Stars ilivunjika baada ya Mohamed Hussein, Mzamiru Yassin na Himid Mao kutoka

Hapo kwa Mohammed Hussein hamna kitu, alistahili kutoka kabisa. Mchezaji amepoteza mipira zaidi ya Mara tano kipindi cha kwanza unategemea kweli amuache. Timu inaacha wachezaji walio kwenye kiwango kizuri kwenye timu zao unaleta Ugali na Sukari. Kocha abebe lawama zote.
 
mohamed hussein na himid mao wote waliomba kutoka,tusilaumu kocha
 
Bila kuwa na Academy hakuna kinacho wezekana
Kwa Sasa academy haziwezekani tena watoto wanaingia shule kuanzia jumatatu hadi jumamosi na ni saa 12:30 asbh hadi 12:00 jioni huo mda wa kuandaa academy utapatikana wapi!?
Mi nadhani tuboreshe ligi usajili wa wageni uongezwe masharti ya Kodi yarekebishwe tuweke mishahara mizuri tupate Forward kama Shalulile na Percy Tau
 
Mohamed Husseni aliumia. Wewe ni Yanga tatizo linaanzia hapo
 
Na pia baada ya Mohamed Hussein kuumia nadhani angemrudisha Nova beki 3 then Kati angerudi Mwamnyeto
 
Uzuri Bongo kila mtu kocha,sijui mchambuzi na makorokocho kama hayo.

Mpira mchezo wa wazi .
 
Fei atafute timu mapema atapotea sio muda. Arudi huko Utopolo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…