Karibu jf.
Nadhani suala la ITV/EATV limewapa funzo na nimefurahishwa na jinsi mlivyoamua kujisafisha kwa kusema kuwa hamuusiki na 'kuchafua' channels zao hivyo walau kujivua lawama za kuwahujumu. Na habari njema zaidi naona kuanzia jana scratch walau zimepungua.
Karibuni sana Star media JF, Mjiandae kupongezwa pia kukosolewa na wanaokosoa wanawapenda kiasi cha kuwaambia udhaifu(holes) kwenye huduma zenu ili kesho muwe washindani bora kwenye soko lililojaa ushindani.
Karibuni uwanja huru.
Star times wamejiunga siku nyingi humu! Wewe ni mgeni humu?
Star times wamejiunga siku nyingi humu! Wewe ni mgeni humu?
Mimi nimetapeliwa kama ifuatavyo na nyinyi StarTimes Tanzania soma hapa
Selcom Star times vender MPESA-TZ MATHIAS BYABATO Account no 02035754616 amount TZS......TransID BL52CM284 Reference 01004779647692. feb 2,2015 07:39:25 mpaka leo channel zenu 17 nilizonunua sijapata.nilipouliza kwenu kwa simu nikaelezwa kuwa nisubiri zitaingia zenyewe.mpaka sasa hakuna na nakusanya fedha ninunue kingamuzi kingine.
Habari zenu wanaJamiiForums
Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?
Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie? Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi
1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi?
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!
STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.
Ahsanteni sana na karibuni nyote
Jamaa anakaa kibamba Chanel nyingine zinaonekana vizuri bali zile zinazoonyesha michezo, kama Eurosport, na TBC2 picha zinaganda yaani unasikia sauti lakini picha inayooneka wakati unapobadili station inaendelea kuwa hiyo tu. Cha kushanga hata TBC2 wakati hakuna mpira inakuwa sawa bali wakati wa mpira ndipo kuganda kunapoaanza. Kifurushi cha 20,000/= kwa mwezi.