Sio tu ukwamo, nje ya IMANI hauwezi kumthibitisha Mungu.
Hapa Mimi nakubaliana na baadhi ya comments kuwa yako mambo huwezi kuyaelezea kisayansi. Mambo kama uwepo wa malaika, uwepo wa majini, uwepo wa uchawi, uwepo wa miujiza. Haya yanaweza kuelezewa kiroho tu.
Lakini pia uwepo wa roho, upendo, chuki, akili (IQ), bado sayansi haiwezi kutuelezea kwa kina kwamba kwa nini mtu mmoja an IQ kubwa na mwingine ana IQ ndogo. Au Fulani ana upendo sana na mwingine ana hasira mara kwa mara na kuwa hivi vinatokana na nini hasa.
Lakini hoja kuwa NJE YA IMANI huwezi kumthibitisha Mungu hapa nitajenga hoja kama Muislam. Natanguliza kujenga hoja kwa aya ndani ya Qur'an kisha nitoe maelezo kwa ufupi.
Mungu anasema katika Surat At-Talaaq aya ya 12.
"
Mwenyezi Mungu nu yule ambaye amezuimba mbingu Saba, na Ardhi kwa mfano wa hizo. Amir zake zinashuka baina Yao, ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba mwenyezi mungu amekizunguka kila kitu kukijua vilivyo kwa elimu yake. (quran 65:12)
Ufafanuzi:
Hapo tumeambiwa Mungu kaumba mbingu saba. Kuna tafsiri mbili hapa na mimi nitatoa moja tu.
Mbingu saba kwa matabaka (Atmosperic layers)
1. Troposphere
2. Stratosphere
3. Ozone Layer
4. Mesosphere
5. Ionosphere
6.Thermosphere
7. Exosphere
Hizo ni major spheres ingawa wanasayansi wamejaribu kuzi-subdivide kama stratopause au tropopause, belts ,nk
Ndani ya hizo layers kuna amri nyingi sana (Commands) kama upepo (kuvuma au kutulia), kupwa na kujaa kwa bahari, kimbunga, photosynthesis, mvua (formation of rains), joto, baridi, Masika, kiangazi, radi, mawingu ya kawaida au ya mvua, mawingu kwenda kasi au kawaida,nk. Na hiyo ni katika Troposphere tu. sijakwambia Ozone layer, repulsion of meteors, x-rays, gamma rays. Nasi humo katika layers tunapata manufaa makubwa sana ya kurusha satellites, kupata mawimbi ya sauti, Simu, radio, TVs, rockets zinapita nk.
Na Ardhi kwa mfano wa hizo:
Hebu nazo tuzione kama kweli zipo saba.
core.
1. Inner Core (Solid)
2. Outer core (Liquid)
Mantle
3. Methosphere
4. Esthenosphere
5. Lisosphere
Crust
6. continental crust
7. oceanic crust
Sijakwambia Amri zinazotoka humo pia kama kupwa na kujaa kwa bahari, aina mbalimbali za udongo, miamba,uoto mbalimbali, madini, maji ya visima, ladha za maji mbalimbali, volcano, landsildes, nk, nk, nk
hizo zote ni amri zinazotoka kwa Allah Muumba. Nasi tunapata Farida kubwa sana humo na Maisha yanaenda.
Na katika hali zote hizo hakuna mwanasayansi aliyetengeneza au kuumba na wala hawezi kubadilisha chochote Zaidi ya kukielezea tu. Cause and effect remain to al-Mighty God and leaves scientists to explain.
Sasa vyovyote watakavyoelezea, wakipatia sawa, wakikosea Mungu kishasema na kufanya. Naye ndiye aliekizunguka kila kitu kwa Elimu (Ujuzi) yake.
Conclusion: Tunaweza kumthibitisha Mungu nje ya Imani.