Tetesi: Standard Chartered Bank kufunga operation zake Tanzania

Tetesi: Standard Chartered Bank kufunga operation zake Tanzania

Kuna hii habari kwamba Standard Chartered Bank wanataka kufungasha vilago ikoje?

Kama ni kweli, Juzi kati tuliambiwa, mama kayafufua mabenki hili halijafufuka?.

NB; Standard Chartered Bank ni banker wangu
Lazima waondoke kama riba za mikopo (interest rates ) za CRDB na NMB zitakuwa chini ya asilimia 10. Mabenki kama Standard chartered walizoea 23% na kuendelea. Sasa kipi bora kwa mwananchi riba ya mkopo ya asilimia 9 au 23 .
 
Kwa sasa Tanzania siyo nchi salama sana kwa wawekezaji, kauli ya mtu mmoja ndio sheria. Huyo mtu akitamka kila kitu kinabadilika, investors wanataka kuwa na uhakika na uwekezaji wao.

Huwa tunaona katiba mpya inawahusu wanasiasa tu, ajira za watu zinaenda kuondoka hapo, na hasara zingine kibao...!
Kuna watu wanaweza wasielwe. Lakini ukweli ni kwamba bila ya mfumo bora wa utawala, hatutapata genuine investors.

Tanzania mpaka leo, based on Australia Economic Intelligency report, ni nchi ambayo siyo salama kwa mitaji ya nje. Report hii ilitolewa wakati wa utawala wa Magufuli, na mpaka leo haijabadilika kwa sababu kimsingi hakuna kilichobadilika. Sheria za nchi na sheria za uwekezaji ni zile zile.
 
Tigo imeondoka Tanzania, kuna ajira imepotea? Standard Charted kuondoka, haimaanishi benki imefilisika, hapana, bali wanauza share zao. na benki inaendelea kama kawaida.

Any way, naona umedaka la ajira tu ukahangaika nalo, je nchi yetu ni mahala salama kwa uwekezaji mkubwa wakati huu ambao kauli ya kiongozi mkuu ni sheria?
 
"Make the lie big, make it simple, keep saying it and eventually they'll believe it"

Kelele za kufungua nchi zikishachuja,nchi itakuwa imeshajifunga kisawasawa!
 
Alia toa taarifa anaponda na kufaurahia wanaochangia nao wanaponda na kufurahia awajui kwamba hapo taifa linapata hasara kwa kukosa kodi na baadhi ya raia wake wanakosa ajira .vibaya hivyo nchi yetu sote tusii ishi kwa visasi aliyekosea ameshaaenda sasa tuangalie mbele
 
Any way, naona umedaka la ajira tu ukahangaika nalo, je nchi yetu ni mahala salama kwa uwekezaji mkubwa wakati huu ambao kauli ya kiongozi mkuu ni sheria?
Labda enzi za Magufuli , lakini Samia hana shida na wawekezaji wakubwa, nitajie jambo moja tu Samia alilosema likawatisha wawekezaji? zama zimebadilika, Hata huko Ulaya makampuni yanafunga biashara kwa kupata hasara. hiyo ni kawaida kwenye biashara.
 
Business rationalization. So they are back to the kind of business, Citibank Tanzania is pursuing.

No individual account, unless linked with a Corporate account (consumer)

No SMEs, (business) and no High Networth (private).

And for corporates, a higher threshold definition. Normally, Corporate Banking targets Multinationals, first with British or European links etc, then Regional Corporates etc, for local, only the top tier. Bakhressa, etc.

Reason: Consumer and Private accounts: probably higher risks associated with high networth individuals whose wealth could present serious challenges to monitor but higher regulatory and reputation risks.

Local corporates and Businesses: difficulties to trace ownership and political influences.

Overall, probably, Stanchart have challenges from NMB, CRDB, DTB, and other Regional banks for competitiveness versus cost of doing business in those categories. So little growth (no appetite) since not much value can they add to what NMB etc are already offering.
 
Bila katiba Mpya wataondoka wengi. Maana hawa maRC wanaokwenda kuwakamua pesa kwa lazima kinyume na sheria lazima wakimbie tu
Kwani kina makonda bado wako kwenye system. Tuendelee kusherekea kifo cha mwendazake.
 
Wanakimbia kashfa ya kutumika kutakatisha pesa za mabilioni.. Sakata la IPTL nknk.. Ni taasisi ya fedha iliyochafuka machoni pa watanzania na haiaminiki tena
Waache kukimbia wakati ule wa dikteta wakimbie sasa hivi nchi mikononi mwa walewale waliopiga hizo pesa?
Hivi kama wangeondoka wakati wa JPM tungeambiwa hii sababu.
 
