Startimes kuja na huduma za DTH

Startimes kuja na huduma za DTH

Startimes,sisi wateja wenu tunataka mboreshe station,sisi kama wateja wenu tunakosa huduma nyingi za soka mna shindwa nini kutuwekea station 1 au 2 zitakazokua zinatuonyesha mipira? Kama mna weza kununua kampuni ya africa ya kusini nini kinawashinda kusikia kilio chetu cha muda mrefu? Niaibu kuwa na kingamuzi chenu tena mnajitapa ninyi ni kampuni kubwa mnashindwa kutuwekea ligi ya uingereza? Embu jitafakarini kwa kina kama mnataka kuteka soko la tanzania,

prince crown, startimes tunatambua kuwa watanzania wengi wanapenda sana mpira, tena hasa EPL, lakini kwa bahati mbaya wakati startimes inaanza tanzania DSTV alikuwa na exclusive right ya muda mrefu (kama sijakosea mpaka 2014 au 2015) kuonyesha EPL alizopata toka G tv, hivyo si startimes pekee bali hakuna kampuni yeyote tanzania itakayoonyesha EPL mpaka DSTV amalize kipindi chake, na nikuhakikishie kutokana na ukuwaji wa kampuni ya startimes katika bara la afrika tunajua tunaweza kupata right za kuonyesha epl. Kwa sasa tumejitahidi tumepata right za kuonyesha UEFA mpaka mwaka 2015 pia ligi ya UFARANSA na ITALIA.

Hata makampuni mengine ya ving'amuzi bado hawana right za kuonyesha epl ukiacha DSTV tu kwa sasa.
 
Nina maswali hapa chini yanahitaji majibu,

1.Wakati mnasajili kampuni pale Brela,mliandika kuwa mtafanya kazi Tanania bara pekee na Zanzibar haiwahusu?

2.Je na Zanzibar mlisajili kampuni nyingine ya Star times?

3.Kama sivyo,kwanini ving'amuzi nyenu mnavyouza bara haviwezi kufanya kazi Zanzibar vivo hivyo kwa vinavyouzwa Zanzibar?

4.Je kama leseni yenu ya biashara mlichukua kwa ajili ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwanini ukitoka na king'amuzi bara ukifika Zanzibar unaambiwa ulipie shilingi elfu sitini(60,000) ndio uweze kupata huduma Zanzibar?

5.Je ukinunua king'amuzi dar ukienda nacho Arusha hakifanyi kazi mpaka ulipie elfu sitini(60,000) ndio niweze kuona wakati ni ndani ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Nahitaji majibu ya maswali hayo na ukishindwa kujibu na kuleta visingizio ujue nyie ni wezi na wababaishaji na ni kati ya makampuni mengi tu yanayofanya wizi mkubwa kwa watanzania.

habari yako Joseph

startimes ni moja Dar, arusha, Zanzibar, Kenya, Burundi na kwingineko kote tuliko

tulipokuwa tunaanza kutoa huduma dar es salaam tulikuwa tunauza ving'amuzi vya DVBT1 lakini kutokana na kukua kwa technologia na kuangalia baadae kampuni iliamua kufunga mitambo iliyo advanced kidogo mikoa mingine ambayo yenyewe inakubali DVBT2 pekee, hii inamaanisha tuliamua kuanza kuuza ving'amuzi vya DVBT2 pekee mikoani. kwa hiyo kama ulinunua king'amuzi mwanzo Dar kwa kuwa vilikuwa DVBT1 hakitofanya kazi mikoani.

sasa ili kuwasaidia wateja wetu wanaohama toka dar tuliweka utaratibu kuwa mteja haimlazimu kununua king'amuzi kipya cha DVBT2 ila itampasa KULIPIA AKAUNTI YAKE angalau miezi 3 ya uhuru na sisi tutampatia KING'AMUZI KIPYA cha DVBT2. Hiyo 60000 hulipii kubadilisha king'amuzi, hapana! king'amuzi tunakubadilishia bureeee tena kipya ukilipia akaunti yako miezi 3 ya uhuru package. hii inamaana unaondoa usumbufu wa kwenda kulipia kila mwezi
 
Endeleeni kupiga porojo na hao startimes. Mwandishi mwenyewe anayejifanya anaandika hapa anajua kuwa anachokiandika si kweli na anajua kabisa jamaa ni wazushi...

Jamani kuna mtu kasema "small is beautiful"
kwanini wasimalize matatizo madogomadogo kisha waende makubwa???

