Mkuu hizo simu zilivyofika posta hukulipia kodi zozote zile??
Mkuu soma hapa utapata picha ya swali lako pia hii itawasaidia na wengine pia
*Kwanza download application ya alixpress kwenye simu yako
* application ikifunguka jisajili kwa kuweka email yako and password zako kumbuka kuhifadhi password vyema ili ikitokea ume unistall hiyo application ukija ku download upya irudi account yako ileile ya awali
*Ingia kwenye application yako ya alixpress kwenye setting tafuta sehem pameandikwa
Shipping adresse hapo ingiza Adress yako
Kwamba unaitwa nani, unakaa wapi, Namba zako za simu zilizopo hewani, post code yako. N.k kisha save
* Tafuta kitu unachotaka kununua ukipata fuata process za kununua hapo hapo kwenye ulipoonea hicho kifaa itakuonyesha pia na shipping cost
Fuata maelekezo hayo ya kununua yatakupeleka mpaka kwenye namna ya kununua hapo utatumia credit card yako ya Visa au Master card au M pesa master card
salio lako litatumwa kwa alixpress baada malipo yako kuwa confirmed
Seller ataanza ku process mzigo wako
Mara nyingi ni 5days then atautuma kwa shipping company
* mzigo wako utatumwa na selller kwa kupitia shipping company uliyo chagua
Kazi yako hapo ww itakuwa ni kungojea mzigo ufike posta kulingana na estimate period iliyowekwa ...
Kumbuka seller atakutumia tracking number hvyo utakuwa una u track mzigo wako kujua maendeleo yake mara nyingi baada ya seller kutuma mzigo huwa inachukua siku 21 au zaidi
Huwa na tumia track24.net hii huwa inanionyesha maendeleo yote ya mzigo wangu mpaka unapo fika posta
* Mm nachukuliaga mizigo yangu posta mpya hapa dar es salaam
Kwahiyo ww utaenda makao makuu ya posta ya mkoa uliopo
Au unaweza kutumia sanduku lako la posta kama unalo ni muhimu kufuatilia mapema mzigo wako posta usingojee mapaka wakutumie msg maana mara nyingi msg zao hazifiki kwa wakati hii inaweza kupelekea mzigo kupotea au kupatataabu kuupata
* kwa mizigo midogo huwa hamna charge zozote ila pale posta mara nyingine huwa wana tukata 1500tsh hata kwa mizigo midogo midogo hii sijajua ni ya nini wajuzi wata dadavua
Vile vile mzogo ukiwa mkubwa zaid ya 0.5kg jamaa TRA wanatakaga 20% ya bei uliyonunulia mzigo hii nazungumzia kwa mizigo midogo dogo
Ila kwenye simu sijawah kukatwa pesa huwa na chukua free
*kumbuka Jina utakaloandika kwenye shipping address liwe ndio hilo hilo lililopo kwenye kitambulisho chako
Maana siku ya kwenda kuchukua mzigo lazima uende na kitambulisho chako cha kura, taifa, au driving license..
Kama una swali karibu