Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Mimi ombi langu tunaomba mtuwekee channel ya TBC INTERNATIONAL. Tumechagua startimes kwa lengo maalum hivyo ni vyema kabisa tukazipata channels zote za TBC. Niko Singida, CHAGUA STARTIMES UPATE UBORA WA MATANGAZO NA CHANNELS BORA
 
Tbc1 mbeya hakuna sauti ni kububu bubu mtindo 1 fanyeni uchunguzi na mtupe raha
 
Kwakweli kingamuzi chenu pelekeni nchi nyigine mlizokwapua zmetosha,hamfai kutoa huduma kwa watz.
 

Huduma zenu mbovu mno.
 
Ukitaka wakujibu uwasifie.... vinginevyo hawata kujibu. My take nunua visimbuzi vinavyo pigwa promo na ITV
 
Angalieni upya setting zenu za kuselekt kifurushi inakupa wrong kifurushi - yaani nikiselect kifurushi cha kwanza inatoa cha pili hali kadhalika
 
Mimi naishi Boko Basihaya. Hata kama umelipia Kingamuzi cha Uhuru, Hizo TBC, channel 10, unasikia Saudi tu halafu no signal, ITV na EATV scratch tupu
 
Technical Team ya Star Times; Mimi nimejaribu mara nyingi kutumia Star Times lakini picha ni hafifu mno, naona napoteza pesa yangu bure kujiunga na mtandao wenu. Picha zinakatika-katika hivyo sijui mwaka gani mtajirekebisha. It is sad!!!!!!
 
nyie hamna haiba na kazi,customercare anajibu utafikiri kavurugwa loh,hii dijitali hii itatuua mapema
 
Mimi nataka kujua ni lini mtakuwa na channel za movie za hollyhood? mmejaza michaneli ya kinejeria na kihindi na kuweka st movie 1 hata pekee wakati haina movie za maana zaidi drama movie. Mimi nitawahama mda si mrefu
Kwwli mkuu, zamani walikuwa na channel nzuri ile "HBO" sasa hivi haipo. Hawaeleweki na machannel yao.
 

Hicho cha Dish kwanini hakina channels zingine ambazo zinapatika kwenye cha Antenna, mfano "Citizen" ile ya Kenya na zingine nyingi?
 
Mlikuwa mnajitambulisha nini humu kama hamtaki kujibu maswali yetu ya msingi?
Chanels zenu za ajabu ajabu, hata mimi niko mbioni kuwahawama.a
 
mimi mwezi uliopita nimenunua kifurushi cha nyota kikaonesha vizuri tu ila jana nimenunua asubuhi nikakuta mnasema sijalipia nimeshidwa kuelewa kabisa
 
Startimes Tafadhalini naomba muweke huduma ya haraka,huduma hii naona kama inachelewa sana,mimi toka asubuhi ya leo hakuna hata channel moja inayokamata nimejaribu kuseti as default ni mbalaa zaid naishi kitunda antena nimezungusha kila pande za dunia acha na ile ya kisarawe..msaada pl
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…