Step 10: Nilivyowekeza laki moja hadi kuanza kutengeneza milioni moja kila siku 3 (step by step)


Nitaelezea kwa urefu as soon as possible, hii post ni kama introduction tu.
 

Sana sana natumi ALibaba, made-in-china, globalsource, aliexpress, banggood, kwa mizigo kutoka china. ebay, amazon na kwingine pia kwa bidhaa za marekani na kwingine.. inategemea wapi ntapata mzigo nnaoutaka kwa bei nafuu kuliko wote, ukijumuisha usafirishaji.
 
Umeelezea vizuri Sana ila jambo la muhimu kabisa umeliacha,

Hebu elezea baada ya kupata mteja malipo yanafanywaje ili pasitokee dhuluma kati ya mnunuzi na muuzaji??

Inategemea mauzo utayafanya vipi, kwa dar-es-salaam ambapo mimi nipo unaweza ukatumia delivery services ambazo zipo, kama unauza kupitia jumia na kwingine unaweza ukatumia delivery service zao, kama utauza mwenyewe kuna delivery services (ambazo ntakuja kuzielezea) , unaweza tafuta na watu wako pia (ambayo ndo nnachofanya siku hizi) na waka lipa on delivery. Kwa mikoani, hapa ndio branding inapohitajika, uki brand vizuri na kuji present kama biashara iliyosimama, watu wanakuamini, then wawili watatu ukishawatumia mizigo yao na wakakupa confirmation kuwa wamepokea, wanaofuata unaweza unawaonesha confirmation za wengine na reciept za mabasi unayotua, hiyo tu inatosha kuweza kupokea malipo kwa m-pesa/tigopesa. Mengine ntaelezea soon
 
Tunaomba pia kujua taratibu za kodi zimekaaje? MZIGO unasafirishwa kwa ndege au meli?
mzigo unasafirishwa kwa ndege... maana naongelea mizigo ya piece 20-100 tu.. meli ni ma container. Kodi vinalipiwa, ni muhimu kwa sikuhizi, cha maana ni kupata bei nzuri ya kununulia ili uje ulipe kodi isyo kubwa sana. Ila kama unaanza na mizigo mdogo piece mbili, tano hadi kumi hivi kama ni vya gharama ndogo unaweza usilipie pia, will talk about this too soon.
 
Salute Mkuu.. ila changamoto Ipo Kwenye Bidhaa Kuchelewa Kufika Mimi Kuna Bidhaa Naagiza Ila Imeshachukua miezi Miwili... Kenya Wanaiba Sana Mizigo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…