Dar tegeta wanalia, zanzibar wanalia, tanga ndo usiseme kila na kuibiwa kabisa wameibiwa na kupokonywa Itv, startv TCRA wapo kimya....Zanzibar kilio kama jamaa alivyouliza, mbeya huko nako yaleyale, morogoro mamaaaaa watu walishawachoka wengi wao wana madish na mengi ni zuku na azam pamoja na FTA, kigoma #smile na wengineo ndo yelewiiiiiii!!?

leo free dish kwa hiyo niliyenunua antena na nina kisimbuzi chake, nalazimika kununua kisimbuzi chenu kingine cha dish ha ha ha ha......mimi sidanganyiki!!!!!!!!!
wadanganyike watz wengine ambao mpaka sasa hawajajua uongo na wizi wenu.

Bora digitek na continental na azam tv wapo sehem chache lakini huduma bora na pia ni wazawa wa nchi hii huwezi linganisha quality ya signal ya hawa jamaa na startimes....
startimes wanajivunia ile theory ya #first mover advantage. Lakini hamna kitu.

Naomba washindani wa visimvuzi waendelee kuja tz zaidi na zaidi kuna siku mtajifunza kutoka kwa washindani wenu huduma bora wanazozitoa....

Bila hivyo #Bampami hadanganyiki!!!!
Ni mtz wa kwanza kabisa #kujielewa na #kutopelekeshwapelekeshwa
na hasa anapogunduwa #m /#watu au #kampuni wanataka kuiba hela yake kirahisirahisi tu...!!!!

Sidanganyiki na startimes tena ng'oooooooo!!!!
 
prince crown, startimes tunatambua kuwa watanzania wengi wanapenda sana mpira, tena hasa epl, lakini kwa bahati mbaya wakati startimes inaanza tanzania dstv alikuwa na exclusive right ya muda mrefu (kama sijakosea mpaka 2014 au 2015) kuonyesha epl alizopata toka g tv, hivyo si startimes pekee bali hakuna kampuni yeyote tanzania itakayoonyesha epl mpaka dstv amalize kipindi chake, na nikuhakikishie kutokana na ukuwaji wa kampuni ya startimes katika bara la afrika tunajua tunaweza kupata right za kuonyesha epl. Kwa sasa tumejitahidi tumepata right za kuonyesha uefa mpaka mwaka 2015 pia ligi ya ufaransa na italia.

Hata makampuni mengine ya ving'amuzi bado hawana right za kuonyesha epl ukiacha dstv tu kwa sasa.

asante kwa majibu mazuri,mr startimes: Swali.mmejipangaje kuakikisha mnapata haki za kurusha [epl] baada ya dstv kumaliza mkataba wake? Ushauri wangu ni kweli mna wateja wengi sana kwa sasa nchini,na wateja tunaitaji huduma ya epl cha msingi ni ninyi mjipange kuanzia sasa kuhakikisha mnapata haki ya kuonyesha epl hata mkiweka pakage nyenye bei kidogo kupata soka la epl cctupotayari kwa moyo mweupe,tuondokane na adha za kwenda kwenye mabaa,,naomba kuwasilisha:
 
Mr. Startimes, asante walau kwa kujitokeza kwenye mtandao wa watu. Kweli kuna maswali mengi kuliko majibu kuhusiana na huduma zenu. Mimi ni miongoni mwa wateja wenu wa mwanzo kabisa lakini sijawahi kufurahia huduma zenu tangu mlipoanza. Naishi eneo la mabondeni huku Mbagala Kongowe lakini sipati signal na nimejaribu kuwasiliana na service provders wenu mpaka siku moja nikamlipia nauli aje aniunganishe ameshindwa. Naweza kupata signal mitambo yenu ikipenda, na mimi nikitaka sipati kitu. Sijajua una msaada gani kwangu kama kweli mimi mteja wako ni mfalme. Najaribu tu hata hivyo kwani tangu Dec. sijapata signal ya aina yoyote, na sitegemei kupata suluhisho la tatizo langu. Nasema tena najaribu...ukipenda waweza piga 0762413142
 
Nina maswali hapa chini yanahitaji majibu,

1.Wakati mnasajili kampuni pale Brela,mliandika kuwa mtafanya kazi Tanania bara pekee na Zanzibar haiwahusu?

2.Je na Zanzibar mlisajili kampuni nyingine ya Star times?

