Sema Mababu umezingua kinoma, yani hadi Mama watoto anakusanua huu ni upuuzi ndo unastuka?Binafsi nilikuwa natazama pamoja na wife ,mke wangu akasema unaangalia ujinga huo.Yaani kwanza hawajui hata adhira iliyopo,eti unataja kabisa Mhe.Rais kwenye comedy hata hujui kuwa Ile ni Taasisi nyeti,ni bora hata angetumia njia nyingine kuchekesha kuliko kumtaja Rais.Eti Mhe Rais Kajala karudiana na Harmonize,huo ni ucheshi?
Yaan watoto wanajifunza nnBinafsi nilikuwa natazama pamoja na wife ,mke wangu akasema unaangalia ujinga huo.Yaani kwanza hawajui hata adhira iliyopo,eti unataja kabisa Mhe.Rais kwenye comedy hata hujui kuwa Ile ni Taasisi nyeti,ni bora hata angetumia njia nyingine kuchekesha kuliko kumtaja Rais.Eti Mhe Rais Kajala karudiana na Harmonize,huo ni ucheshi?
Hawa comedian wetu wamejitengeza wenyewe bila mfumo wowote rasmi hadi kufikia hatua ya kumweka Rais wa nchi mbele yao, hawajapikwa na taasisi yoyote. Tuwapongeze kwa kutumia ujinga wetu kama Taifa.Hawa ni vijana wenzangu wanajitafta!
Inchi imepanua sana wigo wa ajira kupitia sanaa! Serikali inatumia kila mbinu kuwainua vijana hata kwa motisha!
Stand up comedy kuna vijana wachache sana tanzania wenye ubunifu wa kisanii!
Wengi wao wanaropoka tu pasipo kuchuja maneno! Sijui ni bangi kichwani.
Mbele ya TV maudhui yao mengi ni ya uchekeshaji wa NGONO NGONO NGONO TUPU yaani unashindwa kuelewa hawa vijana hawajui vipindi tunazama watu wa maana kabisa tukiwa na watoto wadogo?
Vijana mnapopewa nafasi kumbukeni pia jamii inawatazama! Msiropoke upuuzi kisa mko live!
Mnachokifanya mtailazimisha serikali ianze kuchuja maudhui yenu jambo linaloweza kuua vipaji vyenu kama stand up comedy.
NGONO NGONO NGONO tupu mkimaliza mnasimulia UMBEA UMBEA UMBEA mtupu mkizani ndo usaniii huo?
Sanaa ni jambo la ubunifu hata kama munasimulia mapenzi katika ucheshi basi jitahidini kuyaweka katika style ya usaniii! Siyo ALIPOMTONGOZA ALIMUINGIZA GHETO AKAMWAMBIA NIKULE WIMA AU .....yaani uchafu tupu ( watoto wanasikia, wakwe wanasikia mnaboa sana)
Tumieni hata story za uongo zinazochekesha kama WENZENU Wafanyavyo huko mataifa!
Msishangae Siku wakialikwa wasanii kutoka inje kuja kuchekesha mtasema wazawa mnatengwa!
FULANI WAMERUDIANA siyo ucheshi, nipe namba nimkomoe X WANGU siyo ucheshi...
vijana wenzangu mnayo nafasi ya kubadilika! Chekesheni lakini muwe na staha na mjue tunatazama kuna watoto, wakwe, walokole na wapagani n.k.
komedi ni sanaa siyo uropokaji
Waongeze ubunifu wanaweza lakini uropokaji iwe mwiko
Kabisa mkuuAlafu zile sio freestyle..
Yaani ni arranged kabisa ni scene na wamefanyia mazoezi aiseeee.
Daaah mi mwenyewe nimeona nimechoka aiseee.
Ucheshi unaweza kuuweka kivyovyote vile ila unapotoa huo ucheshi zingatia hv vtu
1/Muktadha
2/Rika
Kabisaa yaan labda vijana wapewe nafas moja nyingine watajirekebishaBongo kitu pekee unaweza kuangalia na familia ni mpira tuu.... vingine vyote unaweza kuaibika na familia yako
Kweli niliangalia issu ya KALAMU, dooh hawa vijana hakuna creativity kabisa, ukipewa nafasi adhimu kama ile ndio pakufanya vizuri ili kujiongezea soko lako, but 🚮Naunga mkono hoja....kuna muda mpka aibu unaipata huku mbali je wa pale ukumbini.
Hahahaha yaani mambo yao shagalabagala tu ngoja liende!Comedians Wamefanya kile wabongo wanachokipenda, wabongo wanapenda upumbavu tuu.
ILa yule dogo isaa amezingua knoma, anaongea utadhani yupo na wapuuzi wenzake.
Hahahaha bora Leonardo kuliko yule dogo Said
View: https://youtube.com/shorts/vJT8nriAHDQ?si=pZoQ72H8XOsDXIyq
Hii sio comedy asee!!!!
Rais nae kawa mwepesi sana.
Hule dogo hana akili alichukulia kipindi kile ndo mazoea!Hahahaha bora Leonardo kuliko yule dogo Said
Huyo mama yenu ndio hakuwa fair Kwa huyo kijana, badala akatafakari mambo nyeti ya nchi yeye anazurura kwenye hizo birthday parties, shame!Halafu yule kijana angeweza kumchekesha Mh. Rais bila kumtaja yeye waziwazi. Pale ni kama alikuwa anamtania Rais ili watu wacheke. Kinyume chake angetania watu wengine ili kumchekesha Rais...! Hakufanya Fair kabisa.
Ndio ajifunze kutulia ikulu na kutafakari mambo ya nchi!Hule dogo hana akili alichukulia kipindi kile ndo mazoea!
Samia bado ni Rais hutakiwi kumzoea na kutunga comedy inayomlenga isiyokuwa na tija hata kidogo!