Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Mm ombi langu ni moja tu namba ya huduma kwa wateja startimes inakuaje mteja ndie akatwe?

Mbona kontinental ni bureeee mm nazan kwa kuwa hiyo ni namba kwa ajir ya wateja wenu bas ni vema iwe free ili mteja awapo na shida iwe rahisi kupata msaada.
 
Mimi king'amuzi changu kinaonesha tbc tu hapa ule utaratibu wa free channels vipi ndugu zangu? nilitop up kipindi mnanipa king'amuzi ili nipewe free local channels ila mmeamua kunimaliza nguvu kabisa with your useless piece of shit.

Sasa ni kwamba tunafanyiana uhuni ama?
 
king'amuzi cha star times kinasumbua sana kwa chanel za itv, star tv na east africa tv ila tbc1 chanel 10 na tv1 zipo vizuri nini tatizo?/
 
mbona startimes hamuoneshi mechi za euro tuelezeni kabla hatujaanza kufikiri kuwahama
 
Karibuni sana Star media JF, Mjiandae kupongezwa pia kukosolewa na wanaokosoa wanawapenda kiasi cha kuwaambia udhaifu(holes) kwenye huduma zenu ili kesho muwe washindani bora kwenye soko lililojaa ushindani.

Karibuni uwanja huru.
nzuri sana
 
Nikilipia kuna channel zinascratch sizpati vizuri local channel tu ndo nazpata sawasawa zngne zinascratch tatzo nn
 
Mi nna tatizo yaani sielewi kwanini muda wa malipo channel zoooote mpaka za nyumbani zinakatika? Ninapatikana Iringa ninatumia king'amuz cha area!
 
Mimi tatizo langu kuhusu malipo naomba kuuliza nikijiunga na kifurushi cha 5000 hakidumu hata mwezi mnakata Chanel jee inamaana vifurushi vyenu vipo kama LUKU kwamba vinaisha kadri ya unavotumia

Namba ya kadi ni hii 02095402031


Phone no 0763717578
 
Tatizo jingine kuna siku watoto wamechezea remote wakalock Chanel moja TBC 2 but password sijui waliingiza zipi naomba msaada wenu 0763717578
 
@StarTimesTanzania acheni utani wa ngumi.
nimenunua kifurushi cha Tsh 12000 ila kilichotokea ni kupata channel kumi tu,
Tbc1, star TV, ITV, yaani zile local channels only,
je ndivyo ilivyo? au tatizo ni nini?
 
Nimesikia mmeshusha gharama ya vifurushi vyenu hadi 12,000/= habari hii ina ukweli wowote?
 
Sina hamu na nyie,nimeamua kugawa king'amuzi tuu,hakina tija kwa sasa,channel hazipatikani,bora tujinyime tununue supersport tuu nyie ovyoo
 
Nikilipia kifurushi cha mambo chaneli za sport sizioni ikiwa kama ofa mlioitangaza
Niko Mbagala no. 02035678993 naombeni msaada juu ya hili
 
Habari Startimes.Nina king'amuzi cha startime ila tangu tarehe 1/7/2016 ni channel mbili tu zinaonekana yaani tbc1 na tv1.Nimelipia 5,000 leo tarehe 4/7/2016 lakini hakuna channel zilizoongezeka zaidi ya tbc1 na tv1.

Je,ni kweli pia mmeondoa local channels ambazo zilikuwa za bure?

Majibu tafadhali.
 
Mimi kingamuzi changu mbona mmenikatia local zote wakati nime kinunua sh 89000/ kunatatizo gani jamani nyie watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…