Stamina ameniangusha kwa hili

Stamina ameniangusha kwa hili

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Kwanza kabisa nimpongeze Stamina kwa kupata deal la parimatch, jamaa Ni mbunifu Sana na anafanya kazi nzuri Sana nimefurahi Sana Jamaa kupata Hili deal maana jamaa alikuwa apati kabisa deal za kuwa ambassador wa makampuni ila safari hii Mungu amemuona.

Jingle aliyofanya la parimatch Ni nzuri lakini Kuna kitu ameniangusha Sana kwenye hiyo jingle sijui Ni kwa sababu ya mchecheto au kukosa elimu ya haya masuala ameisifia parimatch na huku akiponda makampuni mengine ya kubet hii sio sawa kabisa hivi kulikuwa na haja gani ya kuponda makampuni mengine si ungesifia parimatch Pekee bila kuponda makampuni mengine angepungukiwa Nini? Hiyo njia inaweza kusababisha ukakosa deal lingine la kampuni ya kubet unazani kampuni Kama sports pesa inaweza kuvutiwa Tena kukuitaji?

Ngojea nimtolee mfano hapa hapa bongo ajifunze haya masuala Diamond alisign contract na Coca-Cola na jingle alilolitengeneza aliisifia Coca-Cola bila hata kuponda makampuni mengine ya kinywaji Je Kama angeponda makampuni mengine ya soda unazani angepata deal la Pepsi kweli?
 
Uzi wa stamina na domo katajwa aiseeee usukule raha
Ukisikia matukio kama "Leaving Neverland" ya Michael Jackson au DocuSeries ya "Surviving RKelly" unaweza kushangaa inatokeaje watu wanakubali kufungiwa ndani na msanii huku wakilawitiwa na wanakaa kimya.

Ila Ukiyaona Mahaba ya mleta mada kwa Domo unaona kabisa suala hilo linawezekana kirahisi kabisa.
 
Ukisikia matukio kama "Leaving Neverland" ya Michael Jackson au DocuSeries ya "Surviving RKelly" unaweza kushangaa inatokeaje watu wanakubali kufungiwa ndani na msanii huku wakilawitiwa na wanakaa kimya.

Ila Ukiyaona Mahaba ya mleta mada kwa Domo unaona kabisa suala hilo linawezekana kirahisi kabisa.
Kwahiyo kinachokuuma sio ushauri wangu kwa stamina ila Ni kumtaja mondi tu?
 
Si usimame uende ulipokuwa unaelekea au amekuangusha akakuvunja miguu akiii
 
Wewe umeangushwa unaweweseka ila mwenzio kala mpunga wake katulia tuli
 
Back
Top Bottom