STEALTH (LOW OBSERVABLE) TECHNOLOGY | Teknolojia ya ndege kutoonekana/kutotambulika na rada (RADAR)

B1B Lancer ni toleo la B1 lenye stealth technology zikiwemo radar absorbent materials katika parts mbalimbali.
B1B Lancer ni modification ya original type. Ni sawa useme Sukhoi Su-30 ni ya kawaida alafu Su-30MKI ni stealth. Ndege stealth ni from the prototype wanaamua iwe hivyo, sio wanamodify dege lililopo eti walifanye stealth.
Labda sema B1B inapunguza radar cross section kuliko original B1 lakini sio stealth. Yani hiyo inaonekana kwenye radar kuliko hata F-16, F-15, Mig-35, Jas-39 sasa unaiitaje stealth.
 
Hivi hizi maneno za UFO kama ingekuwa kweli naamini zingeonekana kwenye radar
 
Teknolojia ya stealth ni pana sana. Pia ni endelevu.

Hizo modification unazosema, nimekwisha kuzisema pia hapa. Na katika suala la hizo modifications,

1) Unamodify nini ama kitu gani?
2) Unamodify ili iweje?
3) Unatumia mbinu zipi?

Kama nilivyosema, teknolojia ya stealth ni muunganiko wa mbinu mbalimbali ambazo hutumika kupunguza radar cross section ya vitu mbalimbali. Kusudi lake ni kuvifanya visionekane kirahisi ama visitambulike na rada. Katika uchambuzi makini wa kiufundi kuhusu B1B Lancer, hizo mbinu zimetumika na zilifanyika kwa makusudi na sababu maalumu.

B1B Lancer ilitokana na kitu kinachoitwa 'redesign' . Yaani muundo wa B1 uliokuwepo ulibadilishwa kwa kuundwa na kuwekewa 'features' nyingine mbalimbali ambazo hazikuwepo hapo kabla, kuanzia muonekano mpaka katika utendaji kazi.

Pia, tukirejea katika ufafanuzi wa kile nilichokileta, zijazungumzia stealth fighters ama stealth bombers bali nimezungumzia STEALTH ama LOW OBSERVABLE TECHNOLOGY kwa ujumla wake.
 
Ukweli ni kwamba hii technology ni kwa Nchi kama zetu hizi, ila sio upeleke nchi kama Urusi yenye Rada tofauti tofauti zaidi ya 200 alafu utegemee utatoboa.utakufa mchana kweupe.
 
Point yangu ni ileile, Rockwell B1B Lancer sio stealth hata kidogo. Nimeona inaoneshwa ina radar cross section ya 1.02 square metre, pengine nimeona 0.72 sq metre na hivyo hatuwezi kuiita stealth.
Ndege kama HAL Tejas ina RCS ya 0.5 sq metre na haiitwi wala hawajawahi kukosea kuiita stealth.
Ingawa kuwa na RCS ndogo hivi kwa ukubwa wake ni jitihada kubwa lakini hakuifanyi iwe stealth. Iko low observable tu kulinganisha na bombers nyingine.
 
Ukweli ni kwamba hii technology ni kwa Nchi kama zetu hizi, ila sio upeleke nchi kama Urusi yenye Rada tofauti tofauti zaidi ya 200 alafu utegemee utatoboa.utakufa mchana kweupe.
Teknolojia hii ya stealth ni kwa yeyote mwenye uwezo wa kuwa nayo.

Stealth ni hitaji la majeshi mengi duniani. Kuanzia yule mwenye uwezo na hata yule asiye na uwezo wa kufanya hivyo na imekuwa hivyo tokea miaka mingi sana. Tangu enzi na enzi.

In fact, kuwa stealth ni NATURE ya binadamu yeyote.

Stealth haina tofauti na Privacy katika maisha ya kila siku. Kila mmoja wetu anapenda kufanya mambo yake fulani fulani kwa uhuru, bila bughudha wala usumbufu na bila wengine kujua ama kugundua kuwa anafanya kitu gani kwa wakati huo.

Kila mmoja huwa huru zaidi kufanya mambo mengi fulani fulani ambayo asingeweza kuyafanya in public ama mbele ya macho ya wengi. Ni jambo la kawaida kabisa ambalo lipo kwa kila aliye na akili timamu. Na katika stealth pia ni vivyo hivyo!

Hili ni hitaji la kila mtu.
Mataifa makubwa kijeshi; Marekani, China, Urusi uliyoitaja na mataifa mengineyo yamekuwa katika uwekezaji wa teknolojia hii ya stealth kwa muda mrefu sasa. Tofauti iliyopo hapo ni kwamba kila mmoja anafanya kuendana na uwezo wake.
 
