Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona

Its true maswali hayajajibiwa, muda ni mdogo ila nimeya forward yote.
Kwa vile Dr. Faustine Ndugulile ni member humu, amekubali akipata muda, atatimba jf na kujibu maswali yenu.
P
 
Biashara muhimi tu pekee kama maduka ya madawa na vyakula ndio yanapaswa kubaki wazi. Kuanzia makanisa, misikiti, maduka ya nguo, baa, na mikusanyiko mingine yote isiyo ya lazima ipigwe marufuku.
Hayo maduka ya chakula unakusudia nini hasa?
 
Hongera Dr.Abas kwa kusema ukweli #kifo Corona TBC, corona ipo si kwa wale tu hata sisi wabongo wa kawaida Mungu baba atunusuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
Corona ipo ila tusisahau na maradhi mengine yanayotusumbu kila siku katika jamii zetu na kusababisha vifo bado maradhi hayo yapo kama kawaida,corona haijaja kusimamisha maradhi mengine maana tunaambiwa marehemu pia alikuwa na maradhi mengine.
 
Iundwe forum maalum ya kuzungumzia hili gonjwa la corona(tuliambiwa ugonjwa ni 'covid-19') ili kupunguza hofu tuliyonayo. Mara ya kwanza tuliambia maambukizi ni kwa njia ya majimaji yanayotoka puani na mdomoni mwa mwenye corona baada ya kupiga chafya,kukohoa au kutema mate. Ila sasa tumeambiwa kuwa pumzi/hewa inayotoka kwa mwenye corona ina hao virusi,na wanaweza kukaa/kuishi kwenye hewa kwa masaa kadhaa(?8hrs). Ukivuta hiyo hewa,unaupata ugonjwa, hizo barakoa vipi sasa. Jana tumemwona balozi wa china akiongea na PM wetu,ametinga barakoa. Kwenye mkutano wa Mh Ummy na viongozi wa dini,niliwaona baadhi yao wamevaa barakoa visivyo,wamefunika midomo tu,pua zikiwa wazi.
 
Watu lockdown cjui wanafikilia ni nin yaan 😁
Wanadhani ni "Total Lockdown" yaani kila kitu kinasimama. Kumbe hata hapa kwetu tayari tuna "lock down" ila watu wanataka iongezwe makali kidogo, Unamtoa mtoto shule kwa hoja ya CORONA lakini Unamwachia aende Kanisani kwenye mlundikano wa watu kuliko kwenye shule aliyotoka.Inashangaza kidogo.
 

Hiyo ni "school closure" siyo "lockdown".
 
Nyumba za ibada ,sehem za sterehe zingekula suspension kwanza watu wasali nyumbani ,walevi walewe nyumbani tukifel kwenye partial lockdown uko mbeleni hata total lockdown itakua ni mtihan mkubwa sana
 
Siyo kila closure ni lockdown. Nchi zinazotajwa hazikufanya lockdown, zilifunga mashule. Pana mtu JF aliandika uzi mzuri sana unaoelezea saikolojia ya wanaolilia lockdown.
Ili kuwe na "Lock down" ni lazima kuwa na "Closure" kwa kuwa huwezi kuwaambia watu wabaki nyumbani wakati kazi zao bado ziko wazi. Hoja hapa mashule hayakufungwa kwa kuwa muda wa kufungwa ulifika bali kwa kuwa serikali iliyafunga (Lock down) kwa hoja ya ugonjwa wa CORONA.

Ndiyo maana nataka kujua inawezekanaje kufanya "Lock Down" bila ya kuwepo kwa "Closure" kwenye shughuli mbali mbali? Yaani inaitwa "Lockdown" kwa kuwa inaamuliwa nje ya matakwa ya mfungaji lakini bado tendo ni ufungaji ama uzuiaji wa shughuli husika.

Hakuna mtu anayelilia "total Lock down", kwani unadhani kuna mtu atafaidika na kufungwa kwa shughuli mbali mbali zinazoendesha maisha ya watanzania?

Halafu tendo la ufungaji shule linakanganya sana. Shule zimefungwa lakini bado hao waliotoka shuleni wamerudi nyumbani na wanaendelea kuchanganyana kwenye makundi makubwa ya watu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…