Star Link yaanza kupigwa vita na makampuni ya simu isije Tanzania

Hili mimi nililitarajia mapema sanaa, kama ambavyo kuna hujuma kwenye kusambaza vituo vya magari ya kutumia gesi ili kundi fulani la waagiza mafuta liendelee kutunyonya na bei kubwa za mafuta ya magari. Ushauri wangu ni kwamba TTCL watafute namna ya kuingia ubia na huyu Elon Musk kwenye hii kitu, hapo watawaweza hao wahuni wa makampuni ya simu kwa sababu TTCL ni serikali.
 
Kwa mfumo wa mambo hapa bongo jamaa watapata shida sana, kama dstv alivyoshikilia soko la ukanda huu, anacheza na wakubwa, starlink nayo itakuja kuwa kama visimbusi vya canal, unanunua huduma toka kenya au nchi jirani walizoruhusu ndo unakuja kutumia huku.

Hapo labda na wao wakubali kula na wakubwa na wakishakubali tu lazima gharama ziwe kubwa yanakua yaleyale
Gharama zikiwa kubwa si unaenda kwenye makampuni ya simu? Acheni kushabikia monopoly.
 
Hili mimi nililitarajia mapema sanaa, kama ambavyo kuna hujuma kwenye kusambaza vituo vya magari ya kutumia gesi ili kundi fulani la waagiza mafuta liendelee kutunyonya na bei kubwa za mafuta ya magari. Ushauri wangu ni kwamba TTCL watafute namna ya kuingia ubia na huyu Elon Musk kwenye hii kitu, hapo watawaweza hao wahuni wa makampuni ya simu kwa sababu TTCL ni serikali.
Katika kampuni ambayo imejichokea ni TTCL hadi huruma
Nina miezi 6 sasa, nahangaikia laini zao. Hazipo, nilifika hadi Arusha napo hakuna
 
Wakumbuke kipindi wanaiba kura walifunga mitandao, lkn watu walipata alternative kirahisi tu.
Acha wakomae na hizo analogia zao si muda mrefu tutapata ma bando free of charges.
Chezea teknolojia....
 
Makampuni mawili ya simu sitaki kuyataja wameanza mkakati wa kuhakikisha Star link haiji Tanzania kwa kuhofia ushindani.

Kibaya zaidi wanagawa rushwa na hata juzi walikua na kikao kizito kizito na baadhi ya watu wasio waaminifu kutoka Tcra na maafisa kadhaa wa serikali.

Hebu imagine hawa watu wanakosa tija kiasi cha kuanza mkakati wa kuhakikisha Star Link hawaruhusiwi kuja Tanzania.

Naiomba serikali hili jambo wasilipuuze hata kidogo, tutapoteza mapato tukiacha uwekezaji wenye manufaa kama huo wa Star Link.

Wanafahamu fika kuwa wamezoea kuwaibia watanzania kwa vifurushi vyao uchwara na MB za mchongo lakini wanafahamu fika kuwa Star link wakija litakua ndio kimbilio la watu wengi kwa sababu ya kasi yao ya intaneti na mabando mazuri yanayoeleweka.

Mimi najiuliza tu jamani hamridhiki?Nyie nyie mmeweka mtu wenu kule ttcl analihujumu lile shirika na sasa linaenda kufa rasmi sasa mnakaa vikao vya kuihujumu Starlink isije Tz hii nchi ina baadhi ya watu walafi sana wenye uchu na wasioridhika

Inasikitisha sana kibaya zaidi wapo maafisa wa serikali watu na heshima zao kwasababu wanapewa pesa mamilioni na makampuni ili wazuie starlink isije tz
Mzee fanya kama mwakyembe taja hao watu hukificha wanajua hawajafahamika.
 
Pole Mwamba najua umeumia Ila huo ni Mpango wa CIA Kwenye program Yao kupambana na Beijing katika Technology hivyo hapo wanahonga kupitia kampuni za simu zilizopo Tz kuitisha vikao vya Siri na Wafanyakazi wa Umma watumie NGUVU kubwa kuikataa hiyo kampuni Maana ikiingia Share holder wa kampuni hizo wenye interest na USA watafilisika maana kampuni hiyo Ikipenya itaua Technology ya USA na Mfumo wa Upelelezi wao.
Si Unajua HUAWEI imepigwa ban USA.
 
Yaani mimi ningepata nafasi ya kuwa raisi wa hili taifa. Magufuri ni cha mtoto aiseee. Ama nitawanyoosha kwanza nikigundua kwa namna yoyote ile aidha mtumishi wa serikalini ama taasisi binafsi anacheza na mifumo kwa masilahi yake binafsi au kikundi na kuhujumu uchumi wa inchi. Ataozea jela na hukumu ni kifo.

