Star tv mmezimwa na CCM au wapambe wa CCM?

Star tv mmezimwa na CCM au wapambe wa CCM?

Bora umeliona hilo na kulisema, nilihisi tu nilipomuona huyo mwenyekiti wa bavicha lazima ccm wataleta shida. Hata asubuhi hali ilikaribia kuwa hiyo hiyo, na nilikuwa namuona kabisa mtangazaji akipata wakati mgumu kila michango ya mwenyekiti wa cdm kanda ya ziwa akichangia. Hapo ndio tulipofikia, kinachotakiwa ni kumsifia rais na ccm, kinyume na hapo lazima mjadala uzimwe!
Hata ukipigiwa mkeo utasema ccm
 
Inaumiza saana mijadala huru inazimwa na CCM na watu wa idara ya usalama wa taifa anyway na mijadala yenu itazimwa miaka mitano ijayo .
Hata ukipigiwa mkeo utasema usalama wa taifa
 
Ccm walitegemea walivyoviziba vyama vingine midomo kwa hii miaka yote ya utawala wa Meko mambo yatakuwa marahisi, matokeo yake dakika za mwisho wanashtuka kuona upinzani upo so hot kama vile hakuna kilichotokea.
 
Startv siku zote naamini ni feki, na wote wanaopata nafasi ya kuzungumza hapo lazima wawe wanafiki ili wakubaliwe.

Mpinzani wa kweli hawezi akapewa nafasi kwenye tv Station ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa; never, watapewa wanafiki wachache tu wanaojidai neutral.
 
Huyo kijana alionekana kama anawavuruga watu, wakati tayari watu wameshavikwa ujinga wa kumkubali Magufuli na ccm. Wakati huo wanaambiwa cdm imekufa. Unategemea akianza kuongea si lazima iwe balaa. Nilitabiri kuelekea uchaguzi mkuu, wapinzani hasa cdm watanyimwa airtime, na wapinzani watafanyiwa unyama na ukatili wa wazi, huku vyombo vya habari vikizuiwa kutangazwa unyama huo.

Wakati hayo yakiendelea ccm, itapewa airtime kubwa, na kutapigwa propaganda kubwa kuwa wapinzani wameishiwa nguvu kutokana na utendaji wa Magufuli. Lile kundi la watu wasiojulikana ndio litafanya kazi kubwa ya kunyamazisha watu, kwa kuwateka, kuwaachia vilema na hata vifo. Muda utatoa majibu ya haya.
Tunaaminishwa kuwa CCM inaongozwa na kiongozi wa Malaika ambaye sasa amebatizwa na kuitwa Yesu.Hii ni kufuru na chukizo mbele ya Mungu.
Najiuliza,hivi Sisi ni binadamu wa kawaida kweli?
 
Back
Top Bottom