mengi ya kifamilia na uchovu wa muda mrefu plus magonjwa yasiyoambukiza,wastaafishe walipe mafao Yao waendeleze ujasiria mali ili kutoa nafasi kwa damu changa yenye ari ya mapambano ya kutoa huduma kwa jamii!!
Sasa basi,baada ya kuwastaafisha utawaajiri vijana Kwa mikataba ya miaka mitano mitano,boresha mishahara yao walau take home ya laki Saba Kwa mwezi!ili wapate mitaji ya kutosha baada ya kumakiza mikataba Yao utawaajiri wengine!!
Tulikaa tukafanya hesabu zifuatazo;-
700000×12 (mwaka mmoja)=8,400,000×5(miaka mitano ya mkataba wa ajira) =42,000,000 .
Kama kijana atatumia walau nusu ya million arobaini na mbili kama matumizi kipindi cha mkataba wake,zinazobaki atajiajiri na hiyo itachochea huo uchumi kukua kila baada ya miaka mitano!!
Karibu nusu ya watumishi wanna miaka 45 na zaidi,itasaidia pia serikali ku save fedha za mishahara coz wenye umri huo wengi na vyeo vikubwa na mishahara mikubwa kuliko ajira mpya,itasaidia serikali kupata fedha Kwa ajili ya matumizi mengine!!!!
Badili sera ya ajira comrade,kilichopo sasa hakina tija,na hao watakaobaki waliochini ya umri 45 walioajiriwa Kwa mfumo wa ajira wa maisha nao wakifika 45 nao wastaafishwe waajiriwe wapya ,Hadi utakapo maliza awamu yako watumishi wote watakua chini ya ajira ya mkataba wa miaka mitano mitano!
Exception itatokea Kwa wale wenye performance ya zaidi ya 95% wanaweza kuongezewa mkataba mwingine kama motisha kwao mwisho iwe miaka 10.
Mafao ya kuwastaafisha unaweza utayapata kwa kushusha mishahara ya wanasiasa kama mpanho KAZI wa muda mfupi,badala ya million 18 utawalipa walau million kumi kwa mwezi hizo million 8 mara idadi ya wabunge karibu 300 ni fedha zinazo tosha kabisa kulipa mafao!!
Naamini hili seke seke la ICC linaweza kukupa mwanya wa kuvunja bunge na serikali iliyopo na ikapatikana serikali ya mpito ya katiba mpya,fedha zilizokua zinalipwa mshahara wabunge na mawaziri zitumie ipasavyo kipindi hicho kufanikisha hilo!!
Nakutakia utekelezaji mwema wa majukumu yako!!
Naomba unikumbuke walua niwe mshauri wako wa karibu kwenye sekta nyeti ya ajira na Tamisemi!!
Kama hunijui,watafute watakujuza,hao wakitaka kunipata watanipata tu Kwa Nia njema na sio kivile kama ambavyo imekuwa desturi Yao sasa!!
Kazi na utu,tunasonga mbele!