Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Unajua kwamba ukitumia aphabet kuandika tayari ushatumia logic hiyo hiyo unayoiponda?

Nilikuuliza swali rahisi sana na hapa nataka ujibu kwa kukiri.

"Je kati ya maneno na logic kipi kilianza ?"
 
Huyo jamaa kwani ndo nani mbona mnatuletea reference za ajabu anyway Mkuu Kiranga unatakaga nini kwani na mambo/hoja yako ya kuwa Mungu hayupo.....????kama unajiona wewe na wenzio wachache ndo waerevu sana kujua Mungu hayupo hongereni kwa miakili yenu mingi iliyotukuka.
Wewe endelea kuvimba tu hapo nyuma ya batton hzoo kuwa Mungu hayupo walikuwepo wenzio wengi tu kama ww... Yahn ww sio wa kwanza na wala hautakuwa wa mwisho.
Nakushauri ingia Google tafuta watu waliomzihaki Mungu na mambo ya ovyo yaliyotukuka na utaona cha mtemakuni kilichowakuta......nakuanzia na huyu wa kwnza eng mkuu wa meli ya Titanic alisema kwa ubora wa meli hii hata Mungu hana uwezo wa kuizamisha kulichotokea unakijua.

Kweli kadri unavyozidi kusoma ndo unavyozidi kuwa mpumbavu.

Acha kumezeshwa matango pori ndugu yangu.

Hivi mtu akipata janga ama kufa kifo kibaya ndiyo kunamaanisha Mungu yupo?

Kama hoja ni hiyo mbona hata hao walioitwa wafuasi wa Yesu/Mungu walikufa vifo vibaya kuzidi hata hao unaowasema kwamba walidhihaki!?

Soma hapa chini,

JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA

1. #Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali dhidi ya kanisa la Kristo. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

2. #Marko
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.

3. #Luka
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

4. #Yohana
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa.

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. #Petro
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisulubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya "X". Petro mwenyewe aliomba asulubiwa kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18).

6.#Yakobo
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe. Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. #Yakobo (mwana wa Zebedayo)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa Yakobo alichinjwa huko Jerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

8. #Batholomayo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo.

9. #Andrea
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la "X" miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri saa kama hii"

10. #Tomaso
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko.

11. #Yuda (Thadei)
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

12. #Yuda (Iskariote)
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha.

NOTE:
13. #Thadayo (au Mathia) ni Mwanafunzi aliyeteuliwa na Yesu kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (msaliti). Huyu alipigwa na mawe hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

14. #Paulo
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka (A.D).

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.
 
Nilikuuliza swali rahisi sana na hapa nataka ujibu kwa kukiri.

"Je kati ya maneno na logic kipi kilianza ?"
Kilianza lini na wapi!?

Tatizo lako ambalo hutaki kujua ni kwamba Kiranga alishakupuuza ndiyo maana hahangaiki kupoteza muda ku reply comments zako zisizo na mantiki.

Jitahidi kuwa unauliza maswali yenye mantiki jamaa yangu.
 
Kitabu kinachohitaji tafsiri hakiwezi kuwa kitabu cha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Ukiona kitabu kinahitaji tafsiri ujue hicho si cha Mungu huyo.

Unaelewa hilo?

Kiranga hakuna kitabu kibovu kuwahi kutokea kama qurani

Tatizo waislam wengi hawajui kiarabu wanakariri quran bila ya kujua maana

Ndiio maana utakuja kukuta uzuri wa qurani ni kiarabu ukibadilisha kukaaa peke yake kwa lugha nyingine hutatamani kukisoma kwakuwa hayo ni mashairi

Mwandishi wa quran amekopi hadithi kutoka ktk bible na akatengeneza mashairi na kupitia maisha anayoona na kutengeneza quran
 
Kwa nini nianzishe mada mpya kuhusu Quran wakati wewe ndiye umeleta habari za Quran kwenye mada hii?
Naificha Hekima yangu katika Upumbavu wangu!.
Ulivyotaka Mungu ajitetee ulitaka nikuletee reference ya Aristottle ???. Nimethibitisha ulichokitaka na kuponda taka na matango pori yote ya Stephen Hawking ambaye ndiye kitovu cha mada tajwa na nikakupa Faida zaidi kwa kuota mfano wa Fireworks a.k.a Fataki.

Naendelea kuficha hekima yangu ndani ya upumbavu wangu. Tusije wote tukaonekana hamnazo.

