Stars isipojifunza kwa Angola na Guinea tutapigwa hadi tuchakae

Mr Alpha

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
273
Reaction score
765
Kucheza na timu zenye uwezo mkubwa na wachezaji mahiri wanaocheza Ulaya timu zenye uzoefu mkubwa na heshima kubwa kisoka Afrika na duniani inabidi uingie uwanjani kupigana jihadi kwa jasho na damu ili kupata matokeo, tumeona namna ndugu zetu Msumbiji na Angola walivyong'ang'ania vigogo tishio kabisa Misri na Algeria na kupata alama.

Vivyo hivyo Guinea haikupewa nafasi kabisa dhidi ya wababe wa kihistoria Cameroon ila jamaa wamepambana mpaka kimeeleweka. Vipi Cape Verde kuwapiga Ghana hatujapata cha kujifunza? Nadhani kama nchi tumeenda AFCON tujue tumeingia kwenye mapambano hakuna kupigwa kinyonge lazima tuingie na mikakati yetu ya iwe mvua iwe jua lazima Morocco aachie point.

Wachezaji lazima wahusiwe mchezo dhidi ya morocco sio mechi NI VITA.

Ukiingia kwenye vita kuna chaguo moja kuua au kuuawa, Morocco hawaez kukubali matokeo ya sare au kushindwa na kibonde kutoka Afrika Mashariki watatumia kila mbinu kutuadhibu hivyo lazima tuingie na mpango wa kuishangaza dunia. Tumeamua kujitoa kwenye kundi la vibonde au kichwa cha mwendawazimu tuna deni la kuithibitishia dunia kwamba kweli tumetoka huko

Kazi kwenu timu ya hamasa na benchi la ufundi taifa stars wafikishieni ujumbe huu vijana wetu, heshima ya nchi ipo mikononi mwao

Wapambane kama hawatakuja kupambana tena hakika juhudi zao zitaandikwa kwa wino wa dhahabu na kuenziwa milele katika taifa la Tanzania

Mungu ibariki Tanzania [emoji120]
 
"Ukiingia kwenye vita kuna chaguo moja kuua au kuuawa".
Kufa au Kupona,
Do or Die
War in Abdijan
 
Guinea wote wanacheza ligi za ulaya .
Kuna mchezaji anachezea bundesliga aliwekwa benchi Jana.
 
Unyonge uwa unatugharimu sana kuna mechi taifa stars tulikuwa tuna uwezo kabisa wa kushinda ila unyonge ndio uliotugharimu tukafungwa
Kwenye jezi ingebidi iwepo Nembo ya Chui Tembo ama Simba.Sasa sisi Nembo yetu Huwa ni Twiga Kwa Kila jambo Twiga ana reflect kitu gani??
 
Kwenye jezi ingebidi iwepo Nembo ya Chui Tembo ama Simba.Sasa sisi Nembo yetu Huwa ni Twiga Kwa Kila jambo Twiga ana reflect kitu gani??
wanaamini twiga ni mnyama mrefu kwa viumbe wa sasa hivi na urefu wake unamfanya kuangaza mbali-
 
tz hatuwezi chochote.mondi anajitahidi kutuwakilisha lakini bado anapigwa majungu.
Aache kuimba nyimbo za 'masuala ya chumbani' tu atunge na za kuwahimiza vijana kufanya kazi zenye maslahi kwao na Taifa.
 
Fact ni kwamba hatutoboi mbele ya Morocco. Tutapokea kichapo mpaka tutapoteana uwanjani.

ANGALIZO: Kama una presha na sukari usiangalie huo mpira kwa siku hiyo.
 
Yaani Chelsea hii inayopumulia mashine huko EPL ndio mchezaji wake atufanye wanyonge?

Hapana labda useme sababu nyinginezo
Kwa sababu ya majina ya timu pinzani tukiskia hakim ziyech anachezea chelsea tunaingiwa ubaridi automatically
 
natumaini kwenye msafara tuna wana saikilojia, hii timu inahitaj wale ma motivationa speakers ili ikajilipue kupambana na hawa GIANTS, tukienda kinyoronyoro na kuwategea lina kibu, novatus na baka tutakula nyingi, wachezaji waweke ubishoo pembeni, haya ndo mashindano makubwa zaidi tunayoweza kushiriki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…