STEALTH (LOW OBSERVABLE) TECHNOLOGY | Teknolojia ya ndege kutoonekana/kutotambulika na rada (RADAR)

Kwa Africa ukiwa na SU-30 6 tu ni nyingi sana ndugu, yani unahesabika kuwa una jeshi la Anga bora.sisi wenyewe tuna JF-7 (11) na JF-6 (3) tu na bado tunatamba
Sisi si tuna J-7G?
JF si huwa ni za Pakistan, sijawahi sikia JF katika jeshi lolote tofauti na Pakistan ambazo walishirikiana na China kutengeneza.
Kwa Afrika tunatamba kwa sababu ya kuwa na army kwa vile air forces hazina ushindani sana. Wenye ndege za kuheshimika ni Egypt ambao wanaongeza Su au Mig kama 24, Algeria wenye jets kadhaa kutoka Russia na South Africa wenye Jas-39 Grippen kadhaa.
Waliobaki ndo kina Uganda wenye airframes 6 then sisi wengine tunapishana huku. Hata ranks za kijeshi huwezi sema Tz tupo top 7 kwa Africa.
 
Hapa nilipoanza kuona Elbit Systems nikashtuka maana najua ni ya Israel. Hizo Mig-21 zina versions nyingi ambazo ni upgraded hivo vigumu kujua zote. Notably hata India walikuwa na upgrade nakumbuka wameziground mwaka huu.
North Korea wanazo na nchi kibao za former Soviet block. Pia Waarabu wengi kina Syria wanazo. Kumbuka Mig-21 is one of the most mass produced jet in the world, I think ni #1.
 
Pamoja sana, nipe kidogo maelezo ya Suppression of Enemy Air Defence (SEAD) na Destruction of Enemy Air Defence (DEAD) na Electronic Warfare (EW) katika habari za Air defence huwa kidogo vinanichanganya mkuu.
DEAD/SEAD inahusika na kuzifanya air defence system zisiwe in operations mfano kwa kuzijam au kutumia electronic warfare. Hii inaweza tokea kwa muda tu, then badae wakarejea kwenye mfumo wao. Hii wanafanya kuweza tekeleza shambulizi moja mfano Israel ilipoenda kushambulia kinu cha nyuklia cha Iraq na cha Syria. Hapa ndege kama E2D Advanced Hawkeye inatumika kujam radar, hata hivo fighters nyingi zinajitahidi kuwa na jamming capabilities. Mfano, Israel wanashambulia anga la Syria lakini hawaharibu ovyo air defence systems zao.

Pia wanaharibu kabisa air defence systems kama wana mpango endelevu wa vita. Hii ni adui wa ile Anti-Access/Area Denial (A2/AD). Hapa DEAD/SEAD ndo inahusisha sana na hiyo stealth technology na ndo lengo lake kuu. Unakuta mfumo kama S-300 unashambuliwa na F-22 Raptor kisha unaharibiwa then zinakuja B1B zikiwa na escort labda ya F-18 kudondosha mabomu kwenye miundombinu ya kijeshi. Mfano, nchini Iraq coalition forces waliharibu air defence systems kabla ya ground troops kuja.
 
Nilikosea, nilitaka kusema F-7 na J-6.
 
Hayo mambo waachieni wayahudi ambao wao hupenetrate radar na kuchange configuration .. wakisha pita wanarudisha kama awali..
 
Viongozi wetu wanajisahau sana kwenye kuboresha majeshi yetu ndo maana wazungu wanakuja kwetu na kufanya wanavyotaka.kama hauna nguvu kwenye air force basi ni ngumu sana kushinda vita kwa sasa maana uwezi kutembeza chochote kile pasipo kulipuliwa na maadaui.
Labda uwe na mifumo ya ulinzi yenye uwezo wa hali ya juu sana ndo unaweza kujitetea.hapo utakuwa umejikomboa kwenye No fly zote
 
T14 Armata na FRANC THE GREAT hawa wajamaa nawaelewa sana sijawahi bishana nao ama kuwaona wakibishana kwamatusi


Ila FRANC THE GREAT inaweza kua umenikosea sana MKUU hujanitag kwahili bandiko napata shida sasa kulisoma ila kazi njema mnooooo kongole.....
 
Turkey kwa tech iko vizuri tu,,mfano componets nyingi za F-35 project inategemea kutoka Turkey,,imagine hata fuselage,watu wanaichukulia poa Turkey,lakini hawa watu mziki wake si kidogo,,kwasada baada ya kutolewa katika mpango wa F-35,wanaunda stealth fighter yao iko kwenye pipeline
 
Hakuna muarabu mwenye akili ya kufanya ivyo ndugu wala tusiongopeane kwa ilo.
Turkey atakaa miaka 100 na bado hataweza kutengeneza ndege kama f-22, f-35 au su-57.
 
Nimesema wasio giants si kwamba nawachukulia poa Turkey lakini ukiambiwa taja tech giants Turkey haipo. Haiwezi izidi South Korea, Japan, Italy, Israel, Spain, Australia na nchi nyingine ambazo zinajulikana. Components za F-35 ilizokuwa itengeneze ni chache na insignificant, walipewa ili kupunguza production cost na kuwafanya wajione wanahusika na project.

Hiyo stealth fighter nakuhakikishia miaka zaidi ya 25 ndo watakuja kuwa nayo, tech gap bado kubwa. Russia kaanza project ya Su-50 tangu mwaka 2002 hadi leo hana hata squadron sembuse Turkey ambaye hajawahi hata kutengeneza fighter.
 
Labda kuna mifumo imara na thabiti ya kukabiliana na hizo ndege na missiles kama PAC3 hatuwezi jua mkuu.
 
Nafurahi pia kuona uwepo wako..
 
F 35 na f 117 ipi yenye uwezo mkubwa?
Neno "uwezo" ni neno pana sana. Pengine swali lingelenga zaidi katika nyanja fulani. Mfano; uwezo wa stealth, uwezo wa mashambulizi n.k.

Isitoshe ndege hizo mbili zinatofautiana sana kuanzia kimuundo, majukumu n.k. Ulinganisho wa vitu unahitaji zaidi kusimamia katika msingi fulani.

Karibu!
 
Kwahiyo majadiliano yalifaa kuwa hii ni bomber na hii ni fighter badala ya hii ni bomber/fighter na hii ni Stealth
Tunaweza kujadili kwamba zana fulani ni bomber ama ni fighter. Pia tunaweza kujadili kuhusiana na zana mojawapo tu kati ya hizo (fighter/bomber) kwamba, ni stealth ama sio stealth kama ilivyokuwa katika mjadala.

Namna hiyo!
 
Mkuu FRANC THE GREAT upo kimya tuliishia na RADAR ABSORBING, Kwa habari za RAM na RAM.

Naamini muda mzuri kuendelea
Nilikuwa occupied na mambo mengine ila nimerejea.

Tuliishia hapo katika maelezo na tumekuwa tukielendelea kujadili masuala kadha wa kadha kuhusiana na STEALTH ama LOW OBSERVABLE TECHNOLOGY kwa ujumla wake.

Tunaendelea!
 
Nakushukuru nawe pia kwa kulisoma bandiko hili. Pia, niwie radhi kwa hilo na kwa changamoto uliyoipata katika kulisoma bandiko hili.

Karibu sana!
 
Japan ni miongoni mwa mataifa machache yenye mpango wa uundwaji wa ndege mahususi za stealth ambapo uzalishwaji wake utaanza mwaka 2031, miaka takribani 11 ijayo.

Wizara ya Ulinzi ya Japan imekwisha tenga dola za Kimarekani milioni 102 katika bajeti ya mwaka huu sawa na shilingi za Kitanzania takribani bilioni 237 kwa ajili ya utekelezwaji wa mpango huo sambamba na gharama zingine. Ndege hizo zitaanza kutumika rasmi panapo mwaka 2035 baada ya uzalishwaji wake.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…