Kumbe hata Agoro Anduru alishafariki, so sad. Hadithi za Kiswahili za magazetini zilizonivutia wakati huo ziliandikwa na huyu Anduru (RIP), Ben Mtobwa, Hammie Rajab, Sam Kitogo (napenda nisikie kuwa hawa bado wako hai). Siku hizi hakuna gazeti la kiswahili lenye hadithi nzuri, ule uandishi umeondoka na wahusika.
Agoro Anduru=marehemuGazeti lake liliitwa Mfanyakazi, kila wiki nilihakikisha napata nakala yangu. Humo ndani pia kulikuwa na hadithi za mtunzi maarufu Agoro Anduru, sijui kaishia wapi siku hizi. Na column fulani ndogo ya vichekesho iliyokuwa ikiitwa Nipashe, yenye picha ya sikio kuubwa.
Nilisikitishwa sana na kifo cha Stan Katabaro, Mungu amweke pema na aisaidie familia yake, Amen.
genekai,Hawa ndo walikuwa waandishi bwana, ila Kubenea naye namkubali, Mnamkumbuka Kabendera Shinani? Naye aliuwawa kule BK kwa kina IWE na alikutwa anaelea ziwani. Wanasema naye alikuwa akifuatilia kashafa moja ya utekaji wa magari mkoani Kagera ambapo kigogo mmoja huko mkoani alikuwa anahusika!
Jamani mnanikumbusha mbali mno gazeti la mfanyakazi na motomoto ila siku hizi tumebaki utadhani tumelogwa na hela na udaku magazeti yananunuliwa ovyo na wanahabari wanahongwa baadhi yao mpaka yanawakuta ya Jerry Muro. tuwaombee Mungu hawa wachache waliobaki wasije wakalogwa tukawa mamluki wa mafisadi
... Tusimsahau John Rutayisingwa.
Huyo bwana ndiye aliyekuwa mhimiri wa kashfa ya Loliondo kabla ya kutolewa Wizara ya Utalii na kupelekwa kuwa RC Singida. Hivi siku hizi yuko wapi huyo Mgumia?
RIP Katabaro.....Namkumbuka sana jinsi alivyokuwa mwandishi mzuri sana na asiye na woga.
Wadau naomba pia mkumbuke jamaa mmoja anaitwa Anthony Ngaiza ambaye aliwahi kuwa editor wa Family Mirror kwenye miaka ya 1992/93 kabla ya kuhamia MCT. Tunahitaji kweli kuwakumbuka hawa jamaa!
Alikufa ghafla!.
Kumfananisha Kubenea na Stan, ni kumpandisha tuu chati Kubenea, Stan alikuwa akiandika investigative journalism kwenye developing story, Kubenea anaandika udaku kwenye medani za siasa, sio uchunguzi in a really sense ya uchuguzi. Waliotaka kufuata nyanyo za Katabalo, ni This Day na Kulikoni, walioanza, wakati wakifuatilia story ya Rada.
nani anakumbuka issue ya lolionda gate. ukiijua hiyo vema utakuwa unamjua katabaro tunayemzungumza. alikauka ghafla mpaka wa leo watu makini wanasikitika jamani katabaro. where is he We miss him so much. R.I.P
Je, mnakumbuka na ile kashfa ya RIO? Kwenye mkutano wa Mazingira Duniani ulifanyika BRAZIL (Rio de Janeiro)
Kwahakika hakuna kama STAN KATABALO.
Kashfa ya LOLIONDO ilimhusu sana sana ABUBAKAR MGUMIA......
Kubenea is an overrated semi-literate Katabalo wannabe kama alivyosema muandishi mmoja wa habari.
BTW, I believe the name is Stanley Katabalo, not Katabaro.
Enzi hizo Jumamosi asubuhi lazima ununue Mfanyakazi hata kwa foleni. Mfanyakazi used to be a hot paper (as hot as it could get under Nyerere) nakumbuka kusoma court proceedings za Kesi ya Uhaini na quips za Muccadam Lakha. Hata "Amini Usiamini" tu ilikuwa very interesting.
ndimara tegambwage,ansibert ngurumo,paschal mayega,lakini bado katabalo is still no one.