Stendi ya Magufuli Kuna kelele sana

Stendi ya Magufuli Kuna kelele sana

Trubarg

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2020
Posts
4,388
Reaction score
7,223
Sijui ni ubunifu au ni kitu Gani. Stand ya Mabasi ya Magufuli ni stand ukiwemo huwezi mpigia mtu simu akakuelewa..yaani ni makelele ya spika na matangazo mwanzo mwisho, Kariakoo Kuna uafadhali. Najiuliza kwani uongozi wa hii stand hawalioni hili?

Kama ni wao ndiyo Wana regulate haya matangazo ni kwanini wasiweke utaratibu unaoeleweka kukawa na utulivu ..ikitokea una mgeni pale inakulazimu umwambie atoke nje ya stand ndo aweze kukupigia simu Ili muelewane.

Nashauri viongozi wapeee tripu ya mafunzo pale airport, Ili waone kwa vitendo wenzako wanafanya vipii matangazo bila kuadhiri utivu wa abiria..
 
Tanzania kuna kelele sana hata mahali pa kazi kila kitu kipo disorganized.

Ukitaka kujua kuwa tunaishi kama watu wasio na utaratibu wowote toka tu nje ya nchi hata hapo kenya tu au uganda utaona aibu mwenyewe.

Hakuna tunalolifanya lipo katika utaratibu makelele yapo kila mahali halafu sasa tumejaa ujuaji mwingiii.

Anyways tupo nyuma sana kwenye swala la ustaarabu ila Mungu atatubadili with time.
 
Kenya na Uganda hapana..hakuna la kujifunza huko nao wanamakelele Zaidi ya tz
 
Simu gani hio mbona sisi tunapigiana na kuelewana vizuri kabisa... Una point nzuri sema exaggeration imekua kubwa
Mara ya mwisho nilikuwa hapo Leo...mgeni wangu tulishindwa elewana nikamwambue atoke nje ya stand ndo tukaelewana..wewe ulienda lini hapo
 
Kelele ni sehemu ya maisha ya Mtanzania
 
Ni muendelezo wa vitu, mambo yetu kukosa utaratibu...
 
Karibu kila siku naingia MBT boss
Utakuwa umekuwa saturated na hayo makelele...yaani ubongo wako na akili zako uneyazoea kiasi kwamba unaona ni normal..kama ilivyo madaktari na manesi hospitali jinsi ambacho hawasikiagi Ile harufu ya chlorine na madawa.
 
Back
Top Bottom