Na sitajali takataka yoyote atakae mtetea nitadeal nae personally atuambie ana masilahi gabi na wizi wa ndugu yake. PUMBAVU SANA.

Taifa linachelewa maendeleo sababu ya machoko wachache sana hili.
Mtu anatiwa ndani na nahakikisha hatoboi. 🤣 Atapigwa Pollonium tu akiwa jela. Akitoka nje miezi 6 mingi lazma alambe futi 6! Hivyo ndo namna ya ku deal na wasaliti.
 
Wote waliotajwa wamevimbirwa tuu.

Nasi tunapenda mavitu makubwa tu wakati matumizi yake yanaweza kuwa ya kihasara hasara...Sidhani kama tunatumia teknolojia iliyopo at full capacity pompous!
What is the full capacity mzae? Kila mtu anatumia internet kwa kiwango chake. Huwezi mpangia mtu atumieje data.
 
😅😂What is the full capacity mzae? Kila mtu anatumia internet kwa kiwango chake. Huwezi mpangia mtu atumieje data.
Bill Gates kupitia computer 4 Africa alimwaga kila aina ya kompyuta Barani Afrika na kama sikosei hata hapa kwetu Tanzania tulifaidika na aina fulani ya misaada hiyo, iwe ni zile Desktops au laptops n.k . Nafikiri tunaweza kubaliana kuwa matamanio ya wote,yaani Bill na Serikali yetu ni kuona Wananchi/Wanafunzi au wale waliokuwa mbali na miji wanapata Taarifa kupitia hii Internet pamoja na faida zake zingine zinazokuja na teknolojia hiyo. Kwa kifupi, mathalani Katiba yetu ingekuwa ipo Digital au ipo digital hivi unataka kuniambia unahitaji miaka mitatu kuisoma na kuilewa? pointi ni uwepo wa hii teknolojia halafu ndio unakuta haijatumiwa at Full capacity, sawa na teknolojia nyingine kama kulima kwa pembejeo za kuswagwa na Ng'ombe na bado tukashindwa kufikia capacity ile ambayo wenzetu walitumia kufika walikofika katika ukulima hadi uzalishaji wa ghafi zake. Sasa leo hii unataka Starlink? Na sisemi hakuna uhitaji, nasema, Je, tumetumia hata hizo fiber or what have you za kurusha na kupokea mawasiliano ya Internet to a capacity tukasema , 'we have made strides' tunataka hiyo starlink kwa nini? Kuleta ushindani? Kupunguza bando tu?

Sasa tukirudi kwenye huo utumiaji wa Data, akija starlink atabadilisha nini? Serikali inatumia haya mabando kuhakikisha ina control Information-naweza kusema ni strategy mpya na effective kuliko ile ya kuzima internet kabisa-unasoma bandiko lako moja JF kwishney!😅😅
 
Makampuni mawili ya simu sitaki kuyataja wameanza mkakati wa kuhakikisha Star link haiji Tanzania kwa kuhofia ushindani.

Kibaya zaidi wanagawa rushwa na hata juzi walikua na kikao kizito kizito na baadhi ya watu wasio waaminifu kutoka Tcra na maafisa kadhaa wa serikali.

Hebu imagine hawa watu wanakosa tija kiasi cha kuanza mkakati wa kuhakikisha Star Link hawaruhusiwi kuja Tanzania.

Naiomba serikali hili jambo wasilipuuze hata kidogo, tutapoteza mapato tukiacha uwekezaji wenye manufaa kama huo wa Star Link.

Wanafahamu fika kuwa wamezoea kuwaibia watanzania kwa vifurushi vyao uchwara na MB za mchongo lakini wanafahamu fika kuwa Star link wakija litakua ndio kimbilio la watu wengi kwa sababu ya kasi yao ya intaneti na mabando mazuri yanayoeleweka.

Mimi najiuliza tu jamani hamridhiki?Nyie nyie mmeweka mtu wenu kule ttcl analihujumu lile shirika na sasa linaenda kufa rasmi sasa mnakaa vikao vya kuihujumu Starlink isije Tz hii nchi ina baadhi ya watu walafi sana wenye uchu na wasioridhika

Inasikitisha sana kibaya zaidi wapo maafisa wa serikali watu na heshima zao kwasababu wanapewa pesa mamilioni na makampuni ili wazuie starlink isije tz
tulishaambiwa 2025 tuchague viongozi vizuri, tuchague wale watakaotusaidia, hawa wasiotusaidie tangu tumeanza kulia suala la bando, tuwaweke pembeni.
 
Back
Top Bottom