END OF QUOTE.
 
Kwanza kwangu mimi sihitaji kujifunza logic eti ili niweze kujenga hoja,kuhoji na kufikia hitimisho juu ya suala fulani.

Kaa ukijua wanafalsafa wa magharibi ya kale wayunani ndio walioleta elimu ya mantiki,ma yalikuwepo maneno kabla ya elimu ya mantiki.

Sasa wewe jiulize kabla kina Aristoto watu walikuwa wanahoji vipi na kuupata ukweli vipi ? Maana yeye ndio wa mwanzo katika logic.

Hapa nakuacha na suali,je unayajua madhaifu ya logic ?

Kujiuliza kupo na ni hulka yetu binadamu,kwahiyo haina uhusiano na logic.

Bora umetambua umuhimu wa kujiuliza. Na mimi shida yangu sio jina gani linatumika, la hasha, ni hapo kwenye kujiuliza, ndio maana kwenye post yangu nimesema huo uwezo au kujiuliza na kutafakari mambo tunao, sioni ubaya kuutumia au kuufanyia kazi kwenye maisha ya kila siku.

Hapo sasa ndio wana scholar wakaenda mbali kwa kuja na mfumo wa logic, ambao wewe ndio umeutaja ulipo ninukuu.

Nitoe mfano, nikiandika au kusema kwamba wewe zuri sio binadamu, ni nyangumi, utafanyaje?
 
It is really shocking following the train of your reason! First and far most, you syllogism does not make sense at! The existence of God does not depend on the existence of death. To go further, your premises are totally unsound. It is not true that death is a cruel extinguish of life and people do cry for very many reasons. It is natural for people to cry. Just you as a rational being do not you thing that death is necessary on this earth. Can you imagine living in the world where there is no death. This is why Leibniz call this the best world of possible worlds.
what do you mean when you say God=greatest love? your mean God is the greatest Love!! If this is what you mean then you are incorrect, Love is merely an attribute of this super natural being. The fact of the matter is, having love for someone does not mean wishing a person to be free from pain. There is what is called tough love. For this matter, if there is death then that does not mean God does not exist. You lack premise to support it.
 
Mr kiranga what I can say about the existence of not of the so called called , depends on our intellectual level.
I don't believe that we have enough brains to explain the universe and our existence. For example we can't explain how it was decided that we should have two sex entities
And by which authority. The two sexes again decided to have a N-S type of a magnetic attraction between.
Mr Hawkins and other scientists can not prove such a perpetuality.
I believe our brains needs an external injection of intelligence if we are to find answers to universal questions.
 
Bora umetambua umuhimu wa kujiuliza. Na mimi shida yangu sio jina gani linatumika, la hasha, ni hapo kwenye kujiuliza, ndio maana kwenye post yangu nimesema huo uwezo au kujiuliza na kutafakari mambo tunao, sioni ubaya kuutumia au kuufanyia kazi kwenye maisha ya kila siku.

Hapo sasa ndio wana scholar wakaenda mbali kwa kuja na mfumo wa logic, ambao wewe ndio umeutaja ulipo ninukuu.

Nitoe mfano, nikiandika au kusema kwamba wewe zuri sio binadamu, ni nyangumi, utafanyaje?

Maneno yako yana busara sana nakufananisha na jirani mwema
 
Kiranga hakuna kitabu kibovu kuwahi kutokea kama qurani

Tatizo waislam wengi hawajui kiarabu wanakariri quran bila ya kujua maana

Ndiio maana utakuja kukuta uzuri wa qurani ni kiarabu ukibadilisha kukaaa peke yake kwa lugha nyingine hutatamani kukisoma kwakuwa hayo ni mashairi

Mwandishi wa quran amekopi hadithi kutoka ktk bible na akatengeneza mashairi na kupitia maisha anayoona na kutengeneza quran
Nimependa sana Jina lako, Astronomer The great na nikaona nikupe Faida kidogo kabla ya kusepa.
INGIA YOUTUBE KISHA ANDIKA "Professor Moshe Sharon". TAFUTA MUDA UMSIKILIZE KATIKA LECTURE ZAKE. UTAFAIDIKA SANA.
 
Upepo hatujawahi kuuona ila tunasema upo kwa kuwa tunaona tu matendo yake kama kupuliza kupeperusha n.k
Vipi wewe unayesema MUNGU hayupo kwa kuwa tu eti hajawahi kuonekana ijapokuwa tunayaona matendo yake
Aliyesema nani kwamba Mungu hayupo kwa sababu haonekani!?

