Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Flat earth si sayansi, the scientific world reached a consesus many years ago that the earth is not flat, by observation, experimentation, research, miaka mingi tu.

Hawa flat earthers ni wannabe contrarians ambao hawajui hata kuwa contrarian.
 
Kwa habari ya nyoka ndio, ninakubali 100%.
 
Kwa habari ya nyoka ndio, ninakubali 100%.
Watu wengi wanaotupa ovyo ovyo "100%" hata hawaelewi 100% ni nini na ugumu wa kuikamilisha.

Nimekuuliza kama unakubaliana na sayansi, naona umejikausha kujibu swali.
 
Kwa habari ya nyoka ndio, ninakubali 100%.
Unakubali kwa vigezo gani?

Tupe vigezo vinavyoweza kupimika na kutoa majibu yasiokua na utata yatayoendana na uhalisia kama namna namna ambavyo tumeona kua kiuhalisia maji hayawezi kukaa juu ya tufe yasimwagike. Nipe vigezo vyenye kuzingatia kanuni hii uliyoitumia mwanzo
 
Sawa Mkuu, nakuletea muda si mrefu...
 
Maoni yangu.Huyo mwanasayansi,si tu alikuwa mwenye akili nyingi,lakini pia alifanya uchunguzi kwa mda mwingi na kutoa hoja zake kwa upeo wa kitaalamu sana kiasi ya kama,hata wale wanaompinga,nadhani wengi hata kuelewa hoja zake wanaishia chini sana kumwelewa kiundani-sisemi ni wote hawamwelewi.na sisemi kuwa huyu mwanasayansi alikuwa sahihi.Lakini,hoja zake nyingi ni za kitaalamu sana,japo maelezo yake yanaonekana mepesi tu kuyaelewa.Hivyo,ili kupingana nazo,zahitaji umwelewe kwanza na uwe na hoja nzuri kumpinga.

Sisemi nitakuwa na hoja nzuri sana au zaidi ya wengine,ila,mtazamo wangu ni huu.

Hizi sheria na kanuni za kisayansi ambazo ndio zatawala na kuathiri vitu hadi tumezoea kuwa uhalisia wote lazima unafuata kanuni fulani n.k.,hizo nazo kuna mahali zinakwama kabisa.Mfano,kanuni zote za kisayansi zinakwama na kupoteza maana inapofikia eneo la black-holes.Hapo kanuni za kisayansi zote hazifanyi kazi; zina-collapse kabisa! Licha ya vingine vyote,mpaka mwanga (light),ambao ndio una spidi kubwa zaidi nao ukipita eneo hilo,humezwa kwenye hiyo black hole na hauwezi kurudi/kuakisiwa toka humo.

Ilimradi walao tuna mazingira ambayo yapo wazi na yanatuonyesha kuwa,hata kanuni zetu tunazozijua,kuziamini na kuzishabikia kuna mahala zinaishia kukwama,hapo ndipo hoja yangu kuwa,walao hizi hazipaswi kutudanganya kuwa ndio kila kitu cha kuamini ama kujengea hoja ya kupinga uwepo wa Mungu.

Najiuliza,iwapo pasingekuwa na black-holes kabisa,ndio tuseme karibia kila kitu akijuacho binadamu,hasa wanasayansi (walao wajuavyo mpaka sasa), wangekuwa na maelezo/majibu na wasingekosa cha kueleza almost kila kitu,kama si vingi zaidi.Black-hole naona imetutia adabu kwetu binadamu na akili zetu za kuhoji kila kitu na kutaka kueleza ama kuwa na jibu la kila kitu.Hapo tumekatwa ngebe na ndio moja ya msaada mzuri wa kujenga hoja dhidi ya kusema kuwa Mungu hayupo.

Pili,binafsi naamini walao kwa ufahamu mdogo kuwa,hata ikiwa big-bang theory ni sahihi,ndio kusema hata kitu kinachoitwa mda (time) nayo ilianzia hapo.Na ndipo uhalisia tuuonao, nao ndipo kila kitu kilipoanzia pamoja na time(mda) kwenye hii reality yetu.Lakini haimaanishi,uhalisia huu tuujuao,ndio kila kitu na ndio huu tu ndio uliopo.Ni kama tupo ndani ya kipande kidogo tu cha uhalisia tukawekewa kanuni zinazojiendesha,lakini sio ndio imekamilika(complete) katika ujumla wa halisia na sio kuwa inawakilisha uhalisia wote mzima aujuao mwenyewe Mwenyezi Mungu.Tumeishi humu,kukulia humu na kwa udogo wa akili zetu ambazo zinahitajika kupambana na haka hauhalisia,hatuwezi (na labda hatukupaswa) kujua uhalisia mwingine zaidi ya huu kwa sasa.Mengine tunaweza kuwa na tetesi tu,kudodosa na hasa kuishia kwenye imani tu zaidi.Kwani,uhalisia huu tu tunauvurunda sana,na hatujaumaliza.

