Stay Strong Zero Brainer

Stay Strong Zero Brainer

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
8.2.2025 pale kwa Tata Madiba, Zero Brainer alishinda TUZO ya mtengeneza maudhui bora ya michezo wa mwaka kutoka TIKTOK.

Tuzo hii ililipa TAIFA la Tanzania heshima kubwa sana, alikuwa anashindana na watu wakubwa kutoka mataifa mbali mbali duniani.
20250223_143505.jpg


Maudhui yake Zero brainer ndio mtanzania anaeongoza kufuatiliwa TANZANIA na kamzidi Followers msanii mkubwa EAST AFRICA Diamond platnumz pale Tiktok kwa kuwa na wafuasi zaidi ya 13.2M mpaka sasa.

Huko instagram jamaa ana wafuasi zaidi ya 2.7M na ndio mtengeneza MAUDHUI mwenye wafuasi wengi kuliko wote wanaolilia tuzo unaowajua wewe hapa TANZANIA.
20250223_143459.jpg


Huko youtube jamaa ana subscribers 2.33M hakuna hata KICHAA mmoja kati ya hao wanaolilia TUZO anaemgusa kwa subscribers.

Content zake hazina UCHAWA, hazina sijui Mama kafanya nini ama Mama amefanya kitu fulani, yeye anakula jezi ambayo inaonyesha kuwa ni mtanzania, mazingira ya Africa kabisa basi (simple and original).
images - 2025-02-23T123519.126.jpeg


Huyu jana ilibidi atambuliwe kwenye jukwaa lile lile lililojaa MACHAWA kwasababu aliletea TAIFA heshima. Ila kwakuwa tuna CHAWA NA WALAMBA VIATU wengi hakuna hata mwaliko aliopewa wala media yoyote kumzunguza.

Ukiongea ukweli huyu Zero Brainer ana mashabiki wengi wanaofuatilia content zake, na anafuatiliwa na watu wengi sana na namba zinaongea. Yeye kutotaka kutambulika jana kwa kulipa heshima taifa wala lisimuumize kwani watanzania tunaelewa kuwa yeye sio mmoja wa vipenzi vya Mama kwa sababu haoneshi uchawa.

Zero Brainer endelea kufurahisha dunia na maudhui yako ambayo hayana HARUFU ZA UCHAWA NA WALA KULAMBA MIGUU WATU. Naamini unatengeneza pesa nyingi sana, na utaendelea kutengeneza nyingi zaidi kwasababu upo kibunifu na sio KICHAWA.
20250223_143505.jpg


Hao watoto wa mama wanaolilia TUZO kisa vipesa vya mboga za majani wacha waendelee kutumika kama BIG G kwenye kampeni, baada ya 2025 kuna NJAA kubwa inakuja kwenye maisha yao hawataamini macho yao.

Stay OG zero brainer 🫡 Stay Strong Captain 💪🏾
 
Hawajapewa wote ila wale nominees 99% walichukuliwa wa cheka tu.
Wapewapuuza wachekeshaji wengine ikiwemo wa 'watu baki'

Na hili lilianza kulalamikiwa pale tu nominees na vipengele vya kugombaniwa vilipotangazwa.

Na ndio maana Baba levo akasema hizi tuzo ni za Coy Mzungu.
Hongera kwao sasa ni wakati wakukitangaza chama kuelekea kampeni za uchaguzi.
 
Kama anapiga pesa kimya kimya ni jambo zuri sana. Watanzania wanga sana walimfanyia uchawi Mbwana Samatta pale Aston Villa kutwa kwenye DM za wachezaji wenzake wanawatukana hawampi pasi Samatta hadi akaachwa msimu mmoja tu.

Ukiona unapiga pesa na Watanzania hawana muda na wewe ni jambo la kushukuru sio kusikitika.
 
Back
Top Bottom