Mbona vipo vingi tu visivyoonekana ila tunajua vipo?

Acha kubwabwaja.

Mungu hayupo,kama yupo thibitisha!
 
Nimependa sana Jina lako, Astronomer The great na nikaona nikupe Faida kidogo kabla ya kusepa.
INGIA YOUTUBE KISHA ANDIKA "Professor Moshe Sharon". TAFUTA MUDA UMSIKILIZE KATIKA LECTURE ZAKE. UTAFAIDIKA SANA.

Asante "UTULUBUL ILMU WALAU BI SWIIN"

Lakini kabla ya kujua njia ya kuenda mahala fulani unatakiwa ujue unaenda wapi

Mfano mm hata kama siijui njia ya mbgala ipo wapi lakini natakiwa nijue naenda mbagala

Je kabla sijaenda kuchukua hiyo elimu kwa huyo profesa je kwanini umenidirect kwa huyo profesa?
 
Even if Hawking is completely discredited,the problemof evil totally contradicts the existence of the omnipotent, omniscient and Omni benevolent Godhead.

One does not need Hawking and sophisticated theories.

One needs to asks a question of simple logic.

A normal father who loves his children does not want to see them suffer in any way.

This is a normal father.

The protection goes up as the love and ability to protect increases.

God is supposed to be the omnipotent, omniscient and Omni benevolent, he can do all, knows all and has the greatest love.

Why did he create a universe in which suffering is possible, while he could have created a universe in which suffering is not possible?
Well that might sound superficial problem but philosophically there is no such a thing as evil. what is evil? Evil is merely a deprivation of good. absence of something does not mean non existence of something else. On this i reckon with Saint Augustine and Thomas Aquinas.
Even if just for sake of argument that evil was existing on this world on which I argue the contrary, the Philosopher Alvin Plantiga says that Existence of evil does not pose a serious problem on the existence of supreme
natural being, what this supreme being has reason of letting evil in this world which we cannot.
 
Mimi kama mmoja wa wanaoamini uwepo wa Mungu naomba niongezee kidogo mambo ya kutafakari ili tujue ni kitu gani kipo mbele yetu na huenda ikaboresha mjadala tukaongeza ufahamu.

Kiranga hana shida na mtu kuamini kwamba Mungu yupo, hilo anakubaliana nalo na hana tatizo kabisa. Shida yake ipo kwenye DHANA nzima ya UWEPO wa Mungu, namaanisha dhana inasema huyu Mungu ni mjuzi wa yote, ana upendo wote, ana uwezo wote. Lakini maandiko hayo hayo yanayompa hizo sifa zote, ndani yake kuna mkanganyinko unaotokana na maelezo kwa matukio mengi kupingana na sifa za huyo Mungu.

- Mungu anaejua yote kamtengeneza Adam kisha baadae anakumbuka, oh, kumbe alitakiwa awe na msaidizi, akamtengeneza HAwa.

- Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote anaamua kuwaondoa waisrael Misri, njiani anaghafilika anataka kuwaangamiza ambakishe Musa peke yake, ni kama anaona haukua uamuzi wa busara au alikosea kuamua kuwapeleka nchi ya Israel.

- Anamuumba binadamu na kumpa maagizo ya namna ya kuishi, anakosea, anamleya Yesu ambae ni Mungu na Hapo hapo ni binadamu, anakuja kufa ili awakomboe wanadamu. Hawa wanadamu wanatakiwa waishinde dhambi na kuishi kama Yesu alivyokuwa duniani wakati wao hawana uungu na ubinadamu kwa wakati mmoja.

- Anaamua kiwango au kiasi cha ufahamu wa kumjua yeye usiwe sawa, utofautiane kwa kila mmoja.

Hayo ni kwa uchache tu, na ndio maana sasa ukijaribu kutafakari ni kama kuna vitu havioani au inabidi uhitaji kiasi flani au kiwango cha tofauti kuweza kuelewa haya mambo, sasa ilitegemewa mambo yaliyopangiliwa na kutengenezwa na Mungu, yawe katika usahihi ikiwa ni mfano wa ufasaha wa mambo.

Na hapo ndipo Kiranga anasema dhana au hoja nzima ya uwepo wa Mungu, imejengwa kwenye msingi dhaifu.

NB. Naamini katika uwepo wa Mungu.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, angekuwepo, asingeumba kiulimwengu cha hapa duniani kina mabaya, na kingine hukopeponi hakina mabaya.