Twajua,kadri ya imani zetu kuwa,Mungu ni roho.Kwa namna yoyote ile,hawezi kuelezewa ama kuendana na huu uhalisia tunaoujua japo twajua yeye anautawala na aweza kuufanyia lolote bila kukinzwa.Sheria za kimwili na vinavyotuzunguka,haziwezi kuwa na ukinzani kwake.Na si sahihi sana kujiaminisha ama kulazimisha kutumia kanuni na sheria za uhalisia huu kama nyenzo ya kuelezea kuhusu Mungu na uwepo wake, kwani,ni vitu dhaifu visivyofaa ama kutosha kuelezea kuhusu Mungu na uwepo wake.Vinatufaa sisi mortal beings na vinavyotuzunguka.

Kwenye maisha haya haya,tuna viumbe/binadamu wenzetu twasikia wanatumia nyungo (kichawi) kupaa angani usiku wakisafiri toka eneo moja hadi jingine na hata mara nyingine kukutwa wameanguka sehemu fulani fulani.Hawa viumbe na nyungo ni vitu vya kawaida kabisa,je,wanasayansi wanaweza kutueleza kisayansi wanapaaje huko angani?Kwa hakika,mambo ambayo yanafanywa na binadamu kwa kutumia nguvu ama za giza au za mwanga,ni mengi.Je,sayansi inaweza kutumia nyenzo na hoja zake kuelezea hayo?!Kama haina majibu,turidhikeje inaposemwa kuwa Mungu hayupo,kwa msingi wa hoja za hali ya juu kisayansi na kwa kutumia kanuni za kiasili tu tunazojua kuelezea mambo mengine ya kawaida?

Mimi binafsi naamini Mungu yupo.Katuweka ndani ya huu ulimwengu na vikanuni vichache tu lakini sio kuwa ndio kila kitu kwake cha kuwezesha sisi kujua ama kuweza kujibu kila kitu.Mbaya zaidi,tuna mengi tu ya kawaida ambayo bado wanasayansi hawajaweza kutoa majibu,hata yaliyo ndani ya miili yetu tu ama mimea tu inayotuzunguka.
 

Mkuu, iko hivi, habari ya nyoka kuzungumza na binadamu inapatikana katika Biblia kitabu Cha Mwanzo mlango wa 3.

Mara nyingine mnyama kuongea na mwanadamu ni katika Hesabu 22:21-35 pale Nabii Balamu alipokemewa na punda wake.

Kuhusu habari ya Punda nina uhakika Malaika alizungumza kupitia Punda, Ila kuhusu Nyoka ninaamini Nyoka alikuwa na uwezo wa kuongea kama Binadamu ama Shetani alizungumza kupitia nyoka.

Biblia inasema nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu.

Kwa sasa tuna Ndege kama Kasuku ambao wanaweza zungumza kama Binadamu.

Biblia ya Kiingereza inamtaja nyoka yule kama 'Serpent' ikiwa na maana in nyoka mkubwa.

Tunaona baada ya Adam na Hawa kuharibu, Mungu alifanya mazungumzo nao na nyoka akiwepo.

Nyoka alilaaniwa kwa kuambiwa atakuwa akitumia tumbo ili kufanya mwendo (hapa yaonekana nyoka alikuwa akitembea na alikuwa na mikono) na atakula mavumbi (kuonesha alikuwa anakula chakula kingine pengine bora zaidi) na uadui ukawekwa kati ya uzao wa nyoka na mwanamke (Japo hili lina maana ya Kitendo kilichotokea pale Kalvari miaka 2000 iliyopita) lakini kwa mazingira ya kawaida mwanadamu na nyoka hawapatani kabisa.

Baada ya kusema hayo, nihitimishe kwa kusema Nyoka alikuwa hazungumzi Bali shetani alizingumza na Hawa kupitia Nyoka, sababu Mara ya Pili Mungu hakumhoji nyoka kwamba kwanini amefanya vile, Bali aliishia kumlaani (kuonesha ule uwezo wa kuzungumza ameshaondoka nao mwenyewe 'Shetani').
 
Mkuu, iko hivi, habari ya nyoka kuzungumza na binadamu inapatikana katika Biblia kitabu Cha Mwanzo mlango wa 3.
Hata habari za dunia kua tufe zinapatikana katika sayansi lakini ulitumia fact zilizo nje na sayansi kuonesha kua haiwezekani maji kukaa juu ya tufe na ndio maana sikutaka tuzame kwenye sayansi. Sasa ni vizuri tutumie kanuni ileile ya uhalisia kufananisha mambo ili tuubaini ukweli

Mara nyingine mnyama kuongea na mwanadamu ni katika Hesabu 22:21-35 pale Nabii Balamu alipokemewa na punda wake.
na mimi nikikuambia mara nyingine tufe hutuamisha maji ukiyaweka vizuri utasemeje???

Kuhusu habari ya Punda nina uhakika Malaika alizungumza kupitia Punda, Ila kuhusu Nyoka ninaamini Nyoka alikuwa na uwezo wa kuongea kama Binadamu ama Shetani alizungumza kupitia nyoka.
ishu hapa ni je inawezekana kiuhalisia punda na nyoka wakafanya convo na binadamu? Niliuelewa mfano wako vizuri kua kiuhalisia haiwezekani maji yakawa juu ya tufe pasipo kumwagika unatumia kichaka cha miujiza kujificha???

