Stand up comedy: Kenya kuna Eric Omondi, Uganda kuna Kansiime na Bongo kuna nani?

Stand up comedy: Kenya kuna Eric Omondi, Uganda kuna Kansiime na Bongo kuna nani?

Haha kuna wale awanaizurura na masinzi ya mkaa usoni wanaweka matambara makalioni
Wengine wanadhani mwanaume kuvaa kama mwanamke ndo kuchekesha kama wakina joti na wale vijana wa Eatv
 
Huyo pilipilimanga ndio hafai kabisa kuitwa comedian mtu anakuwa kazi yake ni ko copy NASWA YA WAKENYA ambao ni ya kibubububu yeye anajifanya anafafanua atunge zake aache kuharibu sanaa za watu wengine
 
Mpoki ana uwezo ila wengine wote hawana uwezo...Kenya wana hazina kubwa sana.. kuna prof Hamo na wengine
Kuna MCA TRICK naye ni noma Kenya...Bongo standy up comedy hamna wanaiga tu...wanaofanya Kenya tena wengi ni graduates wanakuwa creative na upeo wao ni mkubwa...
Bongo Comedian wengi hawajaenda shule labda Mc Pilipili alikuwa mwalimu ila na yeye ndiyo hana kipaji kabisa
 
Stand up comedy Bongo imeanza kupata nafasi kwa kasi lakini kuna changamoto kubwa hasa ya kuwa na wachekeshaji mahiri watu kama.

Mc pili pili yeye anajitaidi lakini anarudia rudia sana aina ya vichekesho vyake kwenye events tofauti.

Idris Sultan huyu jamaa sidhani kama ana talent ya kuchekesha japo kwenye social media anawafuasi wengi, nimeona baadhi ya show zake bado sijaona kiwango.

Stave Nyerere huyu jamaa nae si haba japo anachekesha kwa kuponda watu(anawachamba kama wadada wanavyoita).

Je, mbongo tunaweza kuwa na comedian wazuri waliofikia level za Eric Omondi wa Kenya au Anne Kansiime wa Uganda?

Kati ya hawa yupi anaweza fika huko
- Mpoki
- Idris Sultan
- Stive Nyerere
- Mc Pilipili
- Katarina wa Karatu
- Dogo pepe
- Joti
- Masanja Mkandamizaji
- Bambo
Yaani ktk list yako umeshindwa kumkumbuka hata Mkude simba aka Kitale? Hujamtendea haki kwakweli...
 
Back
Top Bottom