Stephen Chelu - You're the one (official music audio)

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Wakuu...
Napenda kuwakaribisha kuasikiliza wimbo wangu wa kwanza kabisa kuuachia uitwao 'you are the one' kupitia youtube channel yangu hapa

Maoni yanahitajika pia, wapi nimeboronga, nirekebishe wapi nk nk.

Ila cha ziada tu nakuombeni tuiangalie maradufu hadi iwe no 1 on trending๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Imefanyika moo record na producer gopabeatz
 
Nimesikiliza wimbo wako mara mbili.

Nikakumbuka sauti yako inafanana na jamaa anaitw Iman, nikaplay wimbo wake wa Farida halafu nikawa naplay wa kwako na wake.

Kisha nikamkumbuka jamaa anaitwa Jimmy Chansa. Nikaplay wimbo wake Am Sorry na We Mchoyo.

Ambacho nimenotice ni kwamba wewe ni kama Jimmy Chansa awe ndani ya mwili wa Iman.

Namaanisha unatumia sauti yako OG kama Jimmy ila unaimba kwa midundo ya kitambo. Hata melody yako imekaa ya enzi za akina Bab Lee na Kizizi.

Beat siyo nzuri kiasi cha kutisha ila ni kama vile mliamua kutengeneza kitu simple ambacho hakitatumia akili nyingi.

Vesi zote mbili unazianza strong ila kati kati unarojeka unaingiza sauti nyingine.

Ushauri wangu mimi;

Wekeza sana kwenye beats, na kwa sauti yako ilivyo naona ukifanya mtindo wa zouk (We Mchoyo wa Jimmy Chansa na Sina wa Baraka) utafiti vizuri.
Pia hebu mcheki jamaa anaitwa Singah na wimbo unaitwa Teyamo hebu wazia kama hiyo beat ingekua yako ungedondokaje.

Beats ziwe catchy hata kama simple, mfano Bill Nass na Whozu kwenye Kwa Leo, au African Beauty ya Diamond.

Pia fanya marketing kubwa haswa fb na Insta. Washkaji zako ndiyo wawe mabalozi wako.

Kingine, nachukulia hii ni ngoma ya kwanza hivyo bado una nafasi....

La mwisho ukiwa unatengeneza wimbo hebu uwe unawazia kua mfano naamua kumshirikisha Chris Brown, hii beat ataendana nayo (I mean beats zako ziwe international).

Kila la kheri.
 
Shukran sana mkuu, umeongea kwa urefu na nimekuelewa vyema. Nijitahidi kuyafanyia kazi hatua kwa hatua.
 
Wimbo kusema ukweli sijauskiliza ila ni mbovu kuwahi kushuhudiwa, sijui kwanini usiachane na musiki ukaenda kulima hata mboga za mchicha huko Kigamboni...... Mm huwa napenda good music sijui wako niuweke kundi gani RnB, Pop, Raggae, poor song... Hujui kuimba kalime kijana
 
Tanzania hatuna upungufu wa chakula, hiyo inatoa picha kuwa wakulima waliopo wanatosha kutosheleza mahitaji ya chakula nchini.
 
Nikope buku mkuu niende kuucheki ...

Kwan mpaka yutibu naul sh ngap
 
Ukimuimbia hivi Salama Jabir lazima utamchikia maisha yako yote.
 
Back
Top Bottom