Ili kuwe na "Lock down" ni lazima kuwa na "Closure" kwa kuwa huwezi kuwaambia watu wabaki nyumbani wakati kazi zao bado ziko wazi. Hoja hapa mashule hayakufungwa kwa kuwa muda wa kufungwa ulifika bali kwa kuwa serikali iliyafunga (Lock down) kwa hoja ya ugonjwa wa CORONA.
Ndiyo maana nataka kujua inawezekanaje kufanya "Lock Down" bila ya kuwepo kwa "Closure" kwenye shughuli mbali mbali? Yaani inaitwa "Lockdown" kwa kuwa inaamuliwa nje ya matakwa ya mfungaji lakini bado tendo ni ufungaji ama uzuiaji wa shughuli husika.
Hakuna mtu anayelilia "total Lock down", kwani unadhani kuna mtu atafaidika na kufungwa kwa shughuli mbali mbali zinazoendesha maisha ya watanzania?
Halafu tendo la ufungaji shule linakanganya sana. Shule zimefungwa lakini bado hao waliotoka shule wamerudi nyumbani na wanaendelea kuchanganyana kwenye makundi makubwa ya watu!