Sasa mkuu, endapo tumepewa uwezowa kufikiri,kuchambua mambo na kufanya maamuzi, hautaki tutumie uwezo huo kupambanua mambo?
Unataka nikiambiwa niwahi posta nikapande treni ya kwenda Zanzibar nikimbie tu bila kujiuliza, Zanzibar na treni wapi na wapi?
Reli imejengwa lini, Je inawezekana ikajengwa usiku mmoja bila watu kuwa na taarifa? Hiyo treni imenunuliwa lini?
Huenda ukatusaidia na jambo jipya leo, ni mambo gani yanahitaji logic na yapi hayahitaji logic mkuu?
Kwanza kwangu mimi sihitaji kujifunza logic eti ili niweze kujenga hoja,kuhoji na kufikia hitimisho juu ya suala fulani.
Kaa ukijua wanafalsafa wa magharibi ya kale wayunani ndio walioleta elimu ya mantiki,ma yalikuwepo maneno kabla ya elimu ya mantiki.
Sasa wewe jiulize kabla kina Aristoto watu walikuwa wanahoji vipi na kuupata ukweli vipi ? Maana yeye ndio wa mwanzo katika logic.
Hapa nakuacha na suali,je unayajua madhaifu ya logic ?
Kujiuliza kupo na ni hulka yetu binadamu,kwahiyo haina uhusiano na logic.