Standard FM ya Singida kuibomoa wasafi Media

Huko maswenkeni, nani ataishi?
 
aisee madelu naona anafanya mambo yake fastafasta kabla hajatua mikoba ya vijisenti
 
Duuuu ima piga mawimbi pande zipii ??
haiko standard sana kivile, mawimbi yake kwa sasa yanafika baadhi ya maeneo ya mikoa ya tabora, simiyu, shinyanga na manyara. Bado iko chini sana kupasua anga kama redio one, rfa, east africa na clouds
 
Hii redio kama ni kweli itahusishwa na Mwigulu.
Watanzania akili zao utadhani singida nzima kuna Mwigulu Nchemba tu.
 
Kina diva wakienda standard fm watakutana na azaria aliyekuwa rfa. Naona delu anataka kufanya usajili wa nguvu kwenye hiyo redio
 
Ndo ile ile standard fm au kuna nyingine nisoijua....
Amna watu pale, sema n ww umeikubali kivyako tu.
 
Redio za mikoani hazina vibe kubwa kama redio za dar. Moshi kuna moshi fm, kili fm, sauti ya injili zina vibe kubwa sana mjini moshi na viunga vya mkoa wa kilimanjaro. Pia kuna Kicheko fm inapasua anga mpaka miji ya kanda ya kati. Ingependeza sana TCRA kutoa masafa ya redio iruke hewani nchi nzima wananchi wajichagulie redio za kusikiliza. Bado kuna miji na vijiji redio hazisikiki watu wanaishi bila kupata habari na taarifa, hata hiyo TBC usikikaji wake ni hafifu, hivi vi local redio vipewe leseni ya kwenda hewani umbali mrefu kuwafikia wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