Unaposema kuwa B1B Lancer "sio stealth hata kidogo" kisha hapohapo tena unasema "iko low observable", huoni utofauti hapo?

Nini maana ya STEALTH na nini maana ya LOW OBSERVABLE?

STEALTH ndio LOW OBSERVABLE.

Katika masuala ya kijeshi, stealth na low observable ni vitu vinavyofanana. Yaani ni vitu vyenye maana sawa, ama kwa kifupi ni kitu kilekile. Ndio maana teknolojia hii kwa ujumla wake hufahamika kama STEALTH TECHNOLOGY vilevile pia hufahamika kama LOW OBSERVABLE TECHNOLOGY. Yote ni sawa!
 
Low observability inatokea wakitumia materials na tech kupunguza radar cross section kwa kiasi fulani. Stealth wanaanza tangu mwanzo kutengeneza shape ya kila eneo, engine maalumu, air intakes zake, wings na hata bomb bays. Ndio maana hata Su-57 haijakamilika kwa kuwa engine yake ya Izdeliye haijatengenezwa. Engine iliyopo inatumika kwenye Su-35 lakini sio kwa ajili ya stealth fighter hivo itafanya ndege ionekane kirahisi kwenye radar.

Hiyo B1B ina external hardpoints za kubebea mabomu sasa unaiitaje stealth. Ingawa hizi F-22 na J-20 zinaweza kubeba mabomu nje lakini kwenye situation hiyo hazichezi kama stealth. Hizo F-22 mission zake kadhaa inafanya ikiwa sio stealth kupunguza gharama za maintenance. Ni sawa uchukue ndege ya Airbus ya AirTanzania uweke radar absorbing materials kisha uiite stealth, si sahihi.
 
Low observability inatokea wakitumia materials na tech kupunguza radar cross section kwa kiasi fulani.
Nilisema hapo awali kwamba, teknolojia ya stealth ni pana sana. Pia ni endelevu.

Hiyo "low observability" unayoisema kutokana na kupunguza radar cross section ndio stealth yenyewe. Low observable ndio stealth hali kadhalika stealth ndio low observable.

Kitu kikishakuwa "low observable" kuliko umbo lake la kawaida, tayari hapo kuna utofauti. Na utofauti huo hauji hivihivi tu bali kuna processes ambazo zimefanyika kwa makusudi maalumu. Hizo processes ndio teknolojia yenyewe hiyo ambayo tunaiita STEALTH ama LOW OBSERVABLE TECHNOLOGY.

Unaposema kitu fulani "sio stealth hata kidogo" kisha hapohapo unasema kiko "low observable" ni contradiction. Unachanganya mambo.

Stealth wanaanza tangu mwanzo kutengeneza shape ya kila eneo, engine maalumu, air intakes zake, wings na hata bomb bays.
Haijalishi kuanzia mwanzo ama kuanzia katikati. Kuna mabadiliko mbalimbali kimipango yanayoweza kutokea kutokana na sababu kadha wa kadha zikiwemo za kisiasa. Kinachojalisha ni nyenzo, mbinu ama teknolojia inayotumika na ndicho kilichopo hapa.

Ni teknolojia gani imetumika kupunguza radar cross section katika B1B Lancer?

Nilisema hapo awali kwamba, B1B Lancer ilitokana na kitu kinachoitwa 'redesign' kimuundo na haiko kama B1 ya awali. B1 ya awali iliishia kwenye prototype, mradi ukafutiliwa mbali hata kwenye production haukuingia.

Kuna utofauti mkubwa sana kati ya hizo ndege mbili yaani, B1B pamoja na B1 ya awali, kuanzia shape, engines, inlets, wings, weapon bays n.k. Na zaidi ya hapo hata katika utendajikazi (performance) wa hizo ndege mbili ni tofauti kabisa.

Hiyo B1B ina external hardpoints za kubebea mabomu sasa unaiitaje stealth.
External hardpoints zipo katika ndege zenye uwezo wa stealth na hata zisizo na uwezo huo. Hata F-22 Raptor stealth fighter ina external hardpoints. Hizo external hardpoints huwa zinatumika katika missions maalumu na si mara zote.

Ni sawa uchukue ndege ya Airbus ya AirTanzania uweke radar absorbing materials kisha uiite stealth, si sahihi.
Mfano huo ulioutoa hauendani kabisa na kile kilichofanyika katika B1B Lancer. Ni dhahiri kuwa hufahamu ni nini kilifanyika katika B1B Lancer. Mfano wako huo umethibitisha hilo!

Nitarudia:
B1B Lancer ilitokana na kitu kinachoitwa 'redesign'. Muundo wa B1 uliokuwepo ulibadilishwa kwa kufanywa ama kuundwa upya kutokana na mabadiliko ya kimahitaji. Ninachozungumzia hapa ni muundo (design) na si 'end product' kama hiyo "Airbus ya Air Tanzania" uliyoisema.

