Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Kwanza kabisa umejuaje mimi msomi? Unajua au unadhani unajua?

Msomi ni nani?

Unajua ukiniita mimi msomi naona unanitukana na kuniwekea uzio kwamba mimi sijui kufanya, najua kusoma tu?

Kwa huo mfano wako, umemfananisha Mungu wako awe sawa na mtu anayeshindwa kutengeneza roboti anayejifahamu?

Unaelewa kwa mfano huo unasema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo?
 
This issue will continue to be an endless merry-go-round of the same 'ol same 'ol until it is conclusively settled, once and for all.

It is the world's greatest mystery, as far as I'm concerned.
 
Kiranga yeye anachohitaji kutoka kwenu ni mjibu swali moja tu:Kama dunia imeumbwa na Mungu ambae ni mjuzi wa yote, mwenye huruma yote, muelewa wa yote,kwa nini hakuna perfection humu duniani?
sasa hapo anakosoa uumbaji wa Mungu na si kigezo kwamba Mungu hayupo.

Na hapa duniani si mahala tulipoandaliwa,hapa tunapita tu, makazi yetu yapo mbinguni.
 
Kivipi?

Hapohujathibitisha, umelazimisha bila ufafanuzi.

Mimi ningekuwa uthibitisho Mungu yupo, nisingeumwa.

Mungu huyo asingeumba dunia inayoweza kuwa na mapungufu.

Naumwa,

Hivyo sijaumbwa na Mungu huyo, nimeumbikakwa process yenye mapungufu.
Unataka kumuona Mungu nikuelekeze namna rahisi zaidi ya kumuona?
 
Haya maswali yako yote kumi nilikujibu kiufasaha zaidi ,kwenye ile thread ya makosa kumi aliyoyatenda Mungu.


Na hilo swali la kwanza unalipenda sana ,ila jibu ni hivi ,hapa duniani si mahala tulipoandaliwa ,makazi yetu yapo mbinguni,hapa duniani tunapita tu.
 
Hahaha mzeee excuse accepted. Mkwanja ni muhimu sana. Hongera kwa kufanikisha.

Majibu yako;

1. Kunya ni tendo la kutoa waste product. Sahihi kabisa. Hapo maana yake ni kwamba mwili unafanya tendo la kujisafisha baada ya kuchakata nutrients na kubakisha zile muhimu and needed for the body. Isn't that glorious?! Kuhusu maradhi yatokanayo na kinyesi - hiyo ni kulingana na mazingira. Kinyesi ni product nzuri sana, endapo kitazagaa ovyo huenda kikaleta usumbufu (soma maradhi), lakini umeshafikiria faida yake endapo kitawekwa kwenye matumizi sahihi mfano kuzalishia biogas, mbolea n.k.? Mungu fundi sana boss.

2. Tendo la kufa huleta huzuni na kutenganisha wapendanao. Naam, nalo umenena vyema kabisa. Lakini kwa kuwa tunazungumzia mambo ya kiroho, tendo hilo kwa waaminio linaleta huzuni ya muda ila faraja yake ni ya milele. Na hiyo ni kwa sababu, kufa ni njia ya kwenda kwa Muumba ambako huko kuna makazi na makutano ya kudumu. Kwa kuwa hiyo ni njia ya wote, basi tumaini la kweli ni kwamba wapendanao wote watakutana huko na Mola wao kuishi na kufurahia. Kisayansi, mwili wa kiumbe hai uliokufa una faida nyingi sana kwenye ardhi. Mambo ya natural recycling, Zisome baadhi hapa Why burying loved ones in unmarked graves could save wildlife

Halafu, uamuzi wa Mungu kuumba kifo na ufufuo ni alama tosha ya kuonesha UWEZO NA UKUU alionao Bwana Mkubwa.

Yupo kweli. Sio hadithi tu!
 
kumbe huyu mzee na ujanja wake wote alikuwa anaamini katika BING BANG THEORY!!!.
Kwa mwanasayansi mwenye akili timamu atajua haiwezekani random eruption ilete systematic output na interdependent kama dunia. Watu wameamua kujitoa fahamu sio mchezo.
 
another theory like " the big bang " , Hawking was angry at God for not healing him, for letting his wife be taken, for ruining his family that's why he endlessly argued there is no God. And he knew some gullible earthians will play along. He was an angry crippled Englishman. He knew by confusing you with physics mumbo jumbo you'll end up denying God's existence. That's another theory, since we can't prove there was actually the big bang.
 
illogical a.k.a pumba!!....ni sawa na kuuliza wapi Magufuli alisema kwa sababu yeye ni raisi atakuwa amri jeshi mkuu?
Haujajibu swali...ila pamoja na ukamilifu wote Mungu alionao ila aliumba ulimwengu kwa hekima yake na ndio maama sis wanadamu kwakua hatuna hekima Kama za Mungu tunaona ulimwengu haupo kamilifu
 
Hujaeleweka.

Mjamaa unayemuongelea ni nani?

Aanakimbilia wapi?

Kwa nini?

Mwenzako ni nani?

Chamoto anakipata kivipi?

Unathibitishaje?
kama hujanielewa usinge ni quote
kama ume quote na kunijibu it's seems umeelewa namzungumzia nani
 
Hujazijibu.

Bora ungeshindwa kuzijibu za kikubwa tungeweza kusema zimekushinda kimo.

Lakini kushindwa kujibu hoja za kitoto ni jambo la aibu sana.
na tungekuwa hatunyi/hatufi
Bila Shaka ungekuja na hoja kuwa mbona hatunyi/hatufi
Ndugu yangu
nyie wote non believers hamnaga hoja zaidi ya kusema
ooh mbona hakuna perfection
mara mbona hajitokezi
tatizo lako unataka hoja zako ndizo zionekane
"MUNGU ni mwema na anapenda wampendao,na wote wamtafutao kwa bidii HAKIKA watamwona"
sasa kama wewe hutaki kumatafuta MUNGU unadhani utamwona wapi??!
lakini ndugu shetani amekamata ufahamu wako
Na mbaya ZAIDI unadhani huo ni Utashi na Akili yako.
 
Last word you are either with us,or against us.We do facts you do faith.
 
Kiranga,yours is the old tool of a defensive idealist,What I see here is not a competent opponent,I rather see a humble believer who is somewhat skeptical.Here me when I tell you this,Nature of Reality is subjective but the truth as much as we may all wish can never be subjective it will always be objective.The existence of God can not be refuted by an inability to prove his existence for we the enquirers exist within the same realm of Gods Existence and we are therefore a part of His being.If by affirming our existence and attributing it to some scientific explanation which only fits our current reality we believe we can challenge the proponents of Gods existence then we are surviving on a weak logic as intellectuals.We must acknowledge our limitation in comprehending his existence and from there seek not to prove his existence but to acknowledge his existence.
 
Ndo mana muhubiri alisema kila jambo na wakati wake. Sasa wewe katika umri wa miaka 19 ukaanza kusoma mavitu ya juu kabisa kuzidi uwezo wako wa kufikiri, ona sasa madhara yake yanavyokusumbua na kukutesa nafsi yako huku ukubwani.

Ulikuwa hujakomaa kiroho ndo mana ukawa mwepesi kupigwa zongo na ibirisi uamini anachotaka yeye uamini na kweli ukaamini, Pole sana mzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…