Hilo hamlioni?
Looks like ur using both emperical scence and speculations. Kwa kifupi tu ni kwamba, Mungu humwekei standards wewe kwa maana ya kuwa si lazima kila unachokiona kibaya kwako na kwake ni kibaya, na si lazima upendo alionao ufananane na upendo walio nao binadamu.Kwani nani kasema kuwa sisi ndiyo tunatakiwa ku-set standards halafu Mungu ndiyo a-follow-suit kwenye standards hizo? Mistake kubwa ndiyo hiyo kwamba standards huwa tuna-approve sisi na kuanza kuzitumia katika kumu-judge Mungu namna alivyo. Mungu si mjinga angekuwa anatumia standards zetu angekuwa ameshaondoa kabisa kifo kisingekuwepo tena!

Just a hint, spritual science is not emperical science and emperical science has not at any time t, claimed to be the basis of source of every kind of knowledge and hence it cannot expalin all phenomena. Reality transcends empirical knowledge.

Another hint: wakati Albert Einstein akiwa anafanya kazi za utafiti kwa kutumia Laws of classical Physics ambazo zilikuwa developed huko nyuma na wana Fizikia wakali kama akina Isaac Newton na wengine, alikuja kubaini kuwa kuna baadhi ya phenomenal cases hizi laws zina-fail ku-explain, na ndiyo akaja aka-developed special Theory of Relativity iliyo base kwenye Quantum Mechanics, ambazo sasa ziliweza ku-reconcile ile failure ya zile za Classical Mechanics. This proves outright that Emperical Science is still developing and hence it cannot explain everything. Huwezi ukawa uko sahihi kwa kuchanganya maelezo yanayohusu discipline moja ya sayansi na maelezo yake kwenye discipline nyingine tofauti ya Sayansi, hili ndiyo kosa kubwa linalofanyika kwenye mijadala hii. Kwa mfano, hamuwezi mka-reconcile discreapancies kwenye imani mbili let's say Uislam na Ukristo kwa kutumia vyote Quran na Biblia. Kwamba mwislamu atumie Quran na mristo atumie Biblia, haiwezekani, kwa sababu mkifanya hivyo mtakuwa mmekosa standards. Aidha inabidi mu-develop standards nyingine za kutumia au mchague kutumia kitabu kimojawapo kati ya hivyo viwili na si vyote. Hivi vitu viko straightforward na huwa ninashangaa sana ninapoendelea kuona mijadala ya namna hii inazidi kuibuka kila kukicha

Mfano mwingine ni kwamba hayupo mtu hapa dunianai ambaye alishawahi kusema kwamba YESU HAJAWAHI KUWEPO, hayupo na ndiyo maana hata the popular world calendar inatumia BC na AD.However, on the same issue,Spritual Science ina-prove,kwa kutumia tools zake ambazo si sawa na zile za emperical, kuwa alifufuka na kupaa mbinguni(kitu ambacho kupaa hewani against gravity ni impossible badsed on emperical laws of nature)
Sasa mimi nakaa najiuliza maswali nashindwa kuelewa. Huu usomi wa kuwa tunasoma hadi tunafikia kushindwa kuelewa sayansi ipi ni ipi tunauokota wapi? Uwe kwenye emperical sayansi halafu uchukue tools za huko na kuzipeleka kwenye spritual science zikatumike huko, nani kasema kwamba emperical sayansi pekee ndiyo inayoweza ku-explain all phenomena?

Je, wakati tunasoma kwenye Research Methodology kwa mfano, tulifundishwa hivyo? Kwamba utatumia Newton's Laws of Motion kujua IDADI ya wakimbizi wa Rohingya Muslims waliotembea kutoka Mynamar Kwenda Bandladesh kisa walikuwa wanatembea (motion)? Kwamba utatumia IDADI ya watu waliokufa kutokana na radiations za URANIUM kujua RADIO-ACTIVE DECAY au Half life ya Uranium, kwamba idadi ya watu walioathirika itakusaidia kujua ni radiatons kiasi gani zimekuwa emitted na Uranium? Hii mifano miwili naifananisha na mtu anaye-apply tools za emperical science ku-prove mambo kwenye spritual science

Emperical sayansi haina tools amnazo zinaweza kuthibitisha uwepo wa Mungu, na hata wanasayansi wanaosema kuwa MUNGU yupo hawajatumia emperica tools kusema hivyo, na kwa hiyo wanaodai kuwa Mungu hayupo NAO PIA hawawezi kutumia emerical tools kudai hivyo, as simple as that.

