Stand up comedy watanzania wanahitaji kuelimishwa watofautishe Sanaa ya uchekeshaji na uropokaji

Stand up comedy watanzania wanahitaji kuelimishwa watofautishe Sanaa ya uchekeshaji na uropokaji

Binafsi nilikuwa natazama pamoja na wife ,mke wangu akasema unaangalia ujinga huo.Yaani kwanza hawajui hata adhira iliyopo,eti unataja kabisa Mhe.Rais kwenye comedy hata hujui kuwa Ile ni Taasisi nyeti,ni bora hata angetumia njia nyingine kuchekesha kuliko kumtaja Rais.Eti Mhe Rais Kajala karudiana na Harmonize,huo ni ucheshi?
Sema Mababu umezingua kinoma, yani hadi Mama watoto anakusanua huu ni upuuzi ndo unastuka?
 
Binafsi nilikuwa natazama pamoja na wife ,mke wangu akasema unaangalia ujinga huo.Yaani kwanza hawajui hata adhira iliyopo,eti unataja kabisa Mhe.Rais kwenye comedy hata hujui kuwa Ile ni Taasisi nyeti,ni bora hata angetumia njia nyingine kuchekesha kuliko kumtaja Rais.Eti Mhe Rais Kajala karudiana na Harmonize,huo ni ucheshi?
Yaan watoto wanajifunza nn
 
Hawa ni vijana wenzangu wanajitafta!

Inchi imepanua sana wigo wa ajira kupitia sanaa! Serikali inatumia kila mbinu kuwainua vijana hata kwa motisha!

Stand up comedy kuna vijana wachache sana tanzania wenye ubunifu wa kisanii!
Wengi wao wanaropoka tu pasipo kuchuja maneno! Sijui ni bangi kichwani.

Mbele ya TV maudhui yao mengi ni ya uchekeshaji wa NGONO NGONO NGONO TUPU yaani unashindwa kuelewa hawa vijana hawajui vipindi tunazama watu wa maana kabisa tukiwa na watoto wadogo?

Vijana mnapopewa nafasi kumbukeni pia jamii inawatazama! Msiropoke upuuzi kisa mko live!

Mnachokifanya mtailazimisha serikali ianze kuchuja maudhui yenu jambo linaloweza kuua vipaji vyenu kama stand up comedy.

NGONO NGONO NGONO tupu mkimaliza mnasimulia UMBEA UMBEA UMBEA mtupu mkizani ndo usaniii huo?

Sanaa ni jambo la ubunifu hata kama munasimulia mapenzi katika ucheshi basi jitahidini kuyaweka katika style ya usaniii! Siyo ALIPOMTONGOZA ALIMUINGIZA GHETO AKAMWAMBIA NIKULE WIMA AU .....yaani uchafu tupu ( watoto wanasikia, wakwe wanasikia mnaboa sana)

Tumieni hata story za uongo zinazochekesha kama WENZENU Wafanyavyo huko mataifa!

Msishangae Siku wakialikwa wasanii kutoka inje kuja kuchekesha mtasema wazawa mnatengwa!

FULANI WAMERUDIANA siyo ucheshi, nipe namba nimkomoe X WANGU siyo ucheshi...

vijana wenzangu mnayo nafasi ya kubadilika! Chekesheni lakini muwe na staha na mjue tunatazama kuna watoto, wakwe, walokole na wapagani n.k.

komedi ni sanaa siyo uropokaji
Hawa comedian wetu wamejitengeza wenyewe bila mfumo wowote rasmi hadi kufikia hatua ya kumweka Rais wa nchi mbele yao, hawajapikwa na taasisi yoyote. Tuwapongeze kwa kutumia ujinga wetu kama Taifa.

Sasa udhaifu wao ni matokeo ya mifumo mibovu ya elimu yetu. Kama hawawezi kumtofautisha Rais na Mwijaku au Manara, hiyo ni kidokezo kuwa jamii ina ujinga mwingi na wao ni matokeo ya ujinga wa Taifa Letu.

Lakini pia nyuma ya ujinga huu ambao Njerere JK aliutambua kama adui, ndio fursa kwa chama twawala kuendelea kushika hatamu.

Kama kiongozi wa nchi ameamua kujiondolea stress za uongozi kupitia comedians, tumkubalie avune matokeo ya ujinga ulioshamiri katika jamii.
 
Nasikia kuna dogo kazingua jana! Mwenye clip ya huyo dogo aitupie.
 
standup comedy wanaona vichekesho vyao ni mapenzi tuu.... sijui hawajifunzi kwa wenzao wa kenya... tena vile vidada vichekesho vyao ndio hata aibu kusikiliza ukiwa na familia
 
Bongo kitu pekee unaweza kuangalia na familia ni mpira tuu.... vingine vyote unaweza kuaibika na familia yako
 
Alafu zile sio freestyle..
Yaani ni arranged kabisa ni scene na wamefanyia mazoezi aiseeee.

Daaah mi mwenyewe nimeona nimechoka aiseee.

Ucheshi unaweza kuuweka kivyovyote vile ila unapotoa huo ucheshi zingatia hv vtu
1/Muktadha
2/Rika
Kabisa mkuu
 
Comedians Wamefanya kile wabongo wanachokipenda, wabongo wanapenda upumbavu tuu.

ILa yule dogo isaa amezingua knoma, anaongea utadhani yupo na wapuuzi wenzake.
 
Je wana followers na watu wanacheka ?; Kama ndio basi angalau wanakidhi kigezo cha kujipatia mkate....

To each their own...; hususan karne hii ya Video on Demand unaweza kuchagua utakacho na usichotaka...
 
Halafu yule kijana angeweza kumchekesha Mh. Rais bila kumtaja yeye waziwazi. Pale ni kama alikuwa anamtania Rais ili watu wacheke. Kinyume chake angetania watu wengine ili kumchekesha Rais...! Hakufanya Fair kabisa.
Huyo mama yenu ndio hakuwa fair Kwa huyo kijana, badala akatafakari mambo nyeti ya nchi yeye anazurura kwenye hizo birthday parties, shame!
 
Ndu
Hule dogo hana akili alichukulia kipindi kile ndo mazoea!
Samia bado ni Rais hutakiwi kumzoea na kutunga comedy inayomlenga isiyokuwa na tija hata kidogo!
Ndio ajifunze kutulia ikulu na kutafakari mambo ya nchi!
 
Mi siangaliagi stand up comedy za hawa wabongo maana nikiangalia badala nicheke huwa naishia kuwaonea huruma hakuna wanacho chekesha.
 
Back
Top Bottom