Stendi ya Magufuli Mbezi Mwisho hakuna huduma ya maji kwenye vyoo na sehemu nyingine siku ya tatu sasa

Stendi ya Magufuli Mbezi Mwisho hakuna huduma ya maji kwenye vyoo na sehemu nyingine siku ya tatu sasa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Taarifa Jamii Forums hali ni mbaya kwenye Stendi ya Mabasi makubwa iliyopo Mbezi Luis maarufu kama Mbezi Mwisho, hakuna huduma ya maji kwa muda wa siku tatu sasa.

Kuanzia juzi Machi 26, 2023 hadi ninavyoandika muda huu asubuhi ya Machi 28, 2023, mamlaka zitusaidie

Kwenye vyoo napo mambo si mambo, unaweza kufikiria kama huduma ya maji hakuna, watu wanatumiaje hivyo vyoo.

=========

Meneja wa stendi hiyo, Isihaka Waziri

Meneja wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli, Isihaka Waziri amesema “Ni kweli tumepata changamoto kidogo, DAWASA hawana maji tangu Ijumaa kutokana na marekebisho ambayo wanafanya Ruvu Juu na Ruvu Chini.

“Hivyo tukawa tunatumia maj ya akiba ambayo nayo yametuishia, DAWASA waahidi kutuletea maji jana (Machi 27, 2023) lakini wakiwa njiani napo wakajulishwa kuwa Mloganzila hakuna maji, ikabidi wayapeleke huko.

“Usiku wa saa saba tukapata maji, lakini bahati mbaya pampu yetu nayo ikaharibika, hivyo mafundi wanaendelea kama kawaida.

“Huduma ya vyoo eneo la chini zimesimama kwa kuwa marekebisho yanaendelea.

“DAWASA wamesema baadaye maji yanaweza kuwa yamerejea.”
 
Nasikia hata mloganzila kamba hii ni mbaya, bora maji yakose huko stand kukiho hospital
 
Hii ni dhuruma ya hali ya juu kwa wananchi maana wanalipia getini alafu huduma muhimu kama hiyo inakosekana
 
Watu kwenye kujisaidia haja kubwa basi shuguli

Ova
 
Back
Top Bottom