Stand up comedy: Kenya kuna Eric Omondi, Uganda kuna Kansiime na Bongo kuna nani?

Stand up comedy: Kenya kuna Eric Omondi, Uganda kuna Kansiime na Bongo kuna nani?

kwenye ubunifu wa Tz zero kabisa, wanasahau kuwa dunia ya leo ya teknolojia huwezi kumuiga Kevin Hart kila kitu halafu utegemee kuvutia maana hakuna atakaeona kipya ambacho hawajakiona tayari kwenye Youtube. Kuna video ya waarabu ili trend hivi karibuni ya mchunga mbuzi kuita majina mbuzi wako zizini, hata wiki haikupita Joti nae kasambaza ya kwake ambayo amecopy A to Z and that's as far as being creative goes for us.

Duh hawaoni aibu kucopy na kukubali hawana kipaji bali wanalazimisha...kweli inaboa na kupoteza mashabiki kwa mtu kama amekutana na hiyo ya kukopi...tena miaka hii.
 
Nimejaribu kucheki stand up comedy za idris sultan..jamaa is a fake, hachekeshi ata kidogo.
 
Tusiwalaumu sana Kuna wengine wazuri kama joti, mpoki ila tatizo lugha ya kingereza na Kuna wengine wanajua lugha ila hawajui kuchekesha kama mc pilipili, evance na idris nikiwatizamaga hata sioni wanachochekesha.

Umemaliza lugha ndio tatizo... Kutoa kichekesho chake kwenye Kiswahili kiende kwa kingereza hapo ndio majanga
 
Honestly, mimi hata huyo eric omondi huwa hanichekeshi....Kansiime clip zake chache zinachekesha.....Kibongo bongo Kitale (Mkude Simba) huwa anajitahidi sana...Japo sidhani kama stand up anaziweza
 
Stand up comedy ni kitu cha tofauti. Ukifanikiwa kuigiza movie yenye vichekesho haimaanishi utakuwa vizuri kwenye stand up comedy.

Stand up comedy inataka uwe na uwezo wa kubadilisha materials ukiwa stejini hivyo inahitaji kipaji haswa as hakuna cha editing pale.

Unaweza enda kuchekesha watu mahali ukakuta materials zako zote haziko relevant kwa audience uliyokutana nayo na hili unalitambua unapokuwa jukwaani hivyo kupaswa ku-switch ghafla. Ndio maana wataalamu wanakwambia stand up comedy ni ngumu sana. Siyo ya kuamka na kusema mimi ni stand up comedian.
 
Back
Top Bottom