Stephano Aziz Ki aitwa timu ya Taifa ya Burkinafaso, kikosi chao hakuna mchezaji anayecheza ligi ya kwao

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Watanzania ifike wakati tuukubali ukweli, hatuna timu ya Taifa ya kushindana na wenzentu mpaka tufikie viwango kama hivi vya Burkinafaso, yani ukicheza ligi ya ndani sahau kuitwa timu ya Taifa, labda usubiri Chan.

.... Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC Aziz Ki (26) tayari ameanza mazoezi na timu yake ya taifa ya Burkinafaso ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ซ katika jiji la Casablanca Nchini Morocco ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ

September 23/2022 timu hiyo itacheza dhidi ya Dr Congo ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฉ na September 27/2022 watacheza dhidi ya Comoros ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ฒ

Mchezaji wa zamani wa Astonvilla ๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ Bertrand Traore amerejea kwenye timu ya taifa baada ya kutojumuishwa kikosini katika michezo minne (4) iliyopita.

Wachezaji wanne pekee kati ya Wachezaji (25) walioitwa kwenye timu ya taifa ya Burkinafaso ndio wanacheza soka Africa wengine wote wanacheza soka Ulaya !

MAGOLIKIPA.
01. Koffi Herve - Charleroi ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ช
02. Nikiema Kylian - Ado den ๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ฑ
03. Konate Hillet - Valenciennes ๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท

MABEKI
04. Tapsoba Edmond - Leverkusen ๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ‡ช
05. Dayo Issoufou - RS Berkane ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ
06. Yago Steeve - Aris Limassor ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡พ
07. Kabore Issa - Marseille ๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท
08. Guiebre Abdoul - FC Reggiana ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡น
09. Ouedraogo Dylan - Oh Louvain ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ช
10. Fofana - Adama - Dijon ๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท
11. Nagalo Adamo - Nordsjaelland ๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ‡ฐ

VIUNGO
12. Aziz Ki - Young Africans ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
13. Bangre Mamady - Quevilly Rouen ๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท
14. Toure Blati - Pyramids ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ฌ
15. Sangare Gustavo - US Quevilly ๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท
16. Ouedraogo Ismahilia - Volos NPS ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ท
17. Salou Dramane - Noah Yerevan ๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ฒ
18. Bandaogo Abdoul - Trofense ๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡น

WASHAMBULIAJI
19. Badolo Cedric - FC Sheriff ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฉ
20. Bertrand Traore - Basaksehir ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ท
21. Ouatarra Dango - FC Lorient ๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท
22. Bayala Cyrille - AC Ajaccio ๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท
23. Tapsoba Fessal - Standard Liege ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ช
24. Ouatarra Abou - FC Sheriff ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฉ
25. Ouatarra Djibril - RS Berkane ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ

Watanzania ifike wakati tuukubali ukweli, hatuna timu ya Taifa ya kushindana na wenzentu mpaka tufikie viwango kama hivi vya Burkinafaso, yani ukicheza ligi ya ndani sahau kuitwa timu ya Taifa, labda usubiri Chan.
Labda utakuwa umesahau kwamba hata kabla hajatua Yanga, alikuwa hachezi ligi ya kwao pia na alikuwa yupo timu ya taifa. Kwa hiyo hakuna jipya
 
Labda utakuwa umesahau kwamba hata kabla hajatua Yanga, alikuwa hachezi ligi ya kwao pia na alikuwa yupo timu ya taifa. Kwa hiyo hakuna jipya
Simba si walisema ameshuka toka she Yanga hapo ilitarajiwa asiitwe sasa cha ajabu yeye kaitwa huku Okrah ambaye alikuwa akiitwa toka she Simba hajaitwa timu ya Taifa hivi karibuni.
 
Hawa sio wenzetu squad yote inatoka nje na sio nje tu nje ya maana sio kama sisi
 
Simba si walisema ameshuka toka she Yanga hapo ilitarajiwa asiitwe sasa cha ajabu yeye kaitwa huku Okrah ambaye alikuwa akiitwa toka she Simba hajaitwa timu ya Taifa hivi karibuni.
Hivi unafikiri ni rahisi kuitwa timu ya taifa ya Ghana, Nigeria, Senegal na Cameroon hata DRC wakati waliopo Ulaya wengine wanaachwa? Kwa mantiki hiyo, Aziz Ki ni mkali kuliko Mayele? Kwa nini ulinganishe Aziz Ki wa Burkina Faso na Okrah wa Ghana, na sio Aziz Ki wa Burkina Faso na Mayele wa DRC?
 
Nimemuweka Okrah kwa sababu wakati anasajiliwa Simba walikuwa wanatembea na gia kuwa mchezaji wa WC na anaitwa Ghana sasa toka aje Simba hata viiitwe vikosi vitatu hautoweza kumkuta.
 
Nimemuweka Okrah kwa sababu wakati anasajiliwa Simba walikuwa wanatembea na gia kuwa mchezaji wa WC na anaitwa Ghana sasa toka aje Simba hata viiitwe vikosi vitatu hautoweza kumkuta.
Okra alikataa kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Ghana, badala yake akaenda Egypt kwenye kambi ya Simba, hata waandishi wa Ghana walikuwa wanamuandika kwa kumshangaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