Starlink yawasilisha maombi ya leseni kwa TCRA. Je, safari hii watatoboa? Ushindani wa gharama na ubora wa internet utakuwaje?

Starlink yawasilisha maombi ya leseni kwa TCRA. Je, safari hii watatoboa? Ushindani wa gharama na ubora wa internet utakuwaje?

kununua vifaa ni KSH 88K = 1.7M

hiyo 130k ni basic plan😂

kuna mkenya nilimsikia anasema bora zuku tu
Kuna options nyingi unaweza chagua kutokana na mfuko wako
Screenshot 2024-11-15 153002.png
Screenshot 2024-11-15 153124.png
Screenshot 2024-11-15 153148.png
Screenshot 2024-11-15 153236.png
Screenshot 2024-11-15 153311.png
 
Bei hazitofautiana sana, In economics there is something called oligopoly market structure na hizo internet service providers ziko katika soko la namna hiyo. Ingekua monopoly wangeweza kuweka bei wanazozitaka, kwa Kasi ndo Kuna ushindani Zaid na area of coverage
#No malice to anybody
 
Bei hazitofautiana sana, In economics there is something called oligopoly market structure na hizo internet service providers ziko katika soko la namna hiyo. Ingekua monopoly wangeweza kuweka bei wanazozitaka, kwa Kasi ndo Kuna ushindani Zaid na area of coverage
#No malice to anybody
Kwani serikali inashindwa nini kuwaacha ISP wote watoe huduma ya vifurushi wanavyoona wao inafaa, maana kila kitu ni ushindani, wao TCRA waangalie wasivunje sheria tu...hata ISP atoe 3 kwa 500 tatizo linakuwa wapi?
Kufanana kwa vifurushi inakuwa na maana gani kuwepo kwa mitandao yote, mimi naona kwenye vifurushi TCRA wawaache ISP's wafanye kipi kinafaa kwa wateja wao. Monopolization ndo best deals kwa sasa hicho wanachofanya ni sawa na kuwaumiza wananchi tu kufanya huduma iwe ghali pasipo saba u za msingi.

Ila kama TCRA kweli walitoa tangazo kuhusu ushirikishwaji wa wananchi juu ya StarLink, wao mbona wakati waliweka same packages ya vifurushi ISP hawajatushirikisha?

Wawache Starlink ili TTCL aamke maana ndio mama wa mkongo wa Taifa but bado kalala usingizi wa pono 😂
 
Ngoja tuone,kwasasa Nape hayupo na kipara labda tutatoboa!!

Ndio maana jk hana furaha coz democratic wameshindwa na wao ndio wanapenda vita vita ,sio trump ambaye hatoingilia mambo yetu na mama atapeta tuuuuuuu!!!
 
Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo?

Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga,

View attachment 3152628
Meanwhile hivi ndivyo voda na wenzake walivyo sasa hivi​


=====

Baada ya muda mrefu wa Watanzania kuhoji kwanini Tanzania hatujaruhusu uwepo wa Internet ya Starlink kutoka kwa tajiri Elon Musk, hatimaye leo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo kuonesha Kampuni hiyo imeomba kupatiwa leseni ya Kitaifa ya Miundombinu na Leseni ya Kitaifa ya Huduma ya Mifumo Tumizi.


Kwa muda mrefu Wananchi wamekuwa wakihoji kwanini Tanzania hatuna huduma hii na hasa ukizingatia kwa wenzetu majirani wanayo; Je, kwanini Tanzania hatupati huduma ya starlink nini shida?

Wakati hapa kwetu kumekuwa na kususua kupokea huduma hii wananchi wakihoji kwanini: Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?

Katika moja ya fafanuzi zake, aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti, hivyo ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.

Na haya yalikuwa majibu ya Nape, kuwa serikali haikuwa imeweka vikwazo vyovyote ila bwana Elon hakuwa na mpango wa kuanzicha huduma hiyo nchini: Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania

Hata hivyo, Februari mwaka huu, akiwa bado Waziri, Nape Nnauye alisema Kampuni hiyo inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa huduma nchini. Aliongeza kuwa ikishatimiza taratibu zote itaanza kutoa huduma na kwamba Serikali inasubiri wakamilishe tu taratibu hizo.

Sasa hivi Kampuni hiyo imeomba leseni tena na TCRA kwa sasa imeweka wazi kabisa uombaji huo tofauti na awali ambapo haikuwa wazi. Sasa maswali ya kujiuliza ni

  1. Bei zitapungua? Au wataambiwa waendane na bei za washindani zilizopo? Najua kwenye ubora jamaa atawapiga chenga
  2. Je, sasa hivi amekubali kujenga ofisi au ile ilikuwa janja janja ya kipindi kile?
kampuni bila hata mtanzania kushika hisa what a https://jamii.app/JFUserGuide
 
Lazima watapelekwa kwenye rates zetu. Kuna taasisi moja iliundwa kwa ushirika na nchi za Ulaya, walikuwa na mpango wa kulipa mishahara minono kama ya Ulaya. Wizara ya fedha ikakataa, ikataka walipwe kwa ngazi za Tanzania. The same happened kwa TBL wakati inabinafsishwa kwa ubia.

Last time walipewa sharti wawe na ofisi Tanzania, may be mambo ya kodi, na kufanikisha udukuzi
Huyo msenge alioleta upumbavu huo ningemtukana straight away. Yani mtu anataka kulipa kwa rates za ulaya wewe unaleta ushenzi wa TGS D.
 
Naona raia wengine wa nairobi wanasema ndani ya jiji la nairobi speed si kubwa kwa sababu ya majengo kukaribiana na signal boosters za wanaotumia safaricom hivyo zinaingiliana na mawimbi ya starlink. Pia starlink wenyewe wamesitisha kuuza vifaa vyao wakisema watumiaji wamekuwa wengi kuliko bandwidth ya hapo.
Ila nje ya nairobi watu wanakula speed za kutosha mpaka mb 200 download speed.
Wajiandae na mafuriko hapa Tanzania. Kumiliki starlink itakuwa sawa na kujenga kwako kuepuka kero za mwenye nyumba
 
Back
Top Bottom