Labda enzi za Magufuli , lakini Samia hana shida na wawekezaji wakubwa, nitajie jambo moja tu Samia alilosema likawatisha wawekezaji? zama zimebadilika, Hata huko Ulaya makampuni yanafunga biashara kwa kupata hasara. hiyo ni kawaida kwenye biashara.
Hizi kauli tuliambiwa wakati wa JPM hatukuamini leo mnataka watanzania waamini kuwa kufungwa kwa biashara ni jambo la kawaida. Tusubirie muda utatuambia nani ni bora.
 
Waache kukimbia wakati ule wa dikteta wakimbie sasa hivi nchi mikononi mwa walewale waliopiga hizo pesa?
Hivi kama wangeondoka wakati wa JPM tungeambiwa hii sababu.
Shoka moja haliangushi mbuyu ..ila zikiwa nyingi lazima mbuyu uende chini...SC wamepoteza trust na wana chain ya kashfa na case za madai
 
Hizi kauli tuliambiwa wakati wa JPM hatukuamini leo mnataka watanzania waamini kuwa kufungwa kwa biashara ni jambo la kawaida. Tusubirie muda utatuambia nani ni bora.
Hukuamini nini sasa? enzi za Magufuli hakuna makampuni yaliyofungwa? Tumeshaona mwelekeo wa Samia ni mzuri kupita magufuli,. .. rais bora tayari tumeshamjua
 
Lazima waondoke kama riba za mikopo (interest rates ) za CRDB na NMB zitakuwa chini ya asilimia 10. Mabenki kama Standard chartered walizoea 23% na kuendelea. Sasa kipi bora kwa mwananchi riba ya mkopo ya asilimia 9 au 23 .
[emoji28][emoji28] hizo riba za chini ya 10% wewe raia wa kawaida kuipata ni kipengele. Kwanza zinaweza tolewa kwa wakopaji wakubwa, pia ni kwa baadhi ya products kama agriculture window tena kwa sababu hizo fedha wanazichukua BOT kwa masharti ya kukopesha chini ya 10%. Otherwise products nyingine bado zipo juu kama mabenki mengine tu
 
Kuna hii habari kwamba Standard Chartered Bank wanataka kufungasha vilago ikoje?

Kama ni kweli, Juzi kati tuliambiwa, mama kayafufua mabenki hili halijafufuka?.

NB; Standard Chartered Bank ni banker wangu
Haina Impact Bank zisizo na faida kwa Watanzania. Imekopesha Wajasiriamali Wangapi au Wakulima Wangapi? Hakuna Jibu zaidi ya kutegemea Hati Fungani tu
 
UBER WAMESEPA NA SASA STANDARD CHARTERED. USHUNGI ANAFUNGUA NCHI KWA KASI SANA
Uber ilikuwa inachangia kodi kiasi gani kwa. Nchi? Kama ni Application peke yake hata Watoto wa DIT wanaweza kuwa nayo
 
Labda enzi za Magufuli , lakini Samia hana shida na wawekezaji wakubwa, nitajie jambo moja tu Samia alilosema likawatisha wawekezaji? zama zimebadilika, Hata huko Ulaya makampuni yanafunga biashara kwa kupata hasara. hiyo ni kawaida kwenye biashara.
Hicho ndicho nilikuwa nakisema, wawekezaji wakubwa hawataki kutegemea hulka na tabia za mtu mmoja.
Samia akibadilika ama akiondoka akaja kama Magufuli?

Kama taifa hatutakiwi kuishi kama waishio kwa kutegemea ramli!

Tunahitaji mwongozo mpya kupitia katiba mpya.
 
Ukifuatilia wachangiaji wengi, Kuna tatizo mahala nchi hii.

Ifikie hatua Watanzania tujue nini tunataka kwa wakati gani, aliyofanya Nyerere kwa wakati wake yalikua sahihi kwa wakati huo, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Maguful pia.

Tunatakiwa kujua tunataka nini kwa sisi kujikwamua lakini kutwa nzima watu wanalinganisha serikali zilizopita, unafikiri Kuna Rais atakaa Ikulu na kutulia? Atakua anafanya kama anashindana na mtangulizi wake ilihali alitakiwa kupeleka Tanzania mbele bila kujali nani alifanya nini.

Matokeo yake tunadumaa na kuamini maendeleo ni kumzidi mtangulizi wako.

Tuanze kuilinganisha Tanzania na nchi zilizoendelea, tuangalie mataifa ya ulaya, China na Marekani yako wapi, wanapiga hatua gani za kimaendeleo.

Haya Magenge yetu ni hovyo na yanakua kama laana kizazi hadi kizazi.

Kweli mtu anakaa na kusema fulani kaleta maendeleo sio kama fulani, Tanzania ina maendeleo? Shuwain.
Nami Jambo hili linanikera kuwa bize kulinganisha flani dhidi ya flani. Ila nadhani viongozi wenyewe ndiyo wanaowaongoza wananchi kwenye tabia hii,kiongozi wa awamu moja anamzodoa kiongozi wa awamu nyingine,basi wananchi nao wanaichukua unakuwa wimbo wao
 
Back
Top Bottom