Step by step nilivyo agiza bidhaa kutoka AliExpress

Ulizwa swali lolote kuhusu M-pesa master card nitakujibu.
Ninakaribia mwaka sasa toka nianzw kutumia M-pesa master card na hususan Aliexpress.
Wanacharge bei gani kwa transaction?
Vipi kuhusu refund, inachukuwa muda gani? Huduma ya customer ikoje huko in case una shida
 
Wanacharge bei gani kwa transaction?
Vipi kuhusu refund, inachukuwa muda gani? Huduma ya customer ikoje huko in case una shida
Hakuna chaji kwa transaction, ila kuna tofauti ya exchange rate ambayo ni ndogo sana.
Kama uanakidhi vigezo vya kurudisha utajaza conflict dispute form na utarudishiwa pesa yako baada ya kuwasiliana na seller na kuthibitisha kuwa kweli unaatahili refund.
 
Elimu nzuri sana hii, binafsi natumia M-pesa mastercard. Ni rahisi sana na haina usumbufu wa aina yoyote. Changamoto ya kuagiza vitu Aliexpress zipo, kwa mfano binafsi nilishatumiwa mzigo feki kama mara 2. Hivi sasa naagiza Amazon na Ebay tu baada ya hizo changamoto.
 
Mkuu hizo simu zilivyofika posta hukulipia kodi zozote zile??
Mkuu soma hapa utapata picha ya swali lako pia hii itawasaidia na wengine pia

*Kwanza download application ya alixpress kwenye simu yako

* application ikifunguka jisajili kwa kuweka email yako and password zako kumbuka kuhifadhi password vyema ili ikitokea ume unistall hiyo application ukija ku download upya irudi account yako ileile ya awali

*Ingia kwenye application yako ya alixpress kwenye setting tafuta sehem pameandikwa
Shipping adresse hapo ingiza Adress yako
Kwamba unaitwa nani, unakaa wapi, Namba zako za simu zilizopo hewani, post code yako. N.k kisha save

* Tafuta kitu unachotaka kununua ukipata fuata process za kununua hapo hapo kwenye ulipoonea hicho kifaa itakuonyesha pia na shipping cost
Fuata maelekezo hayo ya kununua yatakupeleka mpaka kwenye namna ya kununua hapo utatumia credit card yako ya Visa au Master card au M pesa master card
salio lako litatumwa kwa alixpress baada malipo yako kuwa confirmed
Seller ataanza ku process mzigo wako
Mara nyingi ni 5days then atautuma kwa shipping company

* mzigo wako utatumwa na selller kwa kupitia shipping company uliyo chagua
Kazi yako hapo ww itakuwa ni kungojea mzigo ufike posta kulingana na estimate period iliyowekwa ...
Kumbuka seller atakutumia tracking number hvyo utakuwa una u track mzigo wako kujua maendeleo yake mara nyingi baada ya seller kutuma mzigo huwa inachukua siku 21 au zaidi
Huwa na tumia track24.net hii huwa inanionyesha maendeleo yote ya mzigo wangu mpaka unapo fika posta

* Mm nachukuliaga mizigo yangu posta mpya hapa dar es salaam
Kwahiyo ww utaenda makao makuu ya posta ya mkoa uliopo
Au unaweza kutumia sanduku lako la posta kama unalo ni muhimu kufuatilia mapema mzigo wako posta usingojee mapaka wakutumie msg maana mara nyingi msg zao hazifiki kwa wakati hii inaweza kupelekea mzigo kupotea au kupatataabu kuupata

* kwa mizigo midogo huwa hamna charge zozote ila pale posta mara nyingine huwa wana tukata 1500tsh hata kwa mizigo midogo midogo hii sijajua ni ya nini wajuzi wata dadavua
Vile vile mzogo ukiwa mkubwa zaid ya 0.5kg jamaa TRA wanatakaga 20% ya bei uliyonunulia mzigo hii nazungumzia kwa mizigo midogo dogo
Ila kwenye simu sijawah kukatwa pesa huwa na chukua free

*kumbuka Jina utakaloandika kwenye shipping address liwe ndio hilo hilo lililopo kwenye kitambulisho chako
Maana siku ya kwenda kuchukua mzigo lazima uende na kitambulisho chako cha kura, taifa, au driving license..

Kama una swali karibu
 
Mfano nikijisajiri kwa kutumia sanduku la posta la mkurugenzi wa Manispaa ya kinondoni maana mi sina ya kwangu, halafu post code nikatumia ya Kijitonyama hapa mzigo utapelekwa wapi?
 
Mkuu Masawe mimi nina sanduku la posta wilaya ya kinondoni eneo la kawe nikiagiza mzigo utakuja kwenye address yangu hii ya kawe au ndo kwende huko makao makuu
 
unafanyaje hapo kama hauna sanduku la posta.
 

Shukrani sana mkuu,umenifilisi kile nilichotaka kukijua,ubarikiwe sana
 
Mfano nikijisajiri kwa kutumia sanduku la posta la mkurugenzi wa Manispaa ya kinondoni maana mi sina ya kwangu, halafu post code nikatumia ya Kijitonyama hapa mzigo utapelekwa wapi?
Kwenye sanduku la posta la mkurugenzi
 
Haina noma mkuu,kumbe naogopaga bure tu kuagizia simu kumbe fresh tu
Ni fresh mkuu mimi mwenyewe nilikuwa mwogo ila baada ya kupata somo kutoka kwa wadau huku kina mwl.rct
Sasa hv naagiza vitu vikubwa zaidi huko alibaba na vinafika ninapo kwama naomba msaada kwa wakongwe humu
 
Ni fresh mkuu mimi mwenyewe nilikuwa mwogo ila baada ya kupata somo kutoka kwa wadau huku kina mwl.rct
Sasa hv naagiza vitu vikubwa zaidi huko alibaba na vinafika ninapo kwama naomba msaada kwa wakongwe humu

Poa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…