State Capture and Treason in Tanzania & Tanganyika -The Port Saga

Ukimaliza kunywa bia kakojowe, ujambe, ulale.
 
Wewe akili zako ni za kibongo 100%. Kazi kukosoa huku hujafanya chochote. Kwanza nikuulize: Ni lini yalishaitishwa maandamano kuhusu hili suala? Hakuna maandamano yaliyokwishafanyika. Pili kuomba mchango ni kuonyesha kutojiandaa? Wewe unadhani hata wangejiandaa miaka kumi, gharama za kuendesha kesi zingeshuka kutoka juu? Si lazima zingechangwa na by the way kuchanga ni njia nzuri kabisa ya kuwashirikisha wananchi!
Kesi imeenda vizuri mno mno, na mahakama imeonyesha udhaifu mkubwa kwani imekubali mkataba siyo halali ila wakaogopa kutoa amri ya ni nini kifanyike.
 
Kwani kuna aliyewazuia nyie mnaojivuta kufanya mnayoona ni sahihi? Unataka kuonyesha walioamua kuchukua hatua mapema ndio wamewakwamsha na kuwazuia nyie. Hayo yote uliyotaja mnaweza kuyatekeleza hata sasa.
 
Wadau wajadili kilichojiri leo, nyuma ya pazia je kuna watu wenye ushawishi walioteka dola ?

 
Mwisho umeandika
Tunataka Tanhanyika yetu....daah nimecheka sana. Yaani umesoma hukumu lakini hamna nukuu ata moja umeweka hapa. Kwanini tusiseme wewe muongo?
 
Nshala Rugemeleza hapa ndiyo ingekuwa wakati muafaka wa yeye kutoa tathmini ya uamuzi huu. Inasikitisha sana hayupo tena kwenye huu mjadala.
 
Chifu Mwaihojo - Wananchi wanapinga mfumo .


Chifu Mwaihojo anena maneno mazito kwa chama chake cha CCM baada ya hukumu ya leo

Azungumza kama msomi, mfumo usikilize maoni ya wananchi ndiyo usomi
 
Dr. Wilbrod Slaa - Rais na baraza lake la mawaziri yaani kabineti lenye jumla ya watu wasiozidi 30 wameteka nchi


Alama za nyakati zipo kila mahali kuonesha nchi imehodhiwa na watu wachache ..
 
Dr. Wilbrod Slaa - Rais na baraza lake la mawaziri yaani kabineti lenye jumla ya watu wasiozidi 30 wameteka nchi


Alama za nyakati zipo kila mahali kuonesha nchi imehodhiwa na watu wachache ..
Acheni ujingaa ..
 
Mapinduzi pekee yanayoweza kufanyika ni ya humu Jamii Forum huko mtaani ukijaribu utaumia vibaya sana.

Mkuu wa majeshi Mabeyo alimhakikishia utii rais Samia siku ile wakati wa msiba wa JPM kule Chato.
Nchi hazipinduliwi na wskuu wa majeshi! Rejea vyeo vya maaskari waliojaribu kumpindua Nyerere!
 
Nchi hazipinduliwi na wskuu wa majeshi! Rejea vyeo vya maaskari waliojaribu kumpindua Nyerere!
Sio kwa Tanzania hii mkuu Bulesi, hii ni nchi yenye wana CCM wengi huko jeshini na huwa wanateuliwa kuwa wakuu wa mikoa ya pembezoni kwa mkakati maalum.
 
wewe mwenye akili za ulaya umefanya Nini?
 
Unaelewa unachoandika wewe..hivi tatizo ni kuona au kusikia wizi na utapeli unaofanyika au tatizo ni kuchukua hatua dhidi ya wizi na utapeli unapofanyika..unaweza kuweka huo ustaarabu mpya hata nchi nzima kuona kila linalofanyika lkn bila kuchukua hatua yote hayo ni BURE!
 
Unateseka ukiwa wapi kamanda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…