Maoni yangu.Huyo mwanasayansi,si tu alikuwa mwenye akili nyingi,lakini pia alifanya uchunguzi kwa mda mwingi na kutoa hoja zake kwa upeo wa kitaalamu sana kiasi ya kama,hata wale wanaompinga,nadhani wengi hata kuelewa hoja zake wanaishia chini sana kumwelewa kiundani-sisemi ni wote hawamwelewi.na sisemi kuwa huyu mwanasayansi alikuwa sahihi.Lakini,hoja zake nyingi ni za kitaalamu sana,japo maelezo yake yanaonekana mepesi tu kuyaelewa.Hivyo,ili kupingana nazo,zahitaji umwelewe kwanza na uwe na hoja nzuri kumpinga.
Sisemi nitakuwa na hoja nzuri sana au zaidi ya wengine,ila,mtazamo wangu ni huu.
Hizi sheria na kanuni za kisayansi ambazo ndio zatawala na kuathiri vitu hadi tumezoea kuwa uhalisia wote lazima unafuata kanuni fulani n.k.,hizo nazo kuna mahali zinakwama kabisa.Mfano,kanuni zote za kisayansi zinakwama na kupoteza maana inapofikia eneo la black-holes.Hapo kanuni za kisayansi zote hazifanyi kazi; zina-collapse kabisa! Licha ya vingine vyote,mpaka mwanga (light),ambao ndio una spidi kubwa zaidi nao ukipita eneo hilo,humezwa kwenye hiyo black hole na hauwezi kurudi/kuakisiwa toka humo.
Ilimradi walao tuna mazingira ambayo yapo wazi na yanatuonyesha kuwa,hata kanuni zetu tunazozijua,kuziamini na kuzishabikia kuna mahala zinaishia kukwama,hapo ndipo hoja yangu kuwa,walao hizi hazipaswi kutudanganya kuwa ndio kila kitu cha kuamini ama kujengea hoja ya kupinga uwepo wa Mungu.
Najiuliza,iwapo pasingekuwa na black-holes kabisa,ndio tuseme karibia kila kitu akijuacho binadamu,hasa wanasayansi (walao wajuavyo mpaka sasa), wangekuwa na maelezo/majibu na wasingekosa cha kueleza almost kila kitu,kama si vingi zaidi.Black-hole naona imetutia adabu kwetu binadamu na akili zetu za kuhoji kila kitu na kutaka kueleza ama kuwa na jibu la kila kitu.Hapo tumekatwa ngebe na ndio moja ya msaada mzuri wa kujenga hoja dhidi ya kusema kuwa Mungu hayupo.
Pili,binafsi naamini walao kwa ufahamu mdogo kuwa,hata ikiwa big-bang theory ni sahihi,ndio kusema hata kitu kinachoitwa mda (time) nayo ilianzia hapo.Na ndipo uhalisia tuuonao, nao ndipo kila kitu kilipoanzia pamoja na time(mda) kwenye hii reality yetu.Lakini haimaanishi,uhalisia huu tuujuao,ndio kila kitu na ndio huu tu ndio uliopo.Ni kama tupo ndani ya kipande kidogo tu cha uhalisia tukawekewa kanuni zinazojiendesha,lakini sio ndio imekamilika(complete) katika ujumla wa halisia na sio kuwa inawakilisha uhalisia wote mzima aujuao mwenyewe Mwenyezi Mungu.Tumeishi humu,kukulia humu na kwa udogo wa akili zetu ambazo zinahitajika kupambana na haka hauhalisia,hatuwezi (na labda hatukupaswa) kujua uhalisia mwingine zaidi ya huu kwa sasa.Mengine tunaweza kuwa na tetesi tu,kudodosa na hasa kuishia kwenye imani tu zaidi.Kwani,uhalisia huu tu tunauvurunda sana,na hatujaumaliza.
Twajua,kadri ya imani zetu kuwa,Mungu ni roho.Kwa namna yoyote ile,hawezi kuelezewa ama kuendana na huu uhalisia tunaoujua japo twajua yeye anautawala na aweza kuufanyia lolote bila kukinzwa.Sheria za kimwili na vinavyotuzunguka,haziwezi kuwa na ukinzani kwake.Na si sahihi sana kujiaminisha ama kulazimisha kutumia kanuni na sheria za uhalisia huu kama nyenzo ya kuelezea kuhusu Mungu na uwepo wake, kwani,ni vitu dhaifu visivyofaa ama kutosha kuelezea kuhusu Mungu na uwepo wake.Vinatufaa sisi mortal beings na vinavyotuzunguka.
Kwenye maisha haya haya,tuna viumbe/binadamu wenzetu twasikia wanatumia nyungo (kichawi) kupaa angani usiku wakisafiri toka eneo moja hadi jingine na hata mara nyingine kukutwa wameanguka sehemu fulani fulani.Hawa viumbe na nyungo ni vitu vya kawaida kabisa,je,wanasayansi wanaweza kutueleza kisayansi wanapaaje huko angani?Kwa hakika,mambo ambayo yanafanywa na binadamu kwa kutumia nguvu ama za giza au za mwanga,ni mengi.Je,sayansi inaweza kutumia nyenzo na hoja zake kuelezea hayo?!Kama haina majibu,turidhikeje inaposemwa kuwa Mungu hayupo,kwa msingi wa hoja za hali ya juu kisayansi na kwa kutumia kanuni za kiasili tu tunazojua kuelezea mambo mengine ya kawaida?
Mimi binafsi naamini Mungu yupo.Katuweka ndani ya huu ulimwengu na vikanuni vichache tu lakini sio kuwa ndio kila kitu kwake cha kuwezesha sisi kujua ama kuweza kujibu kila kitu.Mbaya zaidi,tuna mengi tu ya kawaida ambayo bado wanasayansi hawajaweza kutoa majibu,hata yaliyo ndani ya miili yetu tu ama mimea tu inayotuzunguka.