Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nzuri sanaKaribuni sana Star media JF, Mjiandae kupongezwa pia kukosolewa na wanaokosoa wanawapenda kiasi cha kuwaambia udhaifu(holes) kwenye huduma zenu ili kesho muwe washindani bora kwenye soko lililojaa ushindani.
Karibuni uwanja huru.
Mi nna tatizo yaani sielewi kwanini muda wa malipo channel zoooote mpaka za nyumbani zinakatika? Ninapatikana Iringa ninatumia king'amuz cha area!Habari zenu wanaJamiiForums
Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?
Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie? Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi
1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi?
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!
STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.
Ahsanteni sana na karibuni nyote
Habari Startimes.Nina king'amuzi cha startime ila tangu tarehe 1/7/2016 ni channel mbili tu zinaonekana yaani tbc1 na tv1.Nimelipia 5,000 leo tarehe 4/7/2016 lakini hakuna channel zilizoongezeka zaidi ya tbc1 na tv1.Habari yako
ndugu mteja, sio kweli kuwa kifurushi cha NYOTA kina matatizo kama unavyofikiri, kama unataka kuhama kifurushi kutoka kifurushi ulichokuwa unalipia awali, ni lazima ubadilishe kifurushi chako, kama awali ulikuwa unatumia kifurushi cha mambo 10000@mwezi alafu ukalipia 4000 bila kubadilisha kufurushi basi fedha yako 4000 itatumika katika kifurushi cha mambo, yaani utaangalia kwa muda wasiku 12 chanel za mambo.
hivyo basi kama awali ulikuwa unatumia kifurushi cha mambo, utakapolipia kifurushi cha NYOTA 4000 ni lazima ubadilishe kifurushi. unaweza kubadilisha kifurushi kwa kupiga namba yetu ya huduma kwa wateja, au kwa kutembelea ofisi zetu au kwa kutumia simu yako ya mkononi kwa kupiga *150*63# kisha ufuate maelekezo utayopewa
ahsante