Fahamu kwamba, tunapozungumzia teknolojia ya STEALTH ama LOW OBSERVABLE hatuzungumzii "stealth bombers" ama "stealth fighters" in particular...La Hasha!...bali tunaizungumzia teknolojia kama teknolojia. Tunazungumzia STEALTH ama LOW OBSERVABLE TECHNOLOGY kwa ujumla wake.

Baada ya kusema hayo, nikushukuru pia kwa mchango wako.
 
Kazi nzuri.
 
Unaweza kuweka data za USAF zinazoonesha kuwa B1B Lancer ni stealth bomber. Yani uweke data za watengenezaji na wamiliki tuachane na za kwetu sisi mashabiki.
 
Unaweza kuweka data za USAF zinazoonesha kuwa B1B Lancer ni stealth bomber. Yani uweke data za watengenezaji na wamiliki tuachane na za kwetu sisi mashabiki.
Unarudia kosa lilelile!

Unachanganya kati ya "stealth bomber" na "stealth technology". Hivyo ni vitu viwili tofauti.

Nilisema na ninarudia;
Tunapozungumzia teknolojia ya stealth ama low observable hatuzungumzii "stealth bombers" ama "stealth fighters" hasa, bali tunaizungumzia teknolojia yenyewe ya stealth. Tunazungumzia STEALTH ama LOW OBSERVABLE TECHNOLOGY kwa ujumla wake.

Stealth bombers ama stealth fighters ni 'end products' ama ni matokeo tu yanayotokana na teknolojia hii ya stealth ama low observable. Teknolojia ya stealth kwa ujumla wake ni pana sana.
 
Basi nauliza hivi, unaweza kuweka data zinazoonesha B1B Lancer ni stealth? Data zitoke USAF- operators au Boeing- manufacturer.
 
Nimekukosoa kuiita B1B kuwa ni stealth, hii sio stealth. Sasa unanambiaje nachanganya kati ya stealth bomber na stealth technology? Kama bomber iko stealth simply tutasema stealth bomber. Hizo B-2 utasikia zinaitwa stealth kabisa bila kukwepa.
Bishana pia na Business Insider. Umeandika article nzuri lakini unabisha kitu wazi kabisa.
Kosa lingine unalofanya ni kuona "low observability" na "stealth" ni vitu sawa. Yani kwenye radar kuna tofauti kubwa mno katika hivyo vitu, huwezi kubeba B1B ikafanye mission ndani ya space ya Russia bila kufanya utangulizi wa kina B-2, F-22 au F-35.
 
Russia’s Defense Ministry said on May 29 statement that “Su-27P and Su-30SM fighters from the air defense alert quick reaction forces of the Southern Military District were scrambled to intercept the targets.”

The crews of the Russian fighter jets approached the air targets within a safe distance and identified them as B-1B strategic aircraft, after which “the US bombers changed their flight course and flew away from the state border of Russia,” the statement runs.

The statement also claimed that the US strategic bombers over the Baltic and Black Seas “were timely uncovered” by the air defense alert quick reaction forces of the Western and Southern Military Districts. The B-1s were tracked by Russian radars at a considerable distance from Russia’s border.

>>> Ulishawahi kusikia B-2, F-22 au F-35 imekuwa intercepted? Turudi kwenye mada, kubali kuwa umekosea kuiita B1B Lancer ni stealth.
 
Hii ndio raha ya ugomvi wa wasomi(GT), mtu unapata elimu ya buuure.

Sasa hapa assume majibizano yenu yangekua majukwaa kama ya celebrity au la siasa.

Sasa hivi tungekua tushajifunza mpaka matusi mapya.

Hongereni sana kwa majibizano(ugomvi) yenu wakuu
 
Ndio maana nikasema kwamba unachanganya. Stealth bomber na stealth technology ni vitu viwili tofauti. Moja ni product ya teknolojia huku nyingine ni teknolojia yenyewe in general na ina vitu vingi sana ndani yake.

Nilisema hapo awali kuwa teknolojia ya stealth ni pana sana na ni endelevu. Ukiyasoma maelezo yote niliyowasilisha hapa utapata kulifahamu vyema hilo.

Unaposema kitu ni "low observable" na wakati huohuo unasema "sio stealth hata kidogo" technically nikueleweje?

Unadhani ni kwanini stealth technology huitwa low observable technology?

Nikuulize maswali mengine mawili yaliyoko ndani ya mjadala:

1) Nini maana ya stealth?
2) Nini maana ya stealth technology?
 
Unasema nimekosea.

Sawa! Let's assume nimekosea. Je, unaweza kunionesha mahali nilipokosea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…