Hii issue ya kuwepo au kutokuwepo Mungu is not as complicated and confusing as it appears to be, but rather the complications and confusions arise from the lack of perfect knowledge, when we try to accommodate both the divine knowledge and emperical knoledge STANDARDS, to the LACK OF STANDARDS in our contemporary morality. Kna kitu sisi wabishani hatuna, na hicho ndicho kinatufanya tubishane. Tatizo hapa ni LACK OF STANDARDS, na si Mungu kuwepo au kutokuwepo!
 
Bora umetambua umuhimu wa kujiuliza. Na mimi shida yangu sio jina gani linatumika, la hasha, ni hapo kwenye kujiuliza, ndio maana kwenye post yangu nimesema huo uwezo au kujiuliza na kutafakari mambo tunao, sioni ubaya kuutumia au kuufanyia kazi kwenye maisha ya kila siku.

Hapo sasa ndio wana scholar wakaenda mbali kwa kuja na mfumo wa logic, ambao wewe ndio umeutaja ulipo ninukuu.

Nitoe mfano, nikiandika au kusema kwamba wewe zuri sio binadamu, ni nyangumi, utafanyaje?

Elimu ya mantiki ina udhaifu katika kuhoji na kufikia hitimisho,nikisema logic siikubali na haina uwezo wa kutufikisha kwenye ukweli wa kuhoji namaanisha haifai kuitumia.
 
Mr kiranga what I can say about the existence of not of the so called called , depends on our intellectual level.
I don't believe that we have enough brains to explain the universe and our existence. For example we can't explain how it was decided that we should have two sex entities
And by which authority. The two sexes again decided to have a N-S type of a magnetic attraction between.
Mr Hawkins and other scientists can not prove such a perpetuality.
I believe our brains needs an external injection of intelligence if we are to find answers to universal questions.

Precisely, it resonates with what Nyani Ngabu mentioned previously, the whole thing remains mystery!
in your view, should we disengage searching answers related to universal questions?
 
Elimu ya mantiki ina udhaifu katika kuhoji na kufikia hitimisho,nikisema logic siikubali na haina uwezo wa kutufikisha kwenye ukweli wa kuhoji namaanisha haifai kuitumia.

Ahsante mkuu, tufanye sijasema utumie logic, nimetoa mfano tu kwamba nikisema wewe zuri sio binadamu ni mnyama aina ya Nyangumi, utafanyaje?
 
Looks like ur using both emperical scence and speculations. Kwa kifupi tu ni kwamba, Mungu humwekei standards wewe kwa maana ya kuwa si lazima kila unachokiona kibaya kwako na kwake ni kibaya, na si lazima upendo alionao ufananane na upendo walio nao binadamu.Kwani nani kasema kuwa sisi ndiyo tunatakiwa ku-set standards halafu Mungu ndiyo a-follow-suit kwenye standards hizo? Mistake kubwa ndiyo hiyo kwamba standards huwa tuna-approve sisi na kuanza kuzitumia katika kumu-judge Mungu namna alivyo. Mungu si mjinga angekuwa anatumia standards zetu angekuwa ameshaondoa kabisa kifo kisingekuwepo tena!

Just a hint, spritual science is not emperical science and emperical science has not at any time t, claimed to be the basis of source of every kind of knowledge and hence it cannot expalin all phenomena. Reality transcends empirical knowledge.

Another hint: wakati Albert Einstein akiwa anafanya kazi za utafiti kwa kutumia Laws of classical Physics ambazo zilikuwa developed huko nyuma na wana Fizikia wakali kama akina Isaac Newton na wengine, alikuja kubaini kuwa kuna baadhi ya phenomenal cases hizi laws zina-fail ku-explain, na ndiyo akaja aka-developed special Theory of Relativity iliyo base kwenye Quantum Mechanics, ambazo sasa ziliweza ku-reconcile ile failure ya zile za Classical Mechanics. This proves outright that Emperical Science is still developing and hence it cannot explain everything. Huwezi ukawa uko sahihi kwa kuchanganya maelezo yanayohusu discipline moja ya sayansi na maelezo yake kwenye discipline nyingine tofauti ya Sayansi, hili ndiyo kosa kubwa linalofanyika kwenye mijadala hii. Kwa mfano, hamuwezi mka-reconcile discreapancies kwenye imani mbili let's say Uislam na Ukristo kwa kutumia vyote Quran na Biblia. Kwamba mwislamu atumie Quran na mristo atumie Biblia, haiwezekani, kwa sababu mkifanya hivyo mtakuwa mmekosa standards. Aidha inabidi mu-develop standards nyingine za kutumia au mchague kutumia kitabu kimojawapo kati ya hivyo viwili na si vyote. Hivi vitu viko straightforward na huwa ninashangaa sana ninapoendelea kuona mijadala ya namna hii inazidi kuibuka kila kukicha

