Wakuu
Kuna tetesi nimezipata kwamba startimes wataanza kuonyesha EPL siku 11 zijazo
Baada ya kupata hiyo tetesi nimeamua kutembelea page yao ndani ya facebook na nikakuta wameandika kwamba bado siku 11 tutawaletea kitu kizuri zaidi ambacho kila mmoja atakifurahia muendelee kuwa nasi na ku like ili kujua nini kinaendelea.
Kila siku wamekua wakipost kuwa bado siku ngapi leo ni 11 kesho zinabaki 10 hivyohivyo mpaka moja
Minong'ono ya kuonyesha EPL imeendelea kusambaa wanapoulizwa hawataji ninini kinakuja wanaacha kama "suprise" kwa wateja
Natamani iwe hivyo kweli ili ukiritimba wa DSTV uishe
Wadau wa michezo wametamani sana EPL ionyeshwe kwa gharama ya ndogo ya kifurushi
Haya sasa ngoja nisubiri hizo siku