Star TV wameonesha udhaifu mkubwa sana
Hapa ndipo power ya njia mbadala za mawasiliano inaingia. Waache traditional media zimekufa, zote zinaogopa kuliko maelezo. Lazima wapinzani waangalie namna mbadala ya kufikia wananchi, wasidharau mitandao ya kijamii.Huyo kijana alionekana kama anawavuruga watu, wakati tayari watu wameshavikwa ujinga wa kumkubali Magufuli na ccm. Wakati huo wanaambiwa cdm imekufa. Unategemea akianza kuongea si lazima iwe balaa. Nilitabiri kuelekea uchaguzi mkuu, wapinzani hasa cdm watanyimwa airtime, na wapinzani watafanyiwa unyama na ukatili wa wazi, huku vyombo vya habari vikizuiwa kutangazwa unyama huo.
Wakati hayo yakiendelea ccm, itapewa airtime kubwa, na kutapigwa propaganda kubwa kuwa wapinzani wameishiwa nguvu kutokana na utendaji wa Magufuli. Lile kundi la watu wasiojulikana ndio litafanya kazi kubwa ya kunyamazisha watu, kwa kuwateka, kuwaachia vilema na hata vifo. Muda utatoa majibu ya haya.
Inaumiza saana mijadala huru inazimwa na CCM na watu wa idara ya usalama wa taifa anyway na mijadala yenu itazimwa miaka mitano ijayo .
Bora umeliona hilo na kulisema, nilihisi tu nilipomuona huyo mwenyekiti wa bavicha lazima ccm wataleta shida. Hata asubuhi hali ilikaribia kuwa hiyo hiyo, na nilikuwa namuona kabisa mtangazaji akipata wakati mgumu kila michango ya mwenyekiti wa cdm kanda ya ziwa akichangia. Hapo ndio tulipofikia, kinachotakiwa ni kumsifia rais na ccm, kinyume na hapo lazima mjadala uzimwe!
jamaa alikuwa anatoa madini yenye kuwa na mashiko