Vincenzo Jr
Platinum Member
- Sep 23, 2020
- 24,262
- 58,728
Speed zao hazifiki mbps 200 mkuu hata kikiwa cha package ya bei hiyo yakifurushiMbona hata hapa unapata kit laki 3 unlimited mpaka laki kwenye hii mitandao yetu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Speed zao hazifiki mbps 200 mkuu hata kikiwa cha package ya bei hiyo yakifurushiMbona hata hapa unapata kit laki 3 unlimited mpaka laki kwenye hii mitandao yetu.
Ajulie wapi yule boyaHivi alikuwa anajua hata kirefu cha SEACOM kweli 🤣🤣🤣🤣
Kwa hiyo 1 umeisoma wapi? Hakuna mahali wameandika 99%Sijaelewa hapo kampuni ya Starlink Satellite Tanzania ina hisa 1%, who owns the rest?
Awali ya yote bwana Musk alitakiwa awe na kampuni ambayo Ina public shares Yani kampuni yake iwe listed Dse,Alafu awe na physical address ili utatuzi wa changamoto za mitambo yao ipatiwe ufumbuzi mapema pindi zinapotokea,na pia atoe ajira kwa asilimia kadhaa Kwa watanzania.(Wasiwe ni wazungu tu).Nadhani kazi Yao bado ni ndefu ukiachilia mbali pia Kuna kampuni yenye jina mfanano na lao wanaitwa Starlink Tanzania Ltd.Hao jamaa watawapinga sana maana brand Yao ni kubwa Tanzania.Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo?
Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga,
View attachment 3152628
Meanwhile hivi ndivyo voda na wenzake walivyo sasa hivi
=====
Baada ya muda mrefu wa Watanzania kuhoji kwanini Tanzania hatujaruhusu uwepo wa Internet ya Starlink kutoka kwa tajiri Elon Musk, hatimaye leo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo kuonesha Kampuni hiyo imeomba kupatiwa leseni ya Kitaifa ya Miundombinu na Leseni ya Kitaifa ya Huduma ya Mifumo Tumizi.
Kwa muda mrefu Wananchi wamekuwa wakihoji kwanini Tanzania hatuna huduma hii na hasa ukizingatia kwa wenzetu majirani wanayo; Je, kwanini Tanzania hatupati huduma ya starlink nini shida?
Wakati hapa kwetu kumekuwa na kususua kupokea huduma hii wananchi wakihoji kwanini: Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?
Katika moja ya fafanuzi zake, aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti, hivyo ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.
Na haya yalikuwa majibu ya Nape, kuwa serikali haikuwa imeweka vikwazo vyovyote ila bwana Elon hakuwa na mpango wa kuanzicha huduma hiyo nchini: Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania
Hata hivyo, Februari mwaka huu, akiwa bado Waziri, Nape Nnauye alisema Kampuni hiyo inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa huduma nchini. Aliongeza kuwa ikishatimiza taratibu zote itaanza kutoa huduma na kwamba Serikali inasubiri wakamilishe tu taratibu hizo.
Sasa hivi Kampuni hiyo imeomba leseni tena na TCRA kwa sasa imeweka wazi kabisa uombaji huo tofauti na awali ambapo haikuwa wazi. Sasa maswali ya kujiuliza ni
- Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo? Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga
- Je, sasa hivi amekubali kujenga ofisi au ile ilikuwa janja janja ya kipindi kile?
Awali ya yote bwana Musk alitakiwa awe na kampuni ambayo Ina public shares Yani kampuni yake iwe listed Dse,Alafu awe na physical address ili utatuzi wa changamoto za mitambo yao ipatiwe ufumbuzi mapema pindi zinapotokea,na pia atoe ajira kwa asilimia kadhaa Kwa watanzania.(Wasiwe ni wazungu tu).Nadhani kazi Yao bado ni ndefu ukiachilia mbali pia Kuna kampuni yenye jina mfanano na lao wanaitwa Starlink Tanzania Ltd.Hao jamaa watawapinga sana maana brand Yao ni kubwa Tanzania.
Kasome Companies Act, 2002 (Cap. 212) of Tanzania,Section 30(1).Alafu niambie kama unaweza kusajili kampuni inayofanana jina na Azam uiite Azam mboga kama itakubaliwa.Hizi drama zenu ndio maana wao wamejisajili kama Starlink Satellite Tanzania Ltd.
Mkuu unakuwa mbishi wakati waomba leseni wametumia jina hilo na TCRA wameonesha kukubaliana nalo. Kama ni kulikataa ilitakiwa ianzie brela kabla ya kwenda TCRA. Ili kulinda jina lenu mmeshawahi kufikiria kulisajili under trademark?Kasome Companies Act, 2002 (Cap. 212) of Tanzania,Section 30(1).Alafu niambie kama unaweza kusajili kampuni inayofanana jina na Azam uiite Azam mboga kama itakubaliwa.