Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Customer care wenu wana dharau sana, hawana ata passion ya kumuhudumia mteja...
 
Asante kwa jibu hilo, pia naomba kuelewa ninalo dish lile kubwa la kizamani yaani maarufu kama ungo je nikichukua hicho king'amuzi cha 48,000 nitaweza cheki chanel kupitia dish langu hilo? Majibu tafadhali ili nichangamkie hicho.
 
Nipo Dodoma na kituo chenu cha huduma watakua wananifahamu nimehangaika sana, imefikia sehemu simu nimewaachia kwa lazima maana walikuwa hawataki kuipokea. lifuatiline hili maana nimeboreka saaana simu nimetumia mwezi imezima, nawafuata nimezungushwa zaidi ya wiki tatu hakuna kinachoeleweka.
 
Star times mnatuchosha,nilinunua kin'gamuzi tarehe 19/12/15,siku ya kwanza na ya pili nilipata chanel za tanzania,star tv na Tv 1 nilizipata,cha kushangaza baada ya hizo siku star tv na tv 1 hazipatikani tena
 
Tafadhari tutumie namba yako ya simu, tutawasiliana nawe na tupate maelezo yako.
 
Star times mnatuchosha,nilinunua kin'gamuzi tarehe 19/12/15,siku ya kwanza na ya pili nilipata chanel za tanzania,star tv na Tv 1 nilizipata,cha kushangaza baada ya hizo siku star tv na tv 1 hazipatikani tena

habari yako, badru Sadick, je unatumia king'amuzi cha antena au cha dishi na je unaishi wapi? pia tujulishe chanel hizo zipo katika orodha ya chanel lakini hazionyeshi au hazipo kabisa. ahsante
 
Asante kwa jibu hilo, pia naomba kuelewa ninalo dish lile kubwa la kizamani yaani maarufu kama ungo je nikichukua hicho king'amuzi cha 48,000 nitaweza cheki chanel kupitia dish langu hilo? Majibu tafadhali ili nichangamkie hicho.

habari yako madish yetu kwa sasa ni madogo, yapo yenye kipenyo cha sm 45 mpaka 60, pia unaweza tumia hata dishi lolote lingine la mtaani
 
Customer care wenu wana dharau sana, hawana ata passion ya kumuhudumia mteja...

habari yako, je ulipata tatizo gani, je ulitatuliwa tatizo lako, tafadhari tutumie namba yako ya simu uliyotumia kupiga simu, pia tujulishe ulipiga simu saa ngapi. ahsante.
 
Me nimeacha kabisa kutumia King'amuzi cha star times, nachanga hela nikanunue cha azam tu maana sina namna
 
Naomba ufafanuzi.
Nina kingamuzi cha Star Times na nilianza kulipia kifurushi cha 20,000 mwaka 2013. kwa kifurushi hicho nilikuwa napata huduma siku 30 kamili yaani kama nimeanza tarehe 20 basi huduma itaenda hadi tarehe 19 au 20 mwezi unaofuata.

Nilihamia kifurushi cha sh 33,000 (hii ni pamoja na TV Sibuka) mwaka 2014. Ajabu siipati huduma hii kwa siku 30, badala yake zikitimia siku 21 huduma inakatikshwa.

Je ndio muda halisi wa gharama ya kifurushi hiki? Sijapata maelezo ya kuridhisha toka kwa wahusika huku niliko.....Zanzibar.
 
Naomba kujuzwa ni lini mtaweka chanel ya Emmanuel Tv na EWTN vitu ambavyo kwa mda mrefu mmeshindwa kuweka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…