Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Stendi ya Mabasi ya Dkt. Samia imeanza rasmi kutoa huduma za usafirishaji leo Mei 27, 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, mkoani Manyara, ikiwa ni hatua muhimu katika kuboresha miundombinu ya usafiri na kukuza shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.
Stendi hiyo ya kisasa inatarajiwa kurahisisha safari za abiria na mizigo ndani na nje ya wilaya, sambamba na kuongeza mapato ya halmashauri kupitia ada mbalimbali za usafirishaji.
Akizungumza wakati wa kikao na wadau mbalimbali wa usafirishaji, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, alieleza kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwa ni pamoja na kutangaza rasmi meneja wa stendi hiyo mpya.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa mujibu wa utaratibu mpya uliowekwa na halmashauri, mabasi yote makubwa, madogo na magari mengine ya abiria yatatakiwa kuondoka na kuwasili kupitia stendi hiyo pekee.
Irafay amesisitiza kuwa haitaruhusiwa tena magari ya abiria kupakia au kushusha abiria katika maeneo yasiyo rasmi, hatua inayolenga kudhibiti uchafuzi wa mazingira na msongamano wa magari katika mji wa Katesh.
Aidha, ametoa wito kwa wamiliki wa magari, madereva, mawakala wa mabasi na wafanyabiashara kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya matumizi ya stendi hiyo na kusisitiza umuhimu wa kudumisha usafi katika eneo hilo ili kulinda afya za watumiaji na kulifanya jiji kuwa na mandhari ya kuvutia.