Biblia inasema nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu.
Sayansi pia imesema dunia ni tufe ulitumia vigezo gani kupinga???

Kwa sasa tuna Ndege kama Kasuku ambao wanaweza zungumza kama Binadamu.
hilo halina mjadala, je tunao nyoka na punda wenye kuzungumza kama binadamu??? (likiwezekana hili basi kwa principle hiyo hiyo tunaweza tukawa na tufe yenye kuhifadhi maji juu bila kumwagika)

Biblia ya Kiingereza inamtaja nyoka yule kama 'Serpent' ikiwa na maana in nyoka mkubwa.
The same damn thing, sayansi imeitaja dunia kama tufe pamoja na hayo mbona ulipinga??

Tunaona baada ya Adam na Hawa kuharibu, Mungu alifanya mazungumzo nao na nyoka akiwepo.
bob kuwa serious basi, umesoma science informations zenye kuzungumzia dunia ni mfano wa tufe mbona umezipinga ulitumia criteria gani kuzipinga?? Sasa unaniletea biblical informations wewe ulitumia fact gani kuzikubali taarifa hizi mpaka uziamini kiasi cha kutolea ushahidi ambao haupo kiuhalisia???


Nilitegemea kukuta extra informations zenye kulenga uhalisia katika mazingira yetu kama ulivyofanya mwanzo lakini nashangaa huja apply kanuni hiyo hapa

Kwaiyo yule jogoo ambaye alimbeba pazi kichwa chini miguu juu yupo kiuhalisia kwasababu kitabu kimesema hivyo?[/QUOTE]
 
[/QUOTE]Daaaah!! Haya majibu hata mimi yamenifikirisha sana. Kudos mkuu kwa kuweza kupangua hoja kiustadi namna hii..
 
[/QUOTE]

Mkuu, hapa tunazungumza kuhusu DINI-IMANI vs SAYANSI.

Ili kufikia hitimisho kwa jambo lolote la Kidini mfano katika Biblia Imani inatumika kuliko hoja.


Ili kufikia hitimisho kwa jambo lolote la Kisayansi, majaribio na hoja zinatumika kuliko imani ndipo tunafikia hitimisho.

So nikutake uelewe hilo kuanzia sasa.

Maelezo niliyokupa kwa mtu mwelewa, yanajitosheleza kabisa.

Kwa mfano, Tofaa (Apple) kudondoka toka kwenye mti hadi chini inaleta Mantiki kwamba kuna kani inaitwa Gravity? Hayo maelezo yanajitosha?

Kwangu Mimi hayajitoshi, na ndio maana naandika kitabu kuonesha namna Sayansi imetufanya wajinga kwa muda mrefu.

Tukio lililotokea pale Eden, haliwezi kuwa na shaka, kwa mfano nikikuuliza kwanini Mashariki ya kati ndiko mafuta mengi yanapatikana, Jibu unalo? Kwanini?
 
Mimi niliisha waambia hawa watu wa aina ya Kiranga kuwa"KISICHOKUWEPO HAKINA JINA,HAKIHISIKI,HAKITAMKWI,NA WALA HAKIJADILIKI.

Kiranga na wote wanaomfuata, uthibitisha uwepo wa MUNGU wao wenyewe kwa kumjadili tu MUNGU.
 
RAFIK IYO NATURE ORIGINI YAKE NI NINI???
 
Daah mkuu mi naamini uwepo wa Mungu

Ila hapa kwenye flat earth unatuangusha kiongoz sio kidogo

Hafu unafanya sisi tunaomwamini Mungu tuonekane maboya

Unajua watu hawataki kubshana na wewe kuhusu flat earth

Maana ni too childish , hata mm nmeona aibu

Sory mkuu , tuko pmj katka uwepo wa mungu

Cc 😡kiranga
 
dah

Mshikaji kaonyesha ana uwezo mdogo sana

Nimeona hadi aibu
 
Ulishakalishwa na Zuri kitambo Sana.Lakini maskini hata ujielewi.
 
Ulishakalishwa na Zuri kitambo Sana.Lakini maskini hata ujielewi.
Hayo ni mawazo yako. Una haki ya kikatiba kuwa na mawazo yako, na mimi natetea haki yako ya kikatiba kuwa na mawazo yako na kujieleza.

Lakini wewe na huyo Zurri wako wote hamjaweza kuthibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo.

Kwa sababu hayupo. Ndiyo maana maelezo ya kuwepo kwake yana contradiction.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo na ondoa contradictions nilizoonesha zipo katika dhana ya kuwepo Mungu huyu.

Ukishindwa haya mawili, nakuona mpiga soga tu usiyejua mbele wala nyuma.

Thibitisha, usipihe soga tu bila uthibitisho.
 
Hana uwezo wa kujibu maswali haya na mfano wa haya,na kuna wakati huwa namuuliza naswaki si kwa lengo anijibu bali huwa naonyesha watu uko wapi ujinga wake na kumuonyesha yeye pia ujinga wake uko wapi. Kwa ufupi huwa namsaidia.
Yaani mkuu umesema kweli .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…