Watumiaji wa Stendi ya NaneNane Mkoani Mbeya tuna changamoto inayohusiana na usalama wetu, kwani nyakati za Usiku abiria wanaoshuka hapo wanakutana na giza kwa asilimia kubwa.
Taa zipo ila haziwaki, tunateseka sana, tunalazimika kutumia mwanga wa simu, hatujajua shida nini.