Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kwa muda mrefu sasa huyu mwanamuziki kila nikikutana na nyimbo yake analalamikia mapenzi tu, sana hasa yanayohusu upande mmoja tu wa mke au mwanamke.
Sina uhakika kuna nyimbo nyingine alizoimba ambazo sio ulalamishi wa kupigwa na mwanamke katika mapenzi na mimi ndiye sijakutana nazo ila huyu bwana analalamika sana katika nyimbo zake kuhusu mke, halafu nyimbo zenyewe ni ndefu sana na kwa mfumo wa kutoa hotuba au mawaidha zaidi kuliko kuimba.
Kuna wakati nilisikia huyu bwana aliibiwa au alichukuliwa mke na mchezaji wa Simba, isije ikawa bado haja "move on" na haya ni matatizo ya kisaikolojia ambayo hayajapoa, kama ni hivyo BASATA hapa wana kazi ya ziada ya kufanya kuhakikisha mdau wao anakaa vyema kiakili.
Vinginevyo kama amefuma soko lake la watu wanaopenda muziki huo wa malalamiko mfano wale wa "kataa ndoa" na hilo soko linamlipa vizuri kila la kheri kwake, itakuwa ni ubunifu mzuri tu pia.