Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Mkuu enzi hizo kulikuwa na heshima ya taaluma zote. Stan Katabalo na Mfanyakazi waliji tofautisha sana kwenye uandishi wake. Mkono wa kifo chake yupo pia Abrahaman Kinana akina JK, Ndolanga and the likes kwa Loliondo Gate.

Mimi naomba tumkumbuke kila tukikumbuka kama mwandishi JASIRI ambaye labda kama hakuwa wa kwanza basi mmoja wa wawili bora.

Nawakumbusha tu miaka ya 60 alitokea mwandishi na mtangazaji mwingine (Marehemu Melek Kangero) alimkosoa sana Mwl. Nyerere akapata life Ban ya ajira kwenye ofisi yo yote ndani na nje ya Tanganyika.

Watawala wetu watateseka sana na ukandamizaji wa Fikra
 
STAN mwandishi mahiri wa habari za kiuchunguzi namkumbuka sana wakati huo miaka ya tisini,je tanzania bado inao waandishi wenye KUTHUBUTU? Kuwaambia viongozi wako UCHI
 
Huyo bwana ndiye aliyekuwa mhimiri wa kashfa ya Loliondo kabla ya kutolewa Wizara ya Utalii na kupelekwa kuwa RC Singida. Hivi siku hizi yuko wapi huyo Mgumia?


RIP Katabaro.....Namkumbuka sana jinsi alivyokuwa mwandishi mzuri sana na asiye na woga.

Wadau naomba pia mkumbuke jamaa mmoja anaitwa Anthony Ngaiza ambaye aliwahi kuwa editor wa Family Mirror kwenye miaka ya 1992/93 kabla ya kuhamia MCT. Tunahitaji kweli kuwakumbuka hawa jamaa!

Stan Katabaro alikuwa mwandishi mahiri sana, ninaposikia hii sekeseke ya Loliondo sasa hivi huwa namkumbuka. Abubakar Mgumia naye ni marehemu.
 
Stan Katabaro alikuwa mwandishi mahiri sana, ninaposikia hii sekeseke ya Loliondo sasa hivi huwa namkumbuka. Abubakar Mgumia naye ni marehemu.


Ahsante sana COPPER,

Huyu Mgumia na Mwinyi walitufanyia kosa kubwa sana ambalo huko mbele ya safari tutakuja kuwafuatilia hata kwa documents ili tujue walichokifanya.

Loliondo itabaki kuwa jipu la ajabu sana kwa Watanzania.
 
Last edited by a moderator:
Kama ambavyo itatuchukua miaka 100 kumpata raisi kama mwalimu Nyerere ndivyo ambavyo itatuchukua miaka 100 kumpata Stan Kabalo mwingine katika uandishi wa habari. Stan Katabalo alikuwa ni zaidi ya mwandishi wa habari. Leo hii maripota wanajiita waandishi wa habari wakati hakuna cha maana wanachofanya zaidi ya kugombania posho/bahasha na kujisajili kwenye kambi (mitandao) zinazogombea uraisi 2015 wakati Watanzania hasa vijijini wanahitaji kuelimishwa mambo ya msingi na kalamu za waandishi wa habari.
 
Stan Katabaro (RIP); kifo chake hakina tofauti na mateso ya Dr. Ulimboka na mhariri Absalom Kibanda, lakini sasa mzimu wake umerejea kule Loliondo, Mwigulu Nchemba na Hamisi Kagasheki hatujajua nani atakuwa mhanga wa Loliondo gate 2 ?!
 
:yo:Tunamuenzi sana na nadhani he inspired a number of current journalists kaka lakini unadhani hawawezi kufanya kama alivyo fanya? roho hii tayari lakin mwili dhaifu! Gazeti la mfanyakazi kaka lilikuwa si la mtu mmoja kama sasa hivi! kila mwandishi atakachojarinu kuandika lazima kiwe na tija na mashiko siyo kwa taifa kaka bali kwa mwenye chombo! Kaka mizumu ya katabalo iko kibao kwa sasa ila hakuna aliyetayari kuihost kaka!
 
Agoro Anduru (The Temptation) ni Marehemu pia (RIP)

Stan hawezi kulinganishwa na mwandishi yeyote katika hii decade 2000 - 2010! Kubenea, Mbwambo, e.t.c they are no where near - kumbuka kuwa wakati the so called "uhuru wa vyombo vya habari" ulikuwa mdogo sana!

RIP Stan K.

Agoro Anduru au Aggrey Andrew! This is living and other stories! Jamaa alikuwa mahiri sana. Mungu ampe pumziko la milele.
 
Agoro Anduru au Aggrey Andrew! This is living and other stories! Jamaa alikuwa mahiri sana. Mungu ampe pumziko la milele.
Kweli tumepotea kama Taifa tunahitaji kila mtu na familia yake ajenge uwezo watoto kusoma vitabu maana hizi audio-visual ni nzuri kwa mafunzo ila haziongezi uwezo wa ubongo kufikiria kwa kina kwa kuwa unasikiliza na kuona tofauti na kusoma lazima ita involve na kutafakari kwa kina, siku hizi ukisikia mtu anazungumzia vitabu utasikia ni vya watu wa nje, kweli long time tulikuwa tuna hazina ya waandishi wa simulizi siku hizi tumebaki na waandishi wetu wa story za kwenye magazeti ya rangirangi. Aisee Baba_Enock amenigusa na kitabu cha Temptation cha marehemu Agoro Anduru
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom