Stendi Kuu za Mabasi Kigoma na Kaliua- Mabwana Afya wajipime

Stendi Kuu za Mabasi Kigoma na Kaliua- Mabwana Afya wajipime

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
25,225
Reaction score
25,488
Salaamu Wakuu: Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Sote tuitikie: Kazi Iendelee!

Moja kwa moja kwenye mada.

Mbali na utaratibu mzuri walionao uongozi wa stendi wa kuwaelekeza utaratibu wa hapo stendi wasafiri wanaotumia eneo hilo wakati wa alfajiri; bado Bwana Afya anayekagua masuala ya usafi eneo hilo ameshindwa kutekeleza wajibu wake.

Vyoo vya abiria stendini hapo ni vichafu kupindukia! Ajipime muhusika huyo vile vile na uongozi ujitafakari juu ya kwa nini wanakusanya ushuru wa kutumia vyoo hivyo lakini bado wanaacha vyoo katika Hali Ile!

Ujumbe huu uwafikie Bwana Afya anayehudumia maeneo ya stendi ya Kaliua- na uongozi wa stendi hiyo!

N.B: Ujumbe huu pia uwafikie baadhi ya wale wanaohudumia vivuko mfano pale Jijini Mwanza!

Hapa natimiza wajibu kwani nipo katika kutekeleza mikakati ya kumshida adui tuliyetangaziwa awamu ya kwanza anayeitwa "Maradhi" ambaye hutumia mamuluki wake uchafu.

Karibuni kwenye mikakati ya namna hii.

Natanguliza Shukrani.
 
Uzi huu bila picha ni majungu tu!
Kweli hapa nimechemka ! Wakati mwingine nitaweka ushahidi.

Lakini, Nina imani wapinga maradhi waliopo maeneo hayo wataleta ushahidi. Na kama wakikuta pamesafishwa huo utakuwa ushindi kwa wote tunaopambana na Mamuluki Uchafu anayetumiwa na Adui Maradhi!
 
Back
Top Bottom