Mfano mwingine ni kwamba hayupo mtu hapa dunianai ambaye alishawahi kusema kwamba YESU HAJAWAHI KUWEPO, hayupo na ndiyo maana hata the popular world calendar inatumia BC na AD.However, on the same issue,Spritual Science ina-prove,kwa kutumia tools zake ambazo si sawa na zile za emperical, kuwa alifufuka na kupaa mbinguni(kitu ambacho kupaa hewani against gravity ni impossible badsed on emperical laws of nature)
Sasa mimi nakaa najiuliza maswali nashindwa kuelewa. Huu usomi wa kuwa tunasoma hadi tunafikia kushindwa kuelewa sayansi ipi ni ipi tunauokota wapi? Uwe kwenye emperical sayansi halafu uchukue tools za huko na kuzipeleka kwenye spritual science zikatumike huko, nani kasema kwamba emperical sayansi pekee ndiyo inayoweza ku-explain all phenomena?

Je, wakati tunasoma kwenye Research Methodology kwa mfano, tulifundishwa hivyo? Kwamba utatumia Newton's Laws of Motion kujua IDADI ya wakimbizi wa Rohingya Muslims waliotembea kutoka Mynamar Kwenda Bandladesh kisa walikuwa wanatembea (motion)? Kwamba utatumia IDADI ya watu waliokufa kutokana na radiations za URANIUM kujua RADIO-ACTIVE DECAY au Half life ya Uranium, kwamba idadi ya watu walioathirika itakusaidia kujua ni radiatons kiasi gani zimekuwa emitted na Uranium? Hii mifano miwili naifananisha na mtu anaye-apply tools za emperical science ku-prove mambo kwenye spritual science

Emperical sayansi haina tools amnazo zinaweza kuthibitisha uwepo wa Mungu, na hata wanasayansi wanaosema kuwa MUNGU yupo hawajatumia emperica tools kusema hivyo, na kwa hiyo wanaodai kuwa Mungu hayupo NAO PIA hawawezi kutumia emerical tools kudai hivyo, as simple as that.

Hii issue ya kuwepo au kutokuwepo Mungu is not as complicated and confusing as it appears to be, but rather the complications and confusions arise from the lack of perfect knowledge, when we try to accommodate both the divine knowledge and emperical knoledge STANDARDS, to the LACK OF STANDARDS in our contemporary morality. Kna kitu sisi wabishani hatuna, na hicho ndicho kinatufanya tubishane. Tatizo hapa ni LACK OF STANDARDS, na si Mungu kuwepo au kutokuwepo!

Kwa ufupi mambo ya Mungu yashughulikiwe kiimani, na mambo ya kisayansi yafuate kanuni zake.

Lakini tukirudi kwenye maandiko yako mheshimiwa, tuchukulie mathalan, watu wote dunia nzima wameamua kukubali, kuamini na kusadiki kwamba Mungu yupo, ni Mungu wa aina gani au Mungu yupi?

Namaanisha wale wa Asia watakua na mtazamo ule elu juu ya Mungu kama walionao waliopo Afrika, Ulaya na nchi zingine?
Ni kipi unakichukulia kama msingi bora iwe kiimani au kisayansi (of course jibu itakua kiimani) kuwa ni kitu cha msingi mzuri kwenye kumfanya mtu amjue Mungu au Uwepo wake?

Shukrani
 
Baadhi ya dini zina miungu tofauti tofauti, ila Mungu wa kweli ni mmoja tu. Kinachopelekea watu waamini miungu ni kukosa ufahamu sahihi sasa baada ya kuwa wame-detect uwepo wa Mungu yule ambaye ni mmoja tu. Lakini at least hata yule anayeabudu miungu, anasignify kwa kiwango kikubwa sana kwamba kuna Mungu wa kweli ila ameshindwa tu kwa namna moja ama nyingine, ku-capture the right signal!
 
Back
Top Bottom