Nimesikiliza wimbo wako mara mbili.
Nikakumbuka sauti yako inafanana na jamaa anaitw Iman, nikaplay wimbo wake wa Farida halafu nikawa naplay wa kwako na wake.
Kisha nikamkumbuka jamaa anaitwa Jimmy Chansa. Nikaplay wimbo wake Am Sorry na We Mchoyo.
Ambacho nimenotice ni kwamba wewe ni kama Jimmy Chansa awe ndani ya mwili wa Iman.
Namaanisha unatumia sauti yako OG kama Jimmy ila unaimba kwa midundo ya kitambo. Hata melody yako imekaa ya enzi za akina Bab Lee na Kizizi.
Beat siyo nzuri kiasi cha kutisha ila ni kama vile mliamua kutengeneza kitu simple ambacho hakitatumia akili nyingi.
Vesi zote mbili unazianza strong ila kati kati unarojeka unaingiza sauti nyingine.
Ushauri wangu mimi;
Wekeza sana kwenye beats, na kwa sauti yako ilivyo naona ukifanya mtindo wa zouk (We Mchoyo wa Jimmy Chansa na Sina wa Baraka) utafiti vizuri.
Pia hebu mcheki jamaa anaitwa Singah na wimbo unaitwa Teyamo hebu wazia kama hiyo beat ingekua yako ungedondokaje.
Beats ziwe catchy hata kama simple, mfano Bill Nass na Whozu kwenye Kwa Leo, au African Beauty ya Diamond.
Pia fanya marketing kubwa haswa fb na Insta. Washkaji zako ndiyo wawe mabalozi wako.
Kingine, nachukulia hii ni ngoma ya kwanza hivyo bado una nafasi....
La mwisho ukiwa unatengeneza wimbo hebu uwe unawazia kua mfano naamua kumshirikisha Chris Brown, hii beat ataendana nayo (I mean beats zako ziwe international).
Kila la kheri.