3.Kama sivyo,kwanini ving'amuzi nyenu mnavyouza bara haviwezi kufanya kazi Zanzibar vivo hivyo kwa vinavyouzwa Zanzibar?

4.Je kama leseni yenu ya biashara mlichukua kwa ajili ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwanini ukitoka na king'amuzi bara ukifika Zanzibar unaambiwa ulipie shilingi elfu sitini(60,000) ndio uweze kupata huduma Zanzibar?

5.Je ukinunua king'amuzi dar ukienda nacho Arusha hakifanyi kazi mpaka ulipie elfu sitini(60,000) ndio niweze kuona wakati ni ndani ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Nahitaji majibu ya maswali hayo na ukishindwa kujibu na kuleta visingizio ujue nyie ni wezi na wababaishaji na ni kati ya makampuni mengi tu yanayofanya wizi mkubwa kwa watanzania.

Mmmmmh, yaani hata decoder zinadai serikali3!!?? Hii ni kali.
 
habari yako Joseph

startimes ni moja Dar, arusha, Zanzibar, Kenya, Burundi na kwingineko kote tuliko

tulipokuwa tunaanza kutoa huduma dar es salaam tulikuwa tunauza ving'amuzi vya DVBT1 lakini kutokana na kukua kwa technologia na kuangalia baadae kampuni iliamua kufunga mitambo iliyo advanced kidogo mikoa mingine ambayo yenyewe inakubali DVBT2 pekee, hii inamaanisha tuliamua kuanza kuuza ving'amuzi vya DVBT2 pekee mikoani. kwa hiyo kama ulinunua king'amuzi mwanzo Dar kwa kuwa vilikuwa DVBT1 hakitofanya kazi mikoani.

sasa ili kuwasaidia wateja wetu wanaohama toka dar tuliweka utaratibu kuwa mteja haimlazimu kununua king'amuzi kipya cha DVBT2 ila itampasa KULIPIA AKAUNTI YAKE angalau miezi 3 ya uhuru na sisi tutampatia KING'AMUZI KIPYA cha DVBT2. Hiyo 60000 hulipii kubadilisha king'amuzi, hapana! king'amuzi tunakubadilishia bureeee tena kipya ukilipia akaunti yako miezi 3 ya uhuru package. hii inamaana unaondoa usumbufu wa kwenda kulipia kila mwezi

Inashangaza sana kuona mnamlazimisha mteja kulipia kitu ambacho yeye hataki ama hana uwezo,kwanini mlazimishe alipie miezi mitatu?Na huo usumbufu mnaouongelea mmeuona kwa miezi mitatu tu au mna ajenda ya siri hapo?Maana kama ni usumbufu basi mngesema iwe mwaka mzima.

Na kwa kuwa nyie ndio mliobadilisha hiyo mitambo yenu,kwanini mnawaingiza wateja wenu kwenye gharama nyingine ambazo nyie wenyewe ndio mlitakiwa kuzibeba baada ya kuamua kubadilisha ving'amuzi vyenu?

Hivi ving'amuzi mnavyosema mnabadilisha baada ya mteja kuingizwa gharama za kulipia miezi mitatu ambazo hazikubaliki kibiashara,je vilianza lini kuingia katika soko?

USHAURI:Kitengo cha huduma kwa wateja yafaa mkiangalie maana ukipiga simu unapewa taarifa za upotoshaji mkubwa na inaonekana dhahiri wafanyakazi hawana uelewa mkubwa wa huduma mnayoitoa.

elekezea mlingoti wako kisarawe teh ipo siku watasema kuzimu

Wamegundua azam TV na Zuku wanawapiga bao mpaka vijijini watu wanafunga dish hizo

hakuna mwanaume asiecheat labda kileo wa joyce kiria!

Hii sahihi yako mmmmh inatakiwa itafutiwe topic
 
wise boy, habari yako, wateja wetu wengi arusha wanafurahia huduma zetu, kugandaganda kwa picha kunatokana na ufungaji usio sahihi wa antena yako au matatizo ya king'amuzi chako, tafadhari jaribu kuwasiliana na kituo cha huduma kwa wateja arusha watakupatia msaada ufurahie huduma zetu

Swali langu hapo juu hujajibu
 
StarTimes Tanzania, maelezo marefu hasaidii kitu hapa, chukua mawazo yetu kama wateja kuwa huduma yanu hairidhishi, weak signal na poor reception maeneo mengi. Nenda mkafanye kazi tuone mabadiliko vinginevyo hatuhitaji utetezi wako